Tanzania tunaathirika na udhaifu wa fikra (Inferiority Complex) wa viongozi wetu wakuu

Kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Tulipaswa kuliamsha dude la maandamano nchi isitwalike. Lkn kwa ujinga huu wa wadanganyika tutaburuzwa sana
Nani wa kuandamana! Si mliambiwa na Lisu muingie barabarani mbona hamkutoka, mavi ya kuku. Chadema yenu matusi tu, endeleeni kususa.
 
Chanzo cha tatizo ni CCM, ili kuficha mapungufu ya kiutendaji ya wakuu wa mihimili yote ya dola na uwajibikaji wao, kwa hiyo wameona ni vyema kubadilisha matakwa ya sheria na kuwapa wote kinga ya kutokushitakiwa.

Hapo ndipo wabunge wa CCM walipofanya kosa kubwa. Na hicho ndicho chanzo cha kulindana hata kama wakuu hao wanafanya mambo ya hovyo kabisa.

Ayubu kwa kutambua kuwa ana kinga ya kutoshitakiwa baada ya kumaliza uongozi wake wa Bunge, ndiyo maana ana kiburi cha kuwalea hao wabunge 19 wajulikanao kama COVID 19.
Dhambi hii watailipia hapa hapa duniani!
 
Nani wa kuandamana! Si mliambiwa na Lisu muingie barabarani mbona hamkutoka, mavi ya kuku. Chadema yenu matusi tu, endeleeni kususa.
Kamuulize Gwajiboy, Polepole au Ndugai. Bora hata sisi tunatype mtandaoni.😅😅
 
Mkuu Ileje , hili la inferiority complex kwa viongozi wetu, niliwahi izungumza humu

Hili pia la makabila inferior na makabila superior pia niliwahi kulizungumzia humu,

ila pia nilizungumzia tatizo fulani la watu wafupi...

Heri ya mwaka mpya
P
Heri na kwako pia. You are ahead Times always
 
Chanzo cha tatizo ni CCM, ili kuficha mapungufu ya kiutendaji ya wakuu wa mihimili yote ya dola na uwajibikaji wao, kwa hiyo wameona ni vyema kubadilisha matakwa ya sheria na kuwapa wote kinga ya kutokushitakiwa.

Hapo ndipo wabunge wa CCM walipofanya kosa kubwa. Na hicho ndicho chanzo cha kulindana hata kama wakuu hao wanafanya mambo ya hovyo kabisa.

Ayubu kwa kutambua kuwa ana kinga ya kutoshitakiwa baada ya kumaliza uongozi wake wa Bunge, ndiyo maana ana kiburi cha kuwalea hao wabunge 19 wajulikanao kama COVID 19.
Hatuko serious kama nchi,serikali inajali maslahi ya wakubwa wachache, kwamba wao hata wavurunde vipi hakuna kushtakiwa,
Ila mtumishi mdogo akipoteza elfu hamsini ashitakiwe,
Tuna manga manga tu
 
Tukianza na Rais yeye anafikiri kuna watu wanamdharau kwa kuwa yeye ni mwanamke. Mawazo haya amekuwa nayo hata kabla hajaapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Na mara baada ya kuapishwa hotuba yake rasmi kama Rais alitamka kwa msisitizo kuwa yeye ni Rais mwanamke! Hali iliyoashiria kuwaonya wale waliomuona kama ni mwanamke na siyo kiongozi! Kutokana na fikra hizo alizonazo amekuwa akifanya maamuzi yasiyo sahihi anapokosolewa kisiasa na katika utendaji wake na viongozi hasa wa upinzani! Hili ameonyesha wazi kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Mbowe kuwa anamdharau. Lakini pia ameonyesha jinsi anavyohamaki akikosolewa na viongozi wenzake ndani ya CCM.

