Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Acha kujipa moyo aliejiajiri ana uhuru mkubwa kuliko kuajiriwa kuajiriwa utumwa jifunze kujituma, mtu adi uombe ruhusa kweli jiajiri tengeneza stream nyingi za income zikufanyie kazi hakika utafurahia maisha na uhuru wako
 
Naomba nisiwasemee Wajasiriamali wengine maana sijui context yao na nature ya kujiajiri kwao, kujiajiri kuna namna zaidi nyingi sana. nijisemee mimi binafsi. Naomba tuu nisitafsiriwe vibaya ila najibu hoja hii ni nzuri.

Nimejiajiri people and money works for me.
Sio lazima niamke asubuhi kuwahi kwenda kuweka vidole kwenye mashine ya scan to prove my attendance ofisini, am a boss doing the needful. huwa nafika muda wowote ofisini kulingana na kazi, majukumu na mood yangu ya siku husika.

Nina uhuru, sina shuruti "must do" na sipangiwi majukumu wala sipimwi kwa "performance indicators" kama mwajiriwa bali kwa ufanisi,uzalishaji na mwenendo wa biashara yangu"scaling".

Sina kipato "uniform" kwa mwezi kama mshahara. Mshahara ni "uniform" kama unapata 10 basi pato lako ni 10 kila mwezi, yaani hata mtoto wako wa darasa la pili anajua tarehe moja baba atakuwa na milioni. Huwa napata 10 mwezi huu mwezi ujao napata 100 na kuna kipindi nakosa kabisa and am happy.

Kuhusu kuumwa, kwa nature ya biashara yangu au nisipokuwepo biashara haifi maana kuna mifumo ipo na watu wapo. Biashara ni mfumo yaani People, Product and Process.

Kuhusu muda wa kuwa na familia umedanganya, employees trade time to money, Entrepreneurs trade products ndio maana kwenye Job description unaambiwa muda wa kufika kazini na kutoka. Hebu fikiria bankers wanapata wapi muda wa kuwa familia zao! Huwezi safiri na familia kwenda vacation au kusalimia nyumbani isipokuwa mpaka likizo ya siku 28 kwa mwaka. Hapa ni uongo Mjasiriamali ana muda mwingi kuliko mtumishi.

Kuhusu Mtumishi kuwa na biashara au "Side hustle" inategemea na mindset ya Mtumishi mwenyewe hilo sikupingi japo bado atakuwa anatumikia mabwana wawili, muda atumikie mwajiri muda asimamie biashara zake hii wengi wanaweza ila inawaletea changamoto kubwa na ndio maana biashara nyingi za watumishi zinakufa kwa kukosa proper management hasa muda wa kuwatumikia mabwana wawili.

Kuhusu kufilisika hilo sikupingi maana sisi kwa nature ni risk takers na kufilisika au zile nyakati za biashara kuboom, recession, slup and recovery ni vitu vya kawaida ndio maana hata nyie mnafukuzwa kazi. Ndio risk hizo.

Kuhusu mikopo au loan facilities ni kwamba Mjasiriamali yeye kinachokopa ni biashara yake na dhamana zake, Mfanyakazi yeye anakopa yeye sio biashara. Kinachokopeshwa ni biashara sio mtu. Hapa najua huwezi kuelewa😁.

Mwisho kabisa nakushauri hujachelewa anza kuwa na Entrepreneurship mindset hata kama upo kazini. Kazi ina mwisho sio upewe hela ya kiinua mgongo ndio uanze biashara na ujasiriamali. Unaweza kuwa Mjasiriamali hata kama ni mfanyakazi. Biashara ni tabia, tunazijenga zinatujenga.
 
Makonda alikuwa mwajiriwa wewe unamzidi utajiri?

Mimi nimekulia Kijijini Kule Watoto wa Mwl ndio walikuwa wanava viatu na kula nyama siku zisizo za sikukuu na vyakula vyao vinaungwa mafuta na kukaangwa.

Watoto wa Mwl ndio wanavaa nguo safi na shati zenye kung'aa

Yaani watoto wa Mwl na Mwl ndio familia kila mtu anakimbilia kukopa akipata shida.
Yaani unaopodharau mtu aliyeajiriwa ni sababu tu ya Ubinafsi kwa kuwa wewe unazo nyingi basi unataka kudharau wengine.
Mkuu Bush Dokta kwanza salamu
Pili nikukumbushe kuwa hapa tunaongelea waliojiajiri sasa usije ukambeba mkulima wa mahindi kwa misimi miwili tena kwa jembe la mkono umlete hapa kusema amejiajiri .

Huyo anatafuta surviving food tu .

Hapa leo nazungumzia mtu aliyeweka atleast laki nane mpaka milioni na kuendelea anayeizungusha .

Nb .Makonda akiwa kazini sikuwa namzidi hela kwa kipindi kile ila kwasasa mimi bado nimeajiriwa lakini nimeshinda kesi ya urithi wa mali za mshua master sioni tabu kukuambia makonda hanifikii hata robo kwasasa .

Nb.walimu usiwafanye wa mfano kwenye mambo ya uchumi kwa maisha ya sasa yamewapiga vibaya mno maana mshahara hauendani na hali ya uchumi.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Somebody had to say this!! Mimi nimefanya sana biashara, nimetoka sana jasho la hustle za hapa na pale ila asikudanganye mtu serikalini ni serikalini tu!!!! Kipindi cha corona biashara ziliyumba, kwenye private sectors baadhi waliondolewa. Ila serikalini mserereko uliendelea.

Na nyie mnaosema kama watoto wao watarithi kazi, kwani ukizaa mtoto unauhakika gani atapenda kitu unachokifanya? Una uhakika gani atakuja kupenda hiyo biashara yako ya mahindi,

Rai, tafuta kazi serikalini, establish vitega uchumi au biashara ambazo sio lazima uwepo 24/7.. unazichanga unawanunulia ardhi wakija kukua hao wanao wana cha kurithi. Na wenyewe unawajengea misingi ya kujitegemea kimaisha hata kama umewaandalia chochote kitu incase ukidondoka. Full stop

Hii mada haihusu wale wanaume wenye watoto sita ndani ya ndoa wanne nje. Nyie mkifa familia zenu zinatamanigi ziwachape makofi ngedere
Hii akili ni ya chuo kikuu, anayebisha aseme.Kuajiriwa ni utumwa.
 
Huu ni ukweli mchungu. Kujiajiri ni sawa na kuajiriwa tu sema faida yake ni haupo chini ya mtu ila kichapo kipo palepale. Yaani kama umejiajiri na usipokuwepo hupati hela basi jua bado safari yako ni ndefu na inabidi uombewe ili ukue na kuvuka hiyo stage. Mimi hua nashauri vijana wasifuate mkumbo. Waingie kwanza kuajiriwa.
 
Kwangu kujiajiri ndokuna faidaa asèe
Hayo yote uliuoyasema siyo mateso ni hali yakuishi mazingira uliyopo
Tukomae ata kama tuko kwenye ajira zawatu tufungue njia tutengeneze ajira zetu
 
Mkuu Bush Dokta kwanza salamu
Pili nikukumbushe kuwa hapa tunaongelea waliojiajiri sasa usije ukambeba mkulima wa mahindi kwa misimi miwili tena kwa jembe la mkono umlete hapa kusema amejiajiri .

Huyo anatafuta surviving food tu .

Hapa leo nazungumzia mtu aliyeweka atleast laki nane mpaka milioni na kuendelea anayeizungusha .

Nb .Makonda akiwa kazini sikuwa namzidi hela kwa kipindi kile ila kwasasa mimi bado nimeajiriwa lakini nimeshinda kesi ya urithi wa mali za mshua master sioni tabu kukuambia makonda hanifikii hata robo kwasasa .

Nb.walimu usiwafanye wa mfano kwenye mambo ya uchumi kwa maisha ya sasa yamewapiga vibaya mno maana mshahara hauendani na hali ya uchumi.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Sawa nimekuelewa. Huyu Mkulima wa jembe la mkono yeye hajajiajiri?😆😆
 
Back
Top Bottom