Hata kipindi cha maombolezo hakijaisha tayari mnaombea upinzani wajitoe kwenye uchaguzi wa 2025? Mheshimiwa Rais hajasema bayana kuwa mikutano ya hadhara ya kisiasa inaruhusiwa, hajafanya mabiliko yeyote kwenye Tume ya Uchaguzi, hajazungumzia Katiba Mpya, hajazungumzia specifically watu waliokuwa na kesi za kubambikwa, hajazungumzia uhuru wa vyombo vya habari, hajazungumzia uhuru wa kupata na kutafuta taarifa, hajazungumzia wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni, hajazungumzia mikataba, hajazungumzia yaliyo mpata Lissu ( Kama Rais), hajazungumziwa uendeshwaji wa Bunge ikiwa pamoja na wale wabunge wakuteuliwa wa "Chadema", hajazungumzia Covid na mambo mengine mengi tu ambayo wapinzani wamekuwa wakiyahoji.
Ni kweli baadhi ya wapinzani wamepongeza baadhi ya hatua alizochukua katika upokeaji wa taarifa za CAG na TAKUKURU lakini safari bado ni ndefu.
Amandla...