Tanzania tuna protocol za ovyo kabisa kwa Viongozi wetu

Tanzania tuna protocol za ovyo kabisa kwa Viongozi wetu

Yaani kiongozi anashuka kwenye gari anazungukwa na minders zaidi ya hamsini wengine wananing'inia kwenye milango, hadi kiongozi anaenda kukaa jukwaani kaambatana na minders zaidi ya 20 wanamzunguka hadi anakaa na bado kuna wanamsimamia kwa nyuma, kwa hatari gani aliyokuwa nayo kiongozi wa nchi masikini kama Tanzania hadi awe na ulinzi mkubwa kuliko kiongozi wa marekani au uingereza aliyekuwa na bifu kubwa na makundi kibao ya ugadi duniani?
Ni kama hawajui kabisa kuwa siku hizi kuna attacks za kibayolojia na kidigitali
 
Yule jamaa alimnasa vibao kisa mzee Mwinyi anashauri watu watumie Kinga ya kondomu wakati wankujamiiana. Unajua tukio linaweza kutokea tu inapokuwepo chance mwingine anaweza kuamua tu kutafuta umaarufu.
Kama yule aliyemrushia Bush viatu jukwaani
 
Sasa umemtaja kama kiongozi au kama raia. Maana mwinyi aliacha uongozi 1995.
We huelewi nilichoandika, watanzania wengi ndio mpo hivi na unaweza kukuta una degree au masters kabisa🤷 rudia kusoma nilichoandika maana unazidi kuhama nilichoandika, shida kweli. Otherwise nipotezee tu sio lazima uniquote .
 
We huelewi nilichoandika, watanzania wengi ndio mpo hivi na unaweza kukuta una degree au masters kabisa[emoji1745] rudia kusoma nilichoandika maana unazidi kuhama nilichoandika, shida kweli. Otherwise nipotezee tu sio lazima uniquote .
Kwani wewe mwenyewe ukisoma ulichoandika unaelewa chochote pale? Nimesoma sentence ya mwanzo tuu kilichofuata nimechoka kusoma naona corrugations tu.
 
Yaani kiongozi anashuka kwenye gari anazungukwa na minders zaidi ya hamsini wengine wananing'inia kwenye milango, hadi kiongozi anaenda kukaa jukwaani kaambatana na minders zaidi ya 20 wanamzunguka hadi anakaa na bado kuna wanamsimamia kwa nyuma, kwa hatari gani aliyokuwa nayo kiongozi wa nchi masikini kama Tanzania hadi awe na ulinzi mkubwa kuliko kiongozi wa marekani au uingereza aliyekuwa na bifu kubwa na makundi kibao ya ugadi duniani?

Yaani unashangaa Joe Biden anshuka kwenye gari hadi anaenda kukaa jukwaani Yuko peke yake na mke wake na hadi anakaa hakuna jitu lina mpumulia nyuma.

Unashangaa hata malkia wa uingereza anashuka kwenye range rover yuko peke yake na kibegi chake kiwikoni anatembea zake hajazongwa na kundi la wapambe wala ushuzi ila sasa sisi watanzania sijui ni nani alianzisha utaratibu huu wa ajabu kwa viongozi wetu kuandamana na utitiri wa watu Hadi wengine wamevaa magwanda kijeshi na mabunduki nje nje hii kitu haikuwepo enzi za nyerere wala mwinyi.

Sijui ni nani aliingiza utaratibu wa kuonesha kana kwamba kiongozi ana maadui wengi kiasi cha kuhitaji idadi kubwa ya kutisha ya wapambe na mibunduki hadharani ambapo zamani silaha ulikua huzioni hadhara kwa viongozi ila unahadithiwa zipo viunoni.

Nahisi kuna watu wanaohusika walianzisha utaratibu wa kuajili ndugu zao kwa kuwajaza kwa viongozi mpaka ikaja kuwa normal kwa viongozi kuzungukwa na wapambe wengi kupita uhitaji.
Cha kushangaa hata katibu mkuu wa ccm eti nae ana ulinzi ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom