Tanzania: Wakimbizi kutoka Msumbiji warudishwa kwa nguvu walikotoka

Tanzania: Wakimbizi kutoka Msumbiji warudishwa kwa nguvu walikotoka

Sheria za kimataifa zinakataza kuwatenda hivyo wakimbizi. Siyo poa
 
Hapo ni mpaka serikali ya Msumbiji iridhie.
Nimeona wanahangaika muda mrefu kuomba msaada Nchi jirani mpaka Zimbabwe alimtosa baadhi ya jirani zake wamekubali na nchi za jumuiya ya ulaya huko watashusha vikosi ufaransa na ureno mmarekani katuma kikosi cha mafunzo jinsi ya kukabiliana na wanamgambo...
 
Hawa alshabab wakizidi kuchekewa watasumbua sana

Ova
 
Hapa ni wananchi wanapigania haki ya mgao wa rasilimali za nchi.

Basi ni ajabu kwamba wanaochinjwa na hawa al-shabab ni wanyonge wasio na chochote. Na sasa wameanza kuchinja hata watoto wadogo wa hao wanyonge!

Huko Nigeria nako Boko Haram wanaangamiza wanyonge vijijini tena Waislamu “wenzao”. Hapo kweli kuna kupigania mgao wa rasilimali?

Kinachoshawishi zaidi ni ile hoja kwamba baadhi ya “mabepari” wanatumia hivyo vikundi kwa malengo ya kimafia wakati mwingine wakishirikiana na serikali za hizo nchi za Afrika ili kuchota rasilimali za asili bila kunufaisha jamii husika na kufisidi hazina za taifa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi! Kuna viongozi wa serikali wanatajirika kishenzi kupitia makundi hayo.
 
Nimeona wanahangaika muda mrefu kuomba msaada Nchi jirani mpaka Zimbabwe alimtosa baadhi ya jirani zake wamekubali na nchi za jumuiya ya ulaya huko watashusha vikosi ufaransa na ureno mmarekani katuma kikosi cha mafunzo jinsi ya kukabiliana na wanamgambo...
Lakini hilo halijustfy kuwarudisha watu waliokimbia kuchinjwa.
 
... mnakumbuka miaka ya nyuma watanzania walivyouliwa Msumbiji? Nina jaama yangu mmoja naye alikumbwa na kadhia hiyo; alifia huko. Ifike mahali ile huruma ya kuwapokea wageni tuseme basi; toka enzi za ukombozi wakivurugana wanakimbilia Tanzania; tuseme basi. Ya kwetu wenyewe yanatushinda, kila mtu abaki kwao kama ni exchange ziwe biashara sio watu.
Tujaribu kuvaa viatu vyao.
 
Ilitakiwa iwe hivi:
1. Mauonevu na manyanyasano ndani ya nchi yasiwepo. Unaweza kukuta watu wa kaskazini ya msumbiji wananyanyaswa na wenzao wa sehemu ingine na kubaguliwa (a.k.a ukanda, udini, ukabila). Sasa vikundi vya kihuni mabeberu wanatumia udhaifu huo kuleta vurugu

2. Kukiwa na haki ndani ya nchi za Afrika na nchi moja ikivamiwa na wahuni majeshi ya nchi zingine za Afrika ziombwe kuingilia kuondoa hao wahuni
Ni kweli kabisa.mabeberu hawampendi mtu.Angalia yaliyomkuta Gadafi mpaka mwenyewe hakuamini akawa analalama kabla ya kifo.Yule Sarkozy aliyemsaidia mapesa mengi ashinde uchaguzi ndiye aliyekuwa wa mwanzo kuishambulia Libya siku ilipofika.Alisahau wema wa Ghadafi akaangalia maslahi ya kiuchumi.Pamoja na kwamba lengo halikufikiwa kwani hatimae Libya ilivamiwa na mafisi mpaka mzoga ikashindikana kuula.
Vijana wa kihuni walidangwanywa sana mpaka wakashikishwa bunduki kumsaka Ghadafi.Muda mfupi baada ya kuondoka wakajua kuwa wamedanganywa lakini walichelewa sana kujua.
 
Hawa UN bhana hao magaidi Mara nyingi utawakuta na ndala tuu kama watia huruma fulani wakishindwa Vita wanavua magwanda wanajifanya wakimbizi kuwapokea hao inatakiwa uchunguzi wa kina kidogo sio kizembe zembe tuu kumbe ndio wanakuja kujikusanya huku tena baada ya kutimuliwa huko msumbiji...
Kwanini Ureno na Ufaransa wasiwachukue has wakimbizi laki saba. Sababu wanawekeza pesa nyingi karibu na 60bn dollars. 140 trillioni tshs.

Kwanini wasifungue kambi ndani ya Msumbiji? Wanajeshi wetu wanaweza kuwalinda ndani ya mipaka yao UN wakiwalipa wanajeshi wetu kama tunavyofanya DRC.
 
Back
Top Bottom