Tanzania unaweza kusema uongo hadharani na usiwajibike popote. Sheria ya kulinda maadili itungwe

Umeandika vizuri na kwa lugha nyepesi.

Naongeza nyama tu.

Watu wadai elimu, watake kuwa na elimu. Biashara ya watu wapewe elimu imeisha muda wake.

Kwa nini? Tofauti ya watu kutaka na kudai elimu na watu kupewa elimu ni nini?

Watu wanaopewa elimu, wanakuwa wapokeaji, wanachukua kitu ambacho kimeshaandaliwa kutoka juu, wao wanapokea tu. Watu wanaotaka elimu, wanaodai elimu, wana ownership, wana umiliki wa hiyo elimu.

Watauliza, sisi tuna njaa, tunataka elimu ya kulima mazao yetu tuweze kuvuna vizuri zaidi, kwa nini mnatupa elimu ya kudarizi suti za Kifaransa? Kwa nini mnatupa elimu ya ushairi wa zama za Pontius Pilato? Yumkini elimu ni elimu, na udarizi wa suti za Kifaransa unaweza kutusaidia kwenye biashara, na ushairi wa zama za Pontius Pilato unaweza kutusaidia kujua historia na mambo ya kifalsafa, lakini, kama hatujaweza kula leo na kesho, hata hayo masomo tutashindwa kuyafuatilia.

Kwa hivyo ni lazima watu wachukue ownership.

Na hili ni jambo la msingi sana. Ndiyo jambo nimekuwa nikilisisitiza mara kwa mara. Ownership.

Hwezi kuwa na sheria inayofanya kazi vizuri kama watu hawajachukua ownership na kuifanya ile sheria kuwa yao. Bila hili, hiyo sheria itaonekana ni mbwembwe za kibwanyenye tu ambazo hazihusiani na maisha ya wananchi.

Kuhusu upotoshaji, kinachoendelea ni aibu. Kuna siku wiki chache zilizopita, Dr. Slaa alifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkataba wa Bandari na DPW (I am not a Slaa fanboy, nimepishana naye kwenye mambo fulani, kwa hiyo huu ni mfano tu, not hagiography).

Katika mkutano ule, katika kujaribu kuwa mzamivu, Dr. Slaa alisema kwamba kimsingi hana tatizo na dhana ya uwekezaji, akaenda kuelezea matatizo anayoyaona kwenye mkataba na DPW.

Kuna baadhi ya magazeti, bila aibu, yakaandika habari ile kama vile Dr. Slaa kasema hana tatizo na mkataba wa DPW. Nilisikitika sana, kwa sababu Dr. Slaa anaeleweka kabisa msimamo wake ukoje. Haya magazeti yaliamua kupindisha ukweli kwa makusudi kabisa.

Mimi nafikiri tunaweza kutunga sheria zilizojikita zaidi kuliko kitu chenye utata kama "kusema uongo".

Wananchi wachukue ownership ya nchi yao na sheria zao.

Tualike wataalamu wa uchumi watushauri kuhusu sheria za uhujumu uchumi.

Tualike wataalamu wa falsafa na siasa tutunge sheria za political speech.

Tualike wataalamu wa saikolojia watusaidie kuelewa saikolojia ya nchi yetu, tusitunge misheria mikali tu bila kujua saikolojia yetu ikoje.

Zaidi ya yote, sote tujielimishe tusiweze kudanganywa kirahisi, tujue maisha ni mapambano, tusitake majibu rahisi kwa maswali magumu, kama kumaliza tatizo la uongo kwa sheria.

Tujue kwamba, kifalsafa, hata swali la uongo ni nini na ukweli ni nini bado lina matatizo mengi sana
 
Naomba nisaidie kuelewesha mkuu.

Maana naweza kufikia sehemu nikachoka.
 
Mleta hoja hata kwa shetani ukisema ukweli wewe ndie ADUI ila ukisema uongo wewe ndie RAFIKI wa shetani!
 
