Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Mada sio kuajiriwa tu mada ni kuajiriwa serikalini au kujiajiri, kupi kuna nafuu ya maisha? Wewe unaleta stori za jamaa njaa mwenzako sijui alitaka kukuajiri na blah blah kibao, serikalini hakuna mbambamba na watu wanaishi kwa marupurupu hawategemei mishahara, kila siku ana uhakika wa kula na akistaafu kuna kiinua mgongo na bado ataendelea kupokea mshahara mpka kufa kwake, japo ni nusu mshahara.
Anyway, mimi nimejiajiri mkuu, leo nimeingia kazini kwangu saa saba mchana na nimeingiza pesa kama kawaida

Wewe endelea kuajiriwa serikalini ila sisi tuliojiajiri na tunaoajiri tuache kama tulivyo

Aliyetaka kuniajiri alivutiwa na mimi baada ya kuona nasimamia vizuri kazi yangu hivyo akataka nitafute kijana nimuajiri kisha nikaungane na yeye kwenye ofisi yake
 
Aliyeajiriwa ni katika sekta gani na aliyejiajiri ni katika sekta gani, tuanzie hapo
Alieajiriwa kama anapata mshahara mkubwa na madili ya hela ndefu mtu aliojiajiri sio rahisi kumkuta. We imagine mtu kama Makamba kalamba uwaziri wa Nishati, Salary tu ni zaidi ya 200M kwa mwaka. Bado ajagusa deals za Billions za kutosha.
 
Aliyeajiriwa ni katika sekta gani na aliyejiajiri ni katika sekta gani, tuanzie hapo
Alieajiriwa kama anapata mshahara mkubwa na madili ya hela ndefu mtu aliojiajiri sio rahisi kumkuta. We imagine mtu kama Makamba kalamba uwaziri wa Nishati, Salary tu ni zaidi ya 200M kwa mwaka. Bado ajagusa deals za Billions
Ukiajiriwa moyo hauendi mbiyo sana kama kujiajiri😆😆😆
TRA, TBS, FIRE, OSHA na wengineo. Hapo ni mwendo wa kuteseka tu kujiajiri
 
Yani mtu unafanya kazi halmashauri huko Namtumbo unataka kujilinganisha na mtu ana biashara zake kariakoo au mabasi, daladala?



Kuweni na heshima!


Unalipwa mshahara milion 2 Kwa mwaka 24. Hiyo Hela haiwezi kuclear hata contena moja la vipodozi au vitenge.

Hapo ninezungumzia salary ya 2,000,000 ambae sio wengi wanalipwa hivyo.


Sasa wewe mwenyewe jitathimini

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Somebody had to say this!! Mimi nimefanya sana biashara, nimetoka sana jasho la hustle za hapa na pale ila asikudanganye mtu Serikalini ni Serikalini tu!!!! Kipindi cha corona biashara ziliyumba, kwenye private sectors baadhi waliondolewa. Ila Serikalini mserereko uliendelea.

Na nyie mnaosema kama watoto wao watarithi kazi, kwani ukizaa mtoto una uhakika gani atapenda kitu unachokifanya? Una uhakika gani atakuja kupenda hiyo biashara yako ya mahindi.

Rai, tafuta kazi Serikalini, establish vitega uchumi au biashara ambazo sio lazima uwepo 24/7.. unazichanga unawanunulia ardhi wakija kukua hao wanao wana cha kurithi. Na wenyewe unawajengea misingi ya kujitegemea kimaisha hata kama umewaandalia chochote kitu incase ukidondoka. Full stop.

Hii mada haihusu wale wanaume wenye watoto sita ndani ya ndoa wanne nje. Nyie mkifa familia zenu zinatamanigi ziwachape makofi ngedere
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23] Mkuu umenichekesha sana hiyo para ya mwisho. Eti watoto sita wa ndani na wanne wa nje
 
Cha ajabu sana ni kwamba matajiri wote duniani wamejiajiri, sijawahi kusikia tajiri aliyeajiriwa serikalini... [emoji23] [emoji23]
Kwa bongo ni kinyume, mwajiriwa wa serikalini anaweza kukwapua 100 billion in a short while. Wewe ukapewa million 50 kwenye kujiajiri it will take you a lifetime kugenerate hio pesa ambayo mwenzio kaikwapua kwa muda mfupi tu.
 
Matajiri wa duniani Hawajajiajiri... Wameajiri watu. Know the difference.

Kuna tofauti kati ya Kujiajiri na Kuajiri wengine wakufanyie kazi. Mada inazungumzia Waliojiajiri vs Waajiriwa, haizungumzii walioajiri watu.
Matajiri walioajiri watu hao ndio Real Entrepreneurs! Mfano ni kina Elon Musk, Mark Zuckeberg. Hao wote wana team za watu zinawafanyia kazi tu wao ni CEOs.

Bongo mtu ananunua nguo Kariakoo na Karume anaenda kuuza pembezon mwa mji anajiita mjasiriamali

Mtu anachoma mishkaki na chips anajiita mjasiriamali 🤣
 
Ni kwel kujiajiri sio kitoto.Hii ni dedication ya watu wazima haswaaa. Ni kazi nzito mnoo ila kwa ajili ya ku guarantee future sio yako tu bali na ya kizaz chako, ni afadhal kujitoa muhanga ujiajiri.
NB
Ajira sio kitu kibaya maana hata sisi tuliojiajiri , tuna waajir pia wengine ili ku leverage mission zetu.
Kujiajiri inategemea na sector gani upo, kuna mtu ni mhandisi kajiajiri anafukuzia tender tu. Akiotea kazi 3 tu kwa mwaka hela anayomeki ni zaidi ya kiinua mgongo cha mwalimu kwa miaka 60 ya kuajiriwa. Ila kuna mtu kajiajiri anachoma mahindi barabarani huyo hawezi kupambana na kipato cha waajiriwa wengi tu wanaolipwa million 3 au zaidi kwa mwezi waliopo kwenye chain ya kupiga dili na kula rushwa.
 
Back
Top Bottom