Tanzania ya Rais Samia ndiyo tunaitaka kwani ni ya amani, utu na upendo na wala hakuna mauwaji na mabaya kama ya kwingineko duniani

Tanzania ya Rais Samia ndiyo tunaitaka kwani ni ya amani, utu na upendo na wala hakuna mauwaji na mabaya kama ya kwingineko duniani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mwili wa mfanyabiashara wa madini ya ujenzi, David Mollel mkazi wa Kata ya Moivaro, umekutwa ukining’inia kwenye mti juu ya Mlima Oldonyowas, jirani na eneo linalotumika kwa maombi.

Inadaiwa Mollel mwenye umri wa kati ya miaka 50 na 55, aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumanne, Oktoba Mosi, 2024 kwa kunyongwa na mkanda wa suruali. Mwili wake ulifunikwa kitambaa chekundu usoni.

Taarifa za awali zinaashiria mgogoro wa kugombea eneo la uchimbaji madini ya ujenzi aina ya moramu ni chanzo cha mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha tukio hilo akisema uchunguzi umeanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Chanzo Taarifa: mwananchi_official

Kwakuwa mnataka sana Kusifiwa na Mkisemwa ili mbadilike mnachukia sasa ni mwendo wa kuwasafuni tu sawa?
 
Tafsida yako kama nimeielewa vyema kama ninavyoamini naweza kuelewa vizuri,
inakinzana na maudhui uliyoyakusudia.

Sina lengo, muda wala Nia ya kumpigia chapuo mtu hapa jukwaani wala nje yake ya na si mfuasi mzuri wa kuvutana hasa juu ya mabo ya kisiasa lakini; Tuulizane kidogo,
Mauaji ( ama yanayodhaniwa kuwa ni mauaji maana haijathibitishwa rasmi na vyombo husika)
yanahusishwa mojakwamoja na mgogoro ambao bila shaka kwa nukuu ya mleta Uzi una chanzo chake kabisa, Sasa ni kwanini kichwa kiwe namna kilivyo?
 
Muhimu ni Ile kauli ya "mitano tena" kule Mbeya, imepogwa marufuku Rasmi.
 
Tafsida yako kama nimeielewa vyema kama ninavyoamini naweza kuelewa vizuri,
inakinzana na maudhui uliyoyakusudia.

Sina lengo, muda wala Nia ya kumpigia chapuo mtu hapa jukwaani wala nje yake ya na si mfuasi mzuri wa kuvutana hasa juu ya mabo ya kisiasa lakini; Tuulizane kidogo,
Mauaji ( ama yanayodhaniwa kuwa ni mauaji maana haijathibitishwa rasmi na vyombo husika)
yanahusishwa mojakwamoja na mgogoro ambao bila shaka kwa nukuu ya mleta Uzi una chanzo chake kabisa, Sasa ni kwanini kichwa kiwe namna kilivyo?
Kuna watu hata wakifumaniwa na.wagoni wao,bado lawama za kufamaniwa kwao watazipeleka kwa Serekali!!
 
Back
Top Bottom