Tanzania tupo kwenye mfumo wa chama kimoja ulioshirikisha vyama vingi

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Ni uongo kusema ya kwamba Tanzania inafuata mfumo wa vyama vingi. Ni kwamba serikali ya Mwinyi ya mwaka 1992 iliruhusu uwepo wa vyama vingi ndani ya mfumo wa chama kimoja. Na hili ndio tatizo, vyama vingi vipo ila mfumo ni wa chama kimoja.

Ili mfumo uitwe wa vyama vingi inatakiwa yafuatayo yafanywe.

1. Vyombo vya Dola viwe neutral visiegemee upande wowote. Ukija Tanzania vyombo vya Dola vipo kwaajili ya kulinda CCM isiondolewe madarakani kwa kura. Pia vipo kwaajili ya kuviumiza vyama pinzani. Kwa mfano Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA alipigwa risasi ila hakuna aliyeingilia kati kupeleleza hata kukamatwa kwa wahusika. Angalia Mwanachama wa CHADEMA Ally Kibao kauawa baada ya kutekwa mchana kweupe na Rais akasema kuwa kifo ni kifo, kisa aliyeuawa ni mfuasi wa upinzani.

2. Spika wa Bunge kutolalia upande wowote:
Ili tuwe kwenye mfumo wa vyama vingi inatakiwa Spika asiwe na upande wowote. Kwa Sasa Tanzania bunge limekuwa Kama mkutano wa chama tawala CCM. Spika ndio anapanga Nini lipitishwe na kipi kisipitishwe. Kwa mfano tuliona Spika akilazimsha mkataba wa DP World upite bungeni. Wabunge walioonesha kupinga Spika aliwahoji maswali na kuwadhihaki kana kwamba hawajui wanachosema. Kwa mfano Bunge kupitia Spika lilikataa kujadili kuhusu kupotea na kutekwa kwa vijana wa upinzani wakiongozwa na Soka. Lakini naamini ingekuwa ni vijana wa CCM wamepotezwa na kutekwa Bunge lingesimama kujadili lakini kwasababu ni wa upinzani hakuna haja ya kujadili.

3. Vyombo vya habari vya umma kutokuwa huru:
Kwa Sasa vyombo vya habari vya umma vimekuwa vikiegemea upande mmoja wa serikali na chama tawala. Na kusahau kwamba ni vyombo vya habari vya umma vinavotakiwa visitor upendeleo Kwa chama chochote Cha siasa. Ila ukienda TBC na magazeti ya serikali ambayo ni mashirika ya umma yanayoendeshwa Kwa Kodi ya wananchi lakini yanaegemea upande mmoja. Inatakiwa TBC irushe mikutano ya CHADEMA, ACT, CUF etc Bure bila vikwazo ila Hilo halifanyiki.

4. Mfumo wa utawala:
Kwenye mfumo wetu wa utawala Viongozi wa juu wamefungamana na chama. Kwenye mfumo wa vyama vingi, chama kinachoshinda kinatakiwa kuwastaafisha Viongozi wote wa chama watakao hudumu kwenye nafasi za uongozi wa serikali.

Lakini Kwa Tanzania ni shida, Rais ndio mwenyekiti wa chama, Spika, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ni wajumbe kamati kuu. Hapo unategemea nini?. Kila kiongozi atalinda maslahi ya chama bila kuangalia uwepo wa vyama vingine. Pale Madagascar , uchaguzi unapokaribia, Rais anastaafu na kumuachia Jaji Mkuu nafasi ya kusimamia uchaguzi. Huwezi kuwa Rais na bado mgombea urais na hapo hapo una mamalaka na Tume ya Uchaguzi. Wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya Hali ni hiyo hiyo. Na kila mkuu wa Mkoa na Wilaya yupo kwaajili ya kuhakikisha chama Cha upinzani hakipati ushindi.

Kuna sababu lukuki kuonesha kuwa tupo kwenye mfumo wa chama kimoja , hasa Tume ya Uchaguzi ndio tatizo kubwa Sana. Bado inafanya kazi na wakurugenzi waliotokana na chama tawala kusimamia uchaguzi wilayani.

Nadhani Mfumo wa vyama vingi utakuja baada ya miaka hamsini ijayo. Kitakapo patikana kizazi kipya kisichokuwa na uchawa tulionao Leo.
 
Ni uongo kusema ya kwamba Tanzania inafuata mfumo wa vyama vingi. Ni kwamba serikali ya Mwinyi ya mwaka 1992 iliruhusu uwepo wa vyama vingi ndani ya mfumo wa chama kimoja. Na hili ndio tatizo, vyama vingi vipo ila mfumo ni wa chama kimoja.
Huu ni ukweli kabisa。Tumeingia vyama vingi kwa katiba ya chama kimoja!。Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla
Ili mfumo uitwe wa vyama vingi inatakiwa yafuatayo yafanywe.

