Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Utawala wa SSH utakuwa tofauti na wa JPM kwa sababu nategemea yafuatayo


Haki za binadamu zitakuwepo

Demokrasia itakuwepo

Uhuru wa kuongea na kutoa maoni utakuwepo.

Uhuru wa habari utakuwepo.

Matumizi sahihi ya fedha za serikali yatakuwepo.

Hakutakuwa na kubambikizia watu kesi.

Atakusanya kodi na kuitumia vizuri

Hakutakuwa na upendeleo


Atakuwa mkali dhidi ya mafisadi.

Atatumbua kwa haki.

Hata ruhusu kujipendekeza pendekeza na kusifiwa kinafki.

Hakutakuwa na mauaji ya ajabu ajabu.
 
Ngoja awafokee tuone mtakavyomshukia hadi namuonea huruma...
Hulka yake haimruhusu kufokea. Kama jana amekaripia bila kufokea. Watu hawakatai kusahihishwa au kukaripiwa. Walichokuwa wanalalamikia ni kufokewa hadharani. Mheshimiwa nae akianza kufokea watu hadharani tutamshangaa na watu watamuuliza kulikoni?

Amandla...
 
Duh.. ni kazi kweli kweli... mbona Jaffo alishapigwa bit ya mwisho na Magu hivi majuzi tu... ila kichwa cha habari chahusika
Ya mwisho? Unajuaje ilikuwa ya mwisho wakati Rais amesema alishaonywa mara tatu hivi? Unajuaje kama angepigwa bit ya nne, ya tano na kuendelea? Rais leo kamwambia kwa utulivu tu kuwa anapwaya na asipojirekebisha ataondolewa kwenye hiyo nafasi. Bila kufokewa. Lakini Jaffo anajua bit ya tano ya tano haitakuja. Ni ama awajibike vizuri zaidi au nafasi atapewa mwingine. Bila kufokewa.

Amