Tanzania ukisoma hadi chuo ni kama laana mtaani

Tatizo wengi tumekaza kwa sababu tumetoka familia duni maana tulijua sisi ndio njia ya kuuaga umaskini wazazi wamekopa sana, wamepiga sana vibarua sa hivi ata nguvu hawana tena ni basi tu tunakaza ila maisha yamekuwa mateso bila chuki
 
Oyaaa acha na wanatunyanyasa maana ndio wana vi IST na viduka vya nguo midizini na karume oya wanatunanga had basi kibaya zaidi hawatupi michongo zaidi kutununulia konyagi tena chupa kubwa watuue mapema 😞😞
Wanaamini tukianza kufanikiwa tutawaacha kwa kasi ya 5G ndio maana hawatupi michongo.
 
Wasomi wa sasa kila mtu anatuita wavivu mara wapumbavu hatuwezi kujiajiri ila hawajui uhalisia maana waTZ tunaongoza kwa maneno bila research
Kwa uvivu nakubali, wengi ni wavivu sana ndio maana hata kujitafuta kujiajiri ni ngumu. Kwa ufupi wasomi tunajionaga ni special sana lakini kama usomi wako hauleti chakula mezani, haulipi bills sio kitu. Life is all about love&money.

Tukija kwenye competition ndio hoi kabisa. Mfumo wetu wa elimu unakazana kuzalisha quantity na sio quality na hii ni shida kubwa sana.

Mtu ana degree ya field fulani lakini hana uwezo wa kujidefend kama msomi wa degree inabaki kuwa ni degree kwa jina na cheti. Tunakoelekea hali ndio itazidi kuwa mbaya zaidi. Acha nilime sasa.
 
Dash kuna uncle wangu ni msomi safi very bright kichwani lakini mwaka wa 6 huu sometimes namuona ni kama anaanza kuloose mind
Oya mi wa 8 huu ni mikazo tu usmart unapotea tushajitolea sana ofisi za watu tushafuga sana kuku lakini hola inatia uchizi sometimes tunamaliza kunywa chai ndio tunapiga maswali au unalala ndio unakumbuka hujaoga siku ya pili
 
Wengi wanasoma, ila wanao elimika ni wachache.
 
Masomo yenyewe ni mwendo wa ku crame ujibu mtihani unategemea bila kukaa kwenye field yako baada ya miaka 7 utakumbuka kitu.. hata kama ni mwalimu miaka 7 bila kufundisha utaweza kweli... Si inakupotezea hata confidence ya kucompete na fresh from school
 
Hivi kuanzisha chekechea unahitaji mtaji ? Hapo ndipo mnapofeli, hivi kuwa fundi unahitaji mtaji? Na vipo vyanzo vingi vya kazi sema tu hamjui namna ya kutumia mazingira uliopo.

Lugha tu inatosha, na hapo ndio elimu ufanya kazi.
 
hao wanafunzi wa chekechea utawafundishia chini ya mti?
Watu wanaongeaga tu Yani,hao chekechea wanahitaji jengo,viti vyakukalia, material za kufundishia, location Kwa maana huwezi fungua darasa la tuition kijijini maana hauta PATA wateja lazima iwe town sasa, gharama yakupata jengo town ni kubwa kupita maelezo. Halafu mtu anaropoka et auhitaji mtaji au fedha none sense 😏😏😏😏
 
Ila elimu nzuri ni mtaji, na, siraha kibindoni, niliona pale UN, ilitangazwa kazi, wote tukagaragazwa na Dada mmoja mwenye degree yake kutoka Udom,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…