Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Umeandika vizuri na kwa lugha nyepesi.nikweli Kikubwa watu wapewe elimu ya kujua kuchambua ukweli na uongo maana asilimia kubwa ya watu tuna utamaduni WA kuwa sisi hatufatilii mambo, alichokisema kiongozi pengne kuhusu jambo flan katika serikali yetu mtu hawezi kufatilia je ni kweli alichokisema kiongozi ni Cha kweli ama uongo
Kingne upotoshaji Kwa njia ya media baadhi ya waandish WA habali pia wamekuwa ni chanzo cha habali za uongo, unakuta kiongozi ameongea kitu Cha ukwel lakin baadhi ya waandish wanaongea kinyume kabisa na ambavyo ilivyo,,
Mm naona Sheria kama hazipo zitungwe za kusema uongo, na kama zipo basi tupew elimu namna ya kuzifahamu na namna ya kuelimisha vizazi vijavyo
Naongeza nyama tu.
Watu wadai elimu, watake kuwa na elimu. Biashara ya watu wapewe elimu imeisha muda wake.
Kwa nini? Tofauti ya watu kutaka na kudai elimu na watu kupewa elimu ni nini?
Watu wanaopewa elimu, wanakuwa wapokeaji, wanachukua kitu ambacho kimeshaandaliwa kutoka juu, wao wanapokea tu. Watu wanaotaka elimu, wanaodai elimu, wana ownership, wana umiliki wa hiyo elimu.
Watauliza, sisi tuna njaa, tunataka elimu ya kulima mazao yetu tuweze kuvuna vizuri zaidi, kwa nini mnatupa elimu ya kudarizi suti za Kifaransa? Kwa nini mnatupa elimu ya ushairi wa zama za Pontius Pilato? Yumkini elimu ni elimu, na udarizi wa suti za Kifaransa unaweza kutusaidia kwenye biashara, na ushairi wa zama za Pontius Pilato unaweza kutusaidia kujua historia na mambo ya kifalsafa, lakini, kama hatujaweza kula leo na kesho, hata hayo masomo tutashindwa kuyafuatilia.
Kwa hivyo ni lazima watu wachukue ownership.
Na hili ni jambo la msingi sana. Ndiyo jambo nimekuwa nikilisisitiza mara kwa mara. Ownership.
Hwezi kuwa na sheria inayofanya kazi vizuri kama watu hawajachukua ownership na kuifanya ile sheria kuwa yao. Bila hili, hiyo sheria itaonekana ni mbwembwe za kibwanyenye tu ambazo hazihusiani na maisha ya wananchi.
Kuhusu upotoshaji, kinachoendelea ni aibu. Kuna siku wiki chache zilizopita, Dr. Slaa alifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkataba wa Bandari na DPW (I am not a Slaa fanboy, nimepishana naye kwenye mambo fulani, kwa hiyo huu ni mfano tu, not hagiography).
Katika mkutano ule, katika kujaribu kuwa mzamivu, Dr. Slaa alisema kwamba kimsingi hana tatizo na dhana ya uwekezaji, akaenda kuelezea matatizo anayoyaona kwenye mkataba na DPW.
Kuna baadhi ya magazeti, bila aibu, yakaandika habari ile kama vile Dr. Slaa kasema hana tatizo na mkataba wa DPW. Nilisikitika sana, kwa sababu Dr. Slaa anaeleweka kabisa msimamo wake ukoje. Haya magazeti yaliamua kupindisha ukweli kwa makusudi kabisa.
Mimi nafikiri tunaweza kutunga sheria zilizojikita zaidi kuliko kitu chenye utata kama "kusema uongo".
Wananchi wachukue ownership ya nchi yao na sheria zao.
Tualike wataalamu wa uchumi watushauri kuhusu sheria za uhujumu uchumi.
Tualike wataalamu wa falsafa na siasa tutunge sheria za political speech.
Tualike wataalamu wa saikolojia watusaidie kuelewa saikolojia ya nchi yetu, tusitunge misheria mikali tu bila kujua saikolojia yetu ikoje.
Zaidi ya yote, sote tujielimishe tusiweze kudanganywa kirahisi, tujue maisha ni mapambano, tusitake majibu rahisi kwa maswali magumu, kama kumaliza tatizo la uongo kwa sheria.
Tujue kwamba, kifalsafa, hata swali la uongo ni nini na ukweli ni nini bado lina matatizo mengi sana