Mkuu Tz tuna makanjanja hatuna waandishi wa habari katu!
 
Ndugu,, vyombo vya habali mm naona vipo Kwa Kasi sana ila ndo chanzo kikubwa ninachokitazam ambacho kinakuja kupotosha jamii kama selikali yetu isipochukua hatua Kwa halaka kupata waandish WA habali WA ukweli na wenye kuelimisha jamii
 
Kati ya vitu umeandika mwaka huu vyenye mashiko hiki ni Cha kwanza!
Nadhani ili tufike huko bunge nalo libinafsishwe kwa mojawapo ya nchi za Ulaya!
Lakini kundelea kuwategemea hawa wanaotumia uongo na ulaghai kushinda chaguzi tutachelewa sana.
 
Hajaandika uongo..
1. Waziri mkuu alidanganya kuwa JPM alikuwa mzima, na mpaka leo hajaomba radhi hadhara aliyoidanganya
2. Waziri mkuu alisema ripoti ya kuungua kwa soko la Kariakoo ingetoka baada ya wiki, lakini kimyaa..!!
3. Kuhusu DPW ndo hatari, kila mtoa ufafanuzi keshadanganya, kuanzi Greyson Msigwa hadi wengine wote waliojifanya kutoa ufafanuzi
 
Ndugu Kiranga, akhsante sana kwa hii kitu, "Wananchi wachukue ownership ya nchi yao na sheria zao."

Kongole sana.
Ningependa siku tuwe na mjadala kuhusu "ownership" na jinsi inavyoleta maendeleo makubwa sana kwa binadamu.

Kiufupi, miaka ya 1990, mzee wangu alikuwa na biashara zake,mimi na ndugu zangu hatukuwa tunajisikia kuwa wafanyabiashara,lakini mzee alichofanya ni kututengeneza kwa kutufanya tufeel "ownership" ya zile biashara japo hatutaki.

Matokeo yake,sote hakuna kingine tunataka kufanya zaidi ya kuendeleza hizo biashara.
 
Ni Sawa. Tutatunga SHERIA nyingi kwa viingereza vingi. Lakini Rostam kamaliza. Sheria zetu ni za watu masikini na wasio na mamlaka
 
I second you, mkuu.

Kutunga Sheria ni jambo moja, kuitekeleza ni jambo lingine.

Kipindi cha Hitler kule Ujerumani, inasemekana Ujerumani ilikuwa miongoni mwa nchi zenye Katiba bora kabisa. Ila Adolf Hitler akaipuuza na kuwa dikteta.

Nchi iwayo yoyote ile, isipokuwa na utamaduni wa kuheshimu Sheriza zake ilizozitunga yenyewe, ipo hatari kwa nchi hiyo kuwa na Sheria nzuri lakini ambazo hazitekelezeki.

Watazame wenzetu Uchina, wakitunga Sheria, kama adhabu ya kosa flani kwenye Sheria hiyo ni kunyongwa; unanyongwa kweli hata uwe nani.

Lakini sisi Waafrika tena hasa Wabongo tumezoea sana kuishi kwa mazoea.
 
Hilo jambo la ownership ni muhimu sana.

Kwa sasa, tatizo si kwamba wananchi tu hawajisikii kuwa na ownership, bali hata hao viongozi wanajiona kama nchi si yao, ndiyo maana wanaiuza kwa vipande arobaini vya fedha.

Mimi najiuliza, ile bandari ingekuwa ya baba yake rais, ni family business yao, angeingia mkataba mbovu kama huu?

Hata viongozi hawajali.
 
Kwani majaliwa
Leo hii Waziri Mkuu aliye madarakani anaendelea baada ya kudanganya taifa kwamba rais alikuwa mzima anachapa kazi, wakati rais alikuwa anajifia zake.
Kwani Majaliwa Majaliwa Bado ni pm?
 
kama kutatungwa sheria ya kuthibiti uropokaji kama wa Nape Nnauye, itapendeza sana.
 
Naunga mkono hoja na iletwe haraka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…