Kiongozi wa pili mwenye matatizo haya ni Spika Ndugai ambaye anaona anashambuliwa katika mitandao ya jamii na pia kudharaulika na viongozi wenzake kwa sababu eti yeye ni MGOGO kwa kabila. Kwamba angekuwa anatoka kabila jingine yasingemkuta hayo madharau! Kutokana na hili na kwa kuwa anataka kuonyesha kuwa na wagogo wanaweza amekuwa akifanya na kuamua mambo kinyume cha Katiba na kuvunja sheria. Mambo haya aliyaonyesha kwa namna alivyoendesha bunge la serikali ya awamu ya tano kwa kuwanyanyasa wabunge wa Chadema kwa kuwafukuza hovyo kadri alivyojisikia. Aidha ameendeleza jambo hili la kuvunja Katiba na sheria kwa namna anavyoendelea kuwalea wabunge wasio na chama maarufu civid-19. Kwa sasa udhaifu wake wa fikra umepelekea aanze kukabiliana na wanachama wenzake wa CCM.

Wa tatu ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma ambaye baada ya kugundua hatoshi katika nafasi hiyo ameamua kujinyenyekeza kwa serikali, badala ya kulinda Katiba na sheria za nchi kwa kutenda na kuamua kwa haki masuala ya kisheria anafanya vile serikali inavyotaka! Hii ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Taifa kwani mahakama sasa imekuwa chombo cha kugandamiza wananchi! Uhuru wa mahakama umetekwa na serikali na sasa muhimili yote mitatu ya dola; serikali, mahakama na bunge inashirikiana kuvunja Katiba na sheria! Viongozi wanafanya na kuamua wanavyotaka wenyewe bila kuheshimu katiba na sheria.

Wananchi tumebaki na jambo moja tu la kufanya, nalo ni kuendelea kupiga kelele na kuwazomea viongozi hawa kwa kadri tutakavyoweza hadi watakapojirekebisha kwani hatuna namna nyingine ya kufanya. Midomo yetu ndiyo silaha yetu!
Kila anayeshikilia usukani anashikwa na jinamizi la hofu ya ccm kufia mikononi mwake. Hivyo litafanywa lolote zuri au la ccm isife. Hao wabunge 19 wasio na chama ni mfano wote wamekaa kimya ila mmoja wao kalisema na bado ni kimya tu.
Kitu chochote ni chema tu ili mradi kinahakikisha maisha ccm. Hawajui kuwa kuimarika kwa ccm kuna uhusiano na kuimarika kwa upinzani. Hivyo kuua upinza ni ni jaribio la kuua ccm na hii imeanza dalili.
 
Kama CCM inataka kuua upinzani ibadilishe katiba turudi katika mfumo wa chama kimoja!
 
Mna mjaribu sana...

Yeye ni mama nanyie ni vijana...
Mkimzingua anawazingua...
 
Alichokionyesha Spika Ndugai leo wakati akimwomba radhi Rais Samia kwa kauli yake kuwa nchi itapigwa mnada kwa sababu ya mikopo si udhaifu wa fikra tu bali pia njaa na uoga wa kukosa madaraka! Aidha kitendo hiki kimeonyesha dhahiri namna ambavyo mihimili ya dola ya bunge na mahakama haiko huru!
 
Wa nne ni yule aliye amua kujiita jiwe. Hiyo ndiyo pure inferiority complexity. Ukali mwingi na kujihami kwingi.
Achana na marehemu huenda naye ulimuelewa vibaya tu,lkn hawezi kujitetea.
 
Alichokionyesha Spika Ndugai leo wakati akimwomba radhi Rais Samia kwa kauli yake kuwa nchi itapigwa mnada kwa sababu ya mikopo si udhaifu wa fikra tu bali pia njaa na uoga wa kukosa madaraka! Aidha kitendo hiki kimeonyesha dhahiri namna ambavyo mihimili ya dola ya bunge na mahakama haiko huru!
Ugali wa bure mtamu.
 
Nani wa kuandamana! Si mliambiwa na Lisu muingie barabarani mbona hamkutoka, mavi ya kuku. Chadema yenu matusi tu, endeleeni kususa.
Acha kuharibu mada kwa kuleta matusi kwa chama Cha siasa. Mada inaongelea inferiority complex ya Viongozi wakuu wewe unaitukana CHADEMA matusi. Tanzania Ni zaidi ya chama Cha siasa wewe Kama bado unaabudu vyama vya siasa shauri yako. Linapotokea suala la kitaifa week uchama pembeni kabisa.
 
