Ni wazi sasa Tanzania ingekuwa mbali sana kama tungekuwa na vyama pinzani ambavyo ni 50/50 kuliko sasa nchi yetu iko chini ya udikteta wa walarushwa nawabinafsi wa CCM.
Tungekuwa mbele kwenye haya
1. Tungekuwa na katiba mpya ambayo inajali maendelo
2. Tungekuwa na mifumo isiyotegemea rushwa kama sasa hata Muktasari wa shamba ni rushwa
3. Tungekuwa na usalama na Polisi inayofanya kazi kuhudumia watu sio chama
4. Tungekuwa na mikataba iliyo wazi
5. Tusingekuwa na upendeleo wa ndugu kwenye kazi za serikali
6. Tusingekuwa na utekaji wa kisiasa kama sasa
7. Tusingekuwa na matumizi mabaya ya serikali kama sasa
8. Tusingekuwa na Machawa kama sasa badala yake tungekuwa na washauri
9. Tusingekuwa na Uzanzibari na Utanganyika kama katiba ingekuwa nzuri
10. Tungekuwa na uchumi mkubwa zaidi ya sasa
Kwa yote haya. Ili tubadilike ni lazima tupate viongozi ambao wako tayari kupunguza nguvu zao wenyewe na za chama na kujali mifumo na nchi.
Kiongozi wa hizi bado hatuna hata Magufuli alikuwa na umimi sana na kushikia watu wengine bila sababu pamoja na mazuri yake. Tuombeeni tupate viongozi wenye uzalendo wa kweli