Tanzania tunawazidi Kenya katika mambo mengi, jambo la msingi tuendelee kuheshimiana

Kauli kama ipi iliyosababisha Kenya kufanya hivyo?

Ni kweli Kenya imekua tegemezi kwa mazao ya nafaka kutoka Tanzania tangu uhuru. Kuna watu wanadhani utegemezi huo hauwezi kuisha. Si kweli!!
 
Ukiongea kwa kichaga huwa unaeleweka vizuri na bavicha wenzako bwashee!
 
Humu JF watu hamuendi na wakati, mnailaumu Kenya kwa kuyakataa mahindi yenye sumu kuvu wakati huohuo Uganda inatulaumu kwa sisi kuwakatalia bidhaa zake kuuzwa nchini mwetu! Hili watanzania wengi wataona ni sawa tu.
 
Watanzania tunapenda kujifariji kwa kauli za ajabu sana.
Ujinga na upumbavu mtupu umetujaa. Wataona sasa kuanzia mbao,mazao. Mahindi sasa hizi yanaliwa na wadudu ndani,yamekosa soko kabisa,wakulima wanalia mazao kukosa soko na kushuka bei. Mijitu bado haijui kama hili lililoleta tred kwamba sababu yote ni vita yetu ya chini chini na Kenya. Kenya sasa watapata sehemu nyingine ya kununua mazao. Tukiendelea na huu ujinga tutajua kwa kupeleka hayo mazao. Hakuna sababu kabisa ya kujiona tunajua,kuna haja gani ya kujimwambafai?. Kiuhalisia Kenya wametutangulia hatua 10 mbele kwa mambo mengi
 
Tanzania ambayo inajulikana kama The Sleeping Giant of East Africa inasumbuliwa na Inferiority Complex kwa Kenya.

Tanzania pamoja na kuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi kama Kenya lakini bado wako nyuma ya Kenya kwa mambo mengi ikiwemo Uchumi, Elimu, Demokrasia nk.
 

Mkuu, mimi nimezungumzia masuala ya kwenye grass root - labda nirudie kuuliza swali langu: Nime hoji hivi: Je,umewahi kutembelea vijiji vya Kenya ambako ndiko watu wana ishi kwa mwingi ukashuhudia maisha yao alisi yalivyo?

Mkuu, usichukulie takwimu za kibajeti kama ndio barometer /mwarobaini wa kuonyesha kiundani kila kitu.

Ukweli unabaki kwamba linapo kuja suala la Gap kati ya Kenyans HAVE and HAVE NOT inatisha asikwambie mtu - je, Tanzania hali hiko hivyo???? Labda tuanzie hapo kudadavua.
 
Ujinga upi sasa mbona huutaji?
 
Hata sisi wana bidhaa zao hapa subiri tutawajibu
 
Aacha uzushi hizo data umezitoa wapi ? GDP ya kenya 70bln na Tz ni 50bln.
 
Jirani YAKO awe maskini au tajiri jua mnategemeana hakuna Cha kumzidi, upatapo majanga ndo wa kwanza kukukimbilia kabla ya ndugu
So kusema kenya tunawazidi mengi ni hoja usiokua na mashiko,na je Kama mnawazidi mengi why pesa yao ipo stable kuliko yetu, sisi tunakwama wapi wakati tunawazidi mengi, binafsi sitaki tz tukwazane na majirani zetu ,haina maana yoyote ,Kama Wanasema mahindi yetu Yana aflotoxic ,sum hasa itokanayo na kutunza mazao vibaya,ikiwemo karanga Basi wizara ya kilimo ije na mikakati ya kulimisha wakulima namna bora ya kutunza vizuri mazao yao
 
Yo
You lie yourself
 
Well done
 
Tabia ya kujifananisha au kujilinganisha na Kenya,Uganda au nchi yoyote tunayoshiriki mipaka nazo ni kukosa Dira..maana zote ni nchi zenye maendeleo madogo(nchi zinazoendelea) sisi tunapaswa kujifunza kuboresha mipango yetu sisi kwa kuzingatia vigezo vinavyopima uchumi na ustawi wa jamii.
 
Vijiji vya nchi zote viko sawa, vyote vina watu wasiopata chakula, maji, elimu na huduma za Afya. Tembelea huko Singida kwa wairaki, hawana nyumba wanaishi kwenye mapango, hawana chakula wanaishi kwa kuwinda na kuhemea asali na matunda ya porini, hawana nguo wala maji na hakuna shule wala hawazijui pia lugha yao ni yao tu wewe huwezi kuielewa, hawa maisha yao huenda ni ya chini sana Afrika Mashariki.
 

Unamanisha kauli za viongozi wetu ndo zimesababisha mahindi yawe na sumu
 
Bila statistics itakuwa ni uganga wa kienyeji tu. Hao maskini wa Kenya unaowataka kuwaongelea vijijini wako Africa nzima hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…