Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Wamachinga wapambanishwe na walimu.. mawaziri na kina sanga store KariakooNdio maana nimeuliza kujiajiri katika angle ipi ya ujasiriamali
Mi ninachoamini kila mtu ana namna yake ya kutoka kimaisha.mbona mnakopa kopa kwa waliojiajiri sasa?kama kuajiriwa na serikali raha?.na mikausha damu inawatafuna vizuri,muuza vitumbua ,amejenga na anasomesha,we ulieajiriwa na serikali unazeekea kwenye nyumba za kota
HahahahhaUkifa mtoto wako ataendelea kupokea mshahara wako?
Hata aliyeajiriwa anakua pia. Kuna annual increment (japo ni ndogo), kuna kupanda cheo.. kuna kuhama taasisi kuhamia taasisi inayolipa zaidi etc.Vipi nafasi ya kukua?
Ukimkuta mtu anaingiza million leo, biashara isipokufa basi mwakani haiwezi kuwa million tena.
Itakuwa imeongezeka....
Mfano alieajiriwa serikalini na aliejiajiri wote wanaingiza milioni 1 kwa mwezi?
1. aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi hadi usiku, alieajiriwa serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni na bado huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.
2. aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa serikalini anapumzika jumamosi na jumapili.
3.aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali, alieajiriwa serikalini haendi kazini idi (hata kama ni mkristo), mwaka mpya, meimosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k
4.aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa serikalini akiumwa anatoa notisi.
5. aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka
6. aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika
7. Aliyeajiriwa serikalini mkopo anapata kwa masharti nafuu na KWA haraka aliyejiajiri hawezi pata mkopo kibwerere
8. alieajiajiriwa na serikali ana muda mwingi wa kuwa na familia yake kuzidi aliejiajiri. ikifika jioni, weekend, sikukuu za serikali, likizo, n.k. ana muda wa kutosha wa kuwa na familia yake
9. Alieajiriwa serikalini anaweza kuwa ma biashara zake za kumuongezea kipato, hizi biashara zinaweza kurithiwa na watoto wake.
Mwisho niseme Kujiajiri watu wanameki bingo lakini ni wale wenye roho ngumu sana, juhudi, kujibana na uvumilivu, kinyume na hapo kukua ni kazi sana, mara kumi heri mtu alie serikalini.
Somebody had to say this!! Mimi nimefanya sana biashara, nimetoka sana jasho la hustle za hapa na pale ila asikudanganye mtu serikalini ni serikalini tu!!!! Kipindi cha corona biashara ziliyumba, kwenye private sectors baadhi waliondolewa. Ila serikalini mserereko uliendelea.
Na nyie mnaosema kama watoto wao watarithi kazi, kwani ukizaa mtoto unauhakika gani atapenda kitu unachokifanya? Una uhakika gani atakuja kupenda hiyo biashara yako ya mahindi,
Rai, tafuta kazi serikalini, establish vitega uchumi au biashara ambazo sio lazima uwepo 24/7.. unazichanga unawanunulia ardhi wakija kukua hao wanao wana cha kurithi. Na wenyewe unawajengea misingi ya kujitegemea kimaisha hata kama umewaandalia chochote kitu incase ukidondoka. Full stop
Hii mada haihusu wale wanaume wenye watoto sita ndani ya ndoa wanne nje. Nyie mkifa familia zenu zinatamanigi ziwachape makofi ngedere
Probabilities zake zikoje? Given wote ni wachapakazi sawa......Hata aliyeajiriwa anakua pia. Kuna annual increment (japo ni ndogo), kuna kupanda cheo.. kuna kuhama taasisi kuhamia taasisi inayolipa zaidi etc.
Kwani probability ya kukua kwa aliyejiajiri ikoje? Ni rahisi rahisi tu? Kila kitu ni kigumu, you have to work hard to achieve.Probabilities zake zikoje? Given wote ni wachapakazi sawa......
Kingine ambacho sio cha kusahau au kujisahaulisha ni......
Anayeingiza 1M ni mtu aliyejiajiri wa level gani na anayechukua take home serikalini ni mtu wa level gani.
Kama biashara itakuwa na sustainability na succession plan.Ila in the long run,
Aliyejiajiri atakuwa na faida zaidi.
Hapa kwenye kujiajiri unazungumzia biashara Kama biashara au hustle yaani una duka au kibanda Cha pumba??Mfano alieajiriwa serikalini na aliejiajiri wote wanaingiza milioni 1 kwa mwezi?
1. aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi hadi usiku, alieajiriwa serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni na bado huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.
2. aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa serikalini anapumzika jumamosi na jumapili.
3.aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali, alieajiriwa serikalini haendi kazini idi (hata kama ni mkristo), mwaka mpya, meimosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k
4.aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa serikalini akiumwa anatoa notisi.
5. aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka
6. aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika
7. Aliyeajiriwa serikalini mkopo anapata kwa masharti nafuu na KWA haraka aliyejiajiri hawezi pata mkopo kibwerere
8. alieajiajiriwa na serikali ana muda mwingi wa kuwa na familia yake kuzidi aliejiajiri. ikifika jioni, weekend, sikukuu za serikali, likizo, n.k. ana muda wa kutosha wa kuwa na familia yake
9. Alieajiriwa serikalini anaweza kuwa ma biashara zake za kumuongezea kipato, hizi biashara zinaweza kurithiwa na watoto wake.
Mwisho niseme Kujiajiri watu wanameki bingo lakini ni wale wenye roho ngumu sana, juhudi, kujibana na uvumilivu, kinyume na hapo kukua ni kazi sana, mara kumi heri mtu alie serikalini.
Kukua serikalini ni kuwa mchapakazi mzuri?Kwani probability ya kukua kwa aliyejiajiri ikoje? Ni rahisi rahisi tu? Kila kitu ni kigumu, you have to work hard to achieve.
Aliyejiajiri na aliye ajiriwa wote wana nafasi za kukua...na kukua huko, you have to work your ass off ili ukue.
1M ya kuajiriwa serikalini na 1M ya kujiajiri, ya kuajiriwa serikalini ina maisha mazuri ya kurelax zaidi kwa point alizotoa mtoa mada.