1. Vyombo vya Dola viwe neutral visiegemee upande wowote. Ukija Tanzania vyombo vya Dola vipo kwaajili ya kulinda CCM isiondolewe madarakani kwa kura. Pia vipo kwaajili ya kuviumiza vyama pinzani. Kwa mfano Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA alipigwa risasi ila hakuna aliyeingilia kati kupeleleza hata kukamatwa kwa wahusika. Angalia Mwanachama wa CHADEMA Ally Kibao kauawa baada ya kutekwa mchana kweupe na Rais akasema kuwa kifo ni kifo, kisa aliyeuawa ni mfuasi wa upinzani.
true,hakuna mafunzo yoyote ya change of arms kwa vyombo vya dola kutumikia chama kingine chochote zaidi ya CCM Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?!
2. Spika wa Bunge kutolalia upande wowote:
Ili tuwe kwenye mfumo wa vyama vingi inatakiwa Spika asiwe na upande wowote. Kwa Sasa Tanzania bunge limekuwa Kama mkutano wa chama tawala CCM. Spika ndio anapanga Nini lipitishwe na kipi kisipitishwe. Kwa mfano tuliona Spika akilazimsha mkataba wa DP World upite bungeni. Wabunge walioonesha kupinga Spika aliwahoji maswali na kuwadhihaki kana kwamba hawajui wanachosema. Kwa mfano Bunge kupitia Spika lilikataa kujadili kuhusu kupotea na kutekwa kwa vijana wa upinzani wakiongozwa na Soka. Lakini naamini ingekuwa ni vijana wa CCM wamepotezwa na kutekwa Bunge lingesimama kujadili lakini kwasababu ni wa upinzani hakuna haja ya kujadili.
Naunga mkono hoja,spika asiwe kada Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?
3. Vyombo vya habari vya umma kutokuwa huru:
Kwa Sasa vyombo vya habari vya umma vimekuwa vikiegemea upande mmoja wa serikali na chama tawala. Na kusahau kwamba ni vyombo vya habari vya umma vinavotakiwa visitor upendeleo Kwa chama chochote Cha siasa. Ila ukienda TBC na magazeti ya serikali ambayo ni mashirika ya umma yanayoendeshwa Kwa Kodi ya wananchi lakini yanaegemea upande mmoja. Inatakiwa TBC irushe mikutano ya CHADEMA, ACT, CUF etc Bure bila vikwazo ila Hilo halifanyiki.
Kwa hili,naomba kuitetea TBC Kampeni UKAWA: Mnyonge Mnyongeni!, TBC, Inastahili Pongezi!, Jana Imefanya Kazi Nzuri Iliyotukuka!
ile 2010,kila kilipopita kipindi cha mchakato majimboni,CCM ilipigwa chini!,baada ya uchaguzi,Tido naye akapigwa chini!。
4. Mfumo wa utawala:
Kwenye mfumo wetu wa utawala Viongozi wa juu wamefungamana na chama. Kwenye mfumo wa vyama vingi, chama kinachoshinda kinatakiwa kuwastaafisha Viongozi wote wa chama watakao hudumu kwenye nafasi za uongozi wa serikali.
hili tumeliongea sana humu,
Lakini Kwa Tanzania ni shida, Rais ndio mwenyekiti wa chama, Spika, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ni wajumbe kamati kuu. Hapo unategemea nini?. Kila kiongozi atalinda maslahi ya chama bila kuangalia uwepo wa vyama vingine.
true
Pale Madagascar , uchaguzi unapokaribia, Rais anastaafu na kumuachia Jaji Mkuu nafasi ya kusimamia uchaguzi. Huwezi kuwa Rais na bado mgombea urais na hapo hapo una mamalaka na Tume ya Uchaguzi.
true,mgombea mmoja ni dola anashindana na makapuku
Wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya Hali ni hiyo hiyo. Na kila mkuu wa Mkoa na Wilaya yupo kwaajili ya kuhakikisha chama Cha upinzani hakipati ushindi.
true,this is wrong
Kuna sababu lukuki kuonesha kuwa tupo kwenye mfumo wa chama kimoja , hasa Tume ya Uchaguzi ndio tatizo kubwa Sana. Bado inafanya kazi na wakurugenzi waliotokana na chama tawala kusimamia uchaguzi wilayani.
true
Nadhani Mfumo wa vyama vingi utakuja baada ya miaka hamsini ijayo. Kitakapo patikana kizazi kipya kisichokuwa na uchawa tulionao Leo.
not necessarily hadi miaka 50,kwa vile CCM
inamsimamisha mgombea mwanamke 2025,Tundu Lissu akisimama kama mgombea wa pamoja wa upinzani,halafu ikapigwa kampeni kamambe ya compare and contrast Samia na Lissu,2025 watu wanapindua meza!,tatizo ni ule ukweli Nape kuhusu chaguzi zetu!Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
 
Back
Top Bottom