Tanzania ukisoma hadi chuo ni kama laana mtaani

Maliza chuo mdogo wangu maneno yako yana ushawishi ila yamekaa kinadharia njoo mtaani ufanye practical kaa miaka mitano afu rudi kutupa mrejesho kwenye huu uzi.. kwamba video za youtube quality aisee kaz kweli kweli 🙌😂😂
 
Tatizo una degree ya uchumi halafu huna lolote zaidi ya uchawa na kusifu serikali.
Watu walivyo na maisha magumu walitarajia watu kama nyie muisaidie serikali kuonesha njia lakini hamfanyi hivyo,unadhani nani atakuelewa?
Hahaha apo kwanza nicheke kwamba mimi ni chawa, Kwamba unaamka unapiga mswaki unakoga unakwenda kuisaidia serikali kuionyesha njia, Baridi mwanangu freshii 🤜
 
Pole sana inaonekana unapitia mazito, Elimu yako weka pembeni jikite katika kutatua changamoto za Jamii inayokuzunguke kama ;

Chakula. Kipindi hiki ni cha mavuno nafaka bei cheee huku mjini bado ghali ingia humu kwa mtaji wowote utauona mwanga.
Biashara ya nafaka usiichukulie poa ina umafia mwingi kupigwa au kuuziwa mchele wenye mawe ni 100%
 
Thread ya kipumbavu kabisa kuwaona hapa JF.
 
Pole sana inaonekana unapitia mazito, Elimu yako weka pembeni jikite katika kutatua changamoto za Jamii inayokuzunguke kama:

Chakula. Kipindi hiki ni cha mavuno nafaka bei cheee huku mjini bado ghali ingia humu kwa mtaji wowote utauona mwanga.
Mtaji ni hela
 
Kaa karibu na madon kijana utapewa connection kama mnavyosema.

Pesa na mafanikio yote unayoyataka yapo upande wa pili.

Wewe mwenyewe huwezi lazima ushikwe mkono.

Fungua macho utaona.
 
Shauri watu,, wasisome kupata kazi.. wa some kupata fani
(Ujuzi), duniani kote shule inakuba basics za jinsi ya kutengeneza motor na sio ujuzi wa jinsi ya kutengeneza motor,, Ukishajua basics kazi ni kwako unaenda kutumia vip huo ujuzi..
Usidanganyike na oh mimi nna passion ya philosophy afu mzima mzima unaenda kusoma degree ya philosophy.. utalaumu watu …

Last but not least, lazima wengine wawe chambo ili kutufikisha nchi ya ahadi…

Usitafute maisha kwa mindset ya kutaka fairness hapa duniani…. Utalaumu watu hadi kufa kwako..

Ukipata aliyekaa kizembe wew mfanye daraja vuka mbele…
Ni hayo tu…
 
The bottom. Line is ,kuzaliwa nchi za makalioni mwa dunia kama Tanzania ni laana tosha .
Raia wake na viongozi wamechoka kiakili , mtu na tumbo lake kubwa kama pipa la ulanzi , anaongea kujiajiri , as if kujiajiri ni kitu easy sana ,wakati ni kitu kinachohitaji resources za kutosha , muda na experience / guidance .
Vitu ambavyo kwa ordinary graduates ni hamna.
 
Jikusanye kuza mtaji hata kwa kuomba mbona shule umesomeshwa tafuta hata 500k tuu ingia Dodoma huku ni njaa njoo uza nafaka utapiga hela mpaka uikimbie..
Sasa mkuu, Inawezekana kweli mtu yupo dar ana laki tano achukue nafaka alete dodoma?
 
Wengi wanasoma, ila wanao elimika ni wachache.
Unaweza kuelimika na usiwe na kipato. Tujaribu kuelewa na kuacha kufikiri kuwa kila anayekosa tatizo ni yeye.
 
Kweli hali ni ngumu mtaani kazi hakuna na tumefikishwa hapa na mfumo wa elimu, mtu anamaliza chuo hata kulima bustani tu hajui ni muda sasa wa gvt kurekebisha mtaala wa elimu wanafunzi wafundishwe skills za mikono kila mtoto akimaliza elimu ya msingi (kidato cha nne) aondoke na ujuzi wakumsaidia huko mbele skills za kujiajiri kama kilimo,ushonaji,mapambo,upishi, ufundi magari au umeme inaweza isimalize tatizo la ajira lakini itapunguza japo kidogo.
Pili vijana wawezeshwe kwa mikopo wapo wanaomaliza chuo wanaweza kuingia kwenye kilimo, ufugaji lakini changamoto ni mitaji , vijana wahamasishwe kujijnga kwenye vikundi wapewe mikopo ile ya asilimia 10 shida vijana wa watz hawapendani ni ngumu kushirikiana kufikia malengo lakini ingewezekana kuungana na ile mikopo ingeaafikia walengo ingesaidia sana kupunguza shida ya ajira.
 
Maisha ni magumu sana sio kwamba kila graduate alieshindwa kujiajiri au jobless ni mpumbavu. Wajinga tu wasiona na uelewa ndio wanaweza kufikiria hivyo
 
Ndio maana watu wameamua kuwa machawa. Hadi waziri anakua chawa anadiriki kisema kuna mtu amepunguza vifo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…