Ukijiondoa ushabiki wa Yanga na kunisikia kidogo, pengine unaweza kuondoka hata na kitu walau kidogo.
Madagascar, Guinea ya Ikweta na Cape Verde ni mifano michache ya nchi zilizokuwa chini sana kisoka barani Africa, lakini ziliamua kutafuta wachezaji popote pale duniani wenye chembechembe ya nchi zao na kuwashawishi wachukue uraia ili wazichezee nchi zao, na jambo hili limewasaidia sana hadi Madagascar na Cape Verde zimekuwa zikikata tiketi ya AFCON na hata Guinea ya Ikweta ilikuwa mwenyeji wa AFCON 2015 na kufika nusu fainali, hatua ambayo ni kubwa sana
Sasa sisi badala ya kuwashawishi wanaoweza kutusaidia eti tunashika bango tena kwa uchungu sana. Kisiasa ni jambo la kawaida sana kwa Waziri kutoa uraia kwa mkimbizi au mgeni mwingine, tena hata kama hasaidii lolote nchini. Tuache povu, waziri ametoa uraia kwa Kibu, na yeye aliyepewa ameukubali
View attachment 1967069
Gwiji la Habari Tanzania
www.habarileo.co.tz