Tanzania tunawazidi Kenya katika mambo mengi, jambo la msingi tuendelee kuheshimiana

Tanzania tunawazidi Kenya katika mambo mengi, jambo la msingi tuendelee kuheshimiana

Yaani tumekuwa taifa la wabaguzi mpaka inatia huruma sio siku nyingi tuanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe
Sisi tulianza kubaguana kwanza halafu tumefuatia kuwabagua majirani. Huoni wanaCCM humu wanawaita Wakenya Mbwa?
 
Hatuwezi kupata soko jingine nje ya nchi kwa sababu Kenya wamesema Kwenye taarifa yao wamesema mahindi kutoka Tanzania yana sumu kuvu (aflatoxin) inayosababisha kansa. Sasa ni nchi gani itakubali kununua mahindi yetu watu wake wakaugue kansa?

Hili jambo ni matokeo ya uongozi wetu kuwa na kauli za kijinga kila wakati
Si kauli tu, serikali yetu kila kitu kimebinafisishwa na siasa, taaluma zimesiginwa. Wataalamu wa kilimo hawana mchango katika uzalishaji mazao. Wako maofini, wakulima wanajihangaikia kivyao. Matokeo ndio kupata mazao duni na yasio kidhi viwango.
 
Hoja kwamba tutauza nchi zingine nayo ni kujipa matumaini tu. Mbona 2017 tulihangaika kutafuta soko hadi mahindi yakaharibika? Hizo nchi zingine hazikuwepo? Tusitoe majibu mepesi kwa maswali magumu. Manji alipoacha kununua Mbaazi tulisema serikali itanunua na kupeleka huko anakopelekaga Manji. Lakini nini kilitokea? Bei imeporomoka kutoka 3,000/= hadi TZS 200/= kwa kilo. Korosho mnakumbuka pia kilichotokea? Kwahiyo tusijipe matumaini. Hali itakua mbaya.

Hili jambo uelewi lolote.

Kauli za kijinga za viongozi wetu ndio matokeo yake
Na wakikwama wanajikausha kama hawajawahi ongelea jambo kama hilo. Lina ulisikia tena serikali ikiongelea soko la mbaazi na korosho, kimya!
 
Naona kidogokidogo Kenya watengeneza mazingira ya "grey zone".

Je, ni maslahi yepi Kenya wanayatafuta kwa kufanya hizi operations?
 
Kenya inaitegemea zaidi Tanzania katika nyanja mbalimbali kuliko Tanzania inavyoitegemea Kenya katika mambo machache sana hasa soko la nafaka na matunda.

Ni vema tukaendelea kuheshimiana maana aliyeshika mpini anajulikana.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
Kutokana na 'comparative & competitive advantages" kila nchi imejaliwa kuwa na vitu muhimu ambapo nyingine haina. Kwa hiyo kila nchi hunufaika kiuchumi kupitia mahusiano mema ya nchi moja na nyingine.

Katika suala hili ni lazima zitumike njia za kidiplomasia ili kurudisha mahusiano mema na yenye kufanya nchi hizi mbili kuzidi kuaminiana ktk masuala ya kibiashara. Sidhani kama ni busara kuanza kuendekeza chuki za wazi, kejeli na vita vya maneno, ni mambo ambayo kwa hakika hayasaidii kitu chochote kile.
 
Kenya inaitegemea zaidi Tanzania katika nyanja mbalimbali kuliko Tanzania inavyoitegemea Kenya katika mambo machache sana hasa soko la nafaka na matunda.

Ni vema tukaendelea kuheshimiana maana aliyeshika mpini anajulikana.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
Bwashee anzia Tarakea mpaka kwenu Marangu bidhaa karibu zote zinatoka Kenya
Huko tv na mitandao ni ya Kenya
 
Bwashee anzia Tarakea mpaka kwenu Marangu bidhaa karibu zote zinatoka Kenya
Huko tv na mitandao ni ya Kenya
Bwashee ndio maana nimekuambia Kenya inaitegemea zaidi Tanzania.

Mimi niko hapa Usseri Rombo bidhaa zote zinatoka Kenya!
 
SUMUKUVU ni kemikali zinazozalishwa na aina za fangasi /ukungu/kuvu wanaoota kwenye punje za nafaka, mbegu za mafuta, mikunde na mazao ya mizizi

Mahindi na unga wake na karanga na bidhaa zake huathiriwa zaidi na sumukuvu. Mazao mengine ni korosho, muhogo, alizeti, mtama na mchele.
SUMUKUVU pia hupatikana katika bidhaa za mifugo kama vile mayai, nyama na maziwa iwapo watakula chakula kilichochafuliwa na sumu
Hupatikana katika maziwa ya mama anayenyonyesha iwapo atakula chakula chenye sumu kuvu


Kuna SUMUKUVU za aina nyingi kulingana na kuvu anayezalisha sumu hiyo, mfano kwa mahindi aflatoxin, fumonisins, and ochratoxin ndiyo za muhimu zaidi.
SUMUKUVU hazionekani kwa macho, hazina harufu, ladha wala rangi. Lakini kuvu wanaozalisha sumu kuvu wanaweza kuwa na rangi kama vile kijani, kijivu, njano chafu au machungwa.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Huchagui jirani lakini kuwa jirani na Kenya ni bahati mbaya Mungu alitupa. Kenya ni washamba.. Wajuaji.. Pro wazungu.. Wana roho mbaya.. Ningekuwa mm Rais ningeimarisha uhusiano na nchi za sadc sana.. Hasa Zambia.. Mozambique.. Kuliko Kenya.. Mbwa hawa
Nilitaka kukuita mpumbavu nikaona haitatosha nikaamua kuacha.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Kwa taarifa kenya wanafanya biashara kubwa sana ya matunda wanayonunua toka tanzania kwa sababu wametuzidi hata akili.
Wananunua kwetu bei chee wanafanya packing nzuri wanauza ulaya na uarabuni.
Sasa how tanzania tuwe vizuri wakati hata biashara tunayofanya na kenya wanatulalia
Kenya inaitegemea zaidi Tanzania katika nyanja mbalimbali kuliko Tanzania inavyoitegemea Kenya katika mambo machache sana hasa soko la nafaka na matunda.

Ni vema tukaendelea kuheshimiana maana aliyeshika mpini anajulikana.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
 
hii serikali yetu ya washamba inaamini kila mtu nje ya tz ni adui, wajinga sana!.
 
Kwa taarifa kenya wanafanya biashara kubwa sana ya matunda wanayonunua toka tanzania kwa sababu wametuzidi hata akili.
Wananunua kwetu bei chee wanafanya packing nzuri wanauza ulaya na uarabuni.
Sasa how tanzania tuwe vizuri wakati hata biashara tunayofanya na kenya wanatulalia
Nimesema wanatutegemea uwe unaelewa bwashee!
 
Back
Top Bottom