Achana naye huyo! Hao ndiyo wakipewa vyeo wako tayari kwenda kusaidia kusafisha vyombo kwa mabosi wao!
 
Ugali wa bure mtamu.
Ndiyo sababu Ndugai akipata mtu wa kumnyanyasa anavimba hasa kwa sababu ni dhaifu mno mbele ya wanaoweza kumng'oa madarakani! Hivyo analipiza kisasi kwa wanyonge wake ili anyenyekewe!
 
Tukianza na Rais yeye anafikiri kuna watu wanamdharau kwa kuwa yeye ni mwanamke. Mawazo haya amekuwa nayo hata kabla hajaapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Na mara baada ya kuapishwa hotuba yake rasmi kama Rais alitamka kwa msisitizo kuwa yeye ni Rais mwanamke! Hali iliyoashiria kuwaonya wale waliomuona kama ni mwanamke na siyo kiongozi! Kutokana na fikra hizo alizonazo amekuwa akifanya maamuzi yasiyo sahihi anapokosolewa kisiasa na katika utendaji wake na viongozi hasa wa upinzani! Hili ameonyesha wazi kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Mbowe kuwa anamdharau. Lakini pia ameonyesha jinsi anavyohamaki akikosolewa na viongozi wenzake ndani ya CCM.

Kiongozi wa pili mwenye matatizo haya ni Spika Ndugai ambaye anaona anashambuliwa katika mitandao ya jamii na pia kudharaulika na viongozi wenzake kwa sababu eti yeye ni MGOGO kwa kabila. Kwamba angekuwa anatoka kabila jingine yasingemkuta hayo madharau! Kutokana na hili na kwa kuwa anataka kuonyesha kuwa na wagogo wanaweza amekuwa akifanya na kuamua mambo kinyume cha Katiba na kuvunja sheria. Mambo haya aliyaonyesha kwa namna alivyoendesha bunge la serikali ya awamu ya tano kwa kuwanyanyasa wabunge wa Chadema kwa kuwafukuza hovyo kadri alivyojisikia. Aidha ameendeleza jambo hili la kuvunja Katiba na sheria kwa namna anavyoendelea kuwalea wabunge wasio na chama maarufu civid-19. Kwa sasa udhaifu wake wa fikra umepelekea aanze kukabiliana na wanachama wenzake wa CCM.

Wa tatu ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma ambaye baada ya kugundua hatoshi katika nafasi hiyo ameamua kujinyenyekeza kwa serikali, badala ya kulinda Katiba na sheria za nchi kwa kutenda na kuamua kwa haki masuala ya kisheria anafanya vile serikali inavyotaka! Hii ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Taifa kwani mahakama sasa imekuwa chombo cha kugandamiza wananchi! Uhuru wa mahakama umetekwa na serikali na sasa muhimili yote mitatu ya dola; serikali, mahakama na bunge inashirikiana kuvunja Katiba na sheria! Viongozi wanafanya na kuamua wanavyotaka wenyewe bila kuheshimu katiba na sheria.

Wananchi tumebaki na jambo moja tu la kufanya, nalo ni kuendelea kupiga kelele na kuwazomea viongozi hawa kwa kadri tutakavyoweza hadi watakapojirekebisha kwani hatuna namna nyingine ya kufanya. Midomo yetu ndiyo silaha yetu!
Tatizo hili lililetwa na rais kulaza mwenye elimu ya dukani alipofikiri kuwa anadharauliwa kwa ukilaza wake. Matokeo yakebl kila mtu aliyaona
 
Agenda ya mikopo ya pupa ipo kwenye kuiendeleza zanzibar iwe kama dubai....
 
Kwa hoja hiyo ipo haja ya katiba mpya ili Zanzibar iwe na uwezo wa kukopa yenyewe au la sivyo Zanzibar iwe na benki kuu yake!
 
Back
Top Bottom