Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Hili suala la msingi sana..sema kwa serikali hii ya wapigaji sahau.Vita ya uchumi, ni kwenye Chakula na mafuta.
Serikali ifufue TIPER, ni kiwanda Cha refinery ya crude oil. Tena TIPER ifufuliwe haraka mno, tununue crude oil, na kusafisha wenyewe, na kuweka akiba .
Kila Kanda iwe na Reserve...IRINGA/Mbeya, Mwanza, Tanga, na Mtwara.
EWURA ni waongo
Wanasema wanayo akiba ya Siku 19 diesel, halafu hapo hapo mafuta yanapandishwa Bei. Kwa Nini mafuta ya Zamani yauzwe Kwa bei mpya?
Kati ya vitu ambavyo Putin alijipanga vizuri baada ya kuivamia Crimea ni kuweka akiba ya fedha za kigeni kubwa ili kuhakikisha kuwa atakapowekewa vikwazo tena visiwe na effect. Sasa Wakati anaivamia Ukraine, alijuwa kuwa atawekewa vikwazo ila kwa vile alikuwa amejipanga, hakuogopa. Rouble ilipoanguka, akatumia ile akiba aliyokuwa ameweka kuinyanyua rouble tena ingawa calculationa yake haikuwa sahihi sana kwani alittegemea Ukraine kuanduka baada ya muda mfupi tu lakini hali haikuwa hivyo.Tanzania ๐น๐ฟ kama taifa tumekuwa tukijivunia kupanda kwa akiba yetu ya fedha za kigeni na pia tumekuwa tukijivunia kiasi kikubwa cha chakula tulicho nacho kwenye maghala ya kuhifadhi nafaka.
Sijawahi kusikia tukisifia kiasi cha akiba cha mafuta ya nishati ambacho serikali inacho. Tunajua kwamba Marekani ana akiba kubwa ya mafuta kuliko nchi yoyote.
Pia sijawahi kujua kiasi cha akiba cha madini tulichonacho benki kuu, nchi nyingine hiweka akiba ya dhahabu na almasi.
Zaidi ya hayo nchi yangu Tanzania ๐น๐ฟ ina akiba ya vitu gani vingine?