Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Faida za kuajiriwa Serikalini
1. Rahisi kupata visa ya nchi yeyeto wanaamini huwezi zamia
2. Kwa mangi unakopa bila shida
3. Unakopa bank
4. Ukiimwa mda mrefu unaendelea tu kula mshahara kitandani
5. Job security kufukuzwa ni process
6. Ruhusa ya kusoma ndani au nje
7. Ukisimamishwa kazi mshahara na maslai yako pale pale ,huku ukiwa na mda wa kutosha kufanya mishe zako mfano bize na shule, biashara au kuajiriwa private company
8. Likizo bila malipo
9. Hela ya pension uzeeni ukistaafu inaingia tu muhimu upambane uwe mkubwa piga tu shule pesheni yako ya mwezi unamzidi graduate.
Mawazo ya kimasikini
 
Nimejiajiri mwaka wa tano huu,sikumbuki lini nilisema nimepumzika Yani nimetulia tu,sikumbuki lini niliamua kusafiri tu bila kutokea matatizo,kwakweli kujiajiri na mtaji wa million ni mateso Sana Bora kuzama serikalini tu
Wewe ni masikini
 
Wanaojiajiri ni wale waliokubali kuzifuata ndoto zao na kizitimiza..

Na nyie wakuajiriwai ndio wale mliokubali kuziacha/kuzikana ndoto zenu na kuzijenga ndoto za wengine

Mnajisifu kwa mishahara mikubwa wakati maendeleo yenu binafsi hayaonekani.....mwishoe mnakaa mnastaafu mkipata izo pensheni ndio mnaanzaga et kujenga tena nyumba za kawaida tu, Wakati huo ujana wako ndio ulikua unatamba kitaa kua mimi mwajiriwa bwana... na kuendekeza starehe

Your salary is the bribe they give you to forget your dream
 
Finally mtu kaeleza ukweli mchungu.
Mh, hivi nyie mnajua mnachoongea kweli au mnaongea kiujumla jumla tu?

Nani kasema ukijiajiri ni lazima utoke nyumbani asubuhi na urudi jioni? Na ni wapi ambako ukijiajiri hupati mkopo kirahisi?

Mi nadhani nyie ni watoto wadogo mlioko shule mkiwa na hamu kubwa ya kuajiriwa.

Mwisho wa siku, ukijiajiri au ukiajiriwa ni sawa tu kulingana na wewe unataka maisha ya aina gani.
 
Mimi nawaheshimu sana waliojiajiri..ndio wananiweka mjini...hivi maduka ya mangi yaanze kupokea cash tu...tutatoboa kweli kuanzia tarehe 10-20 pale.
 
Back
Top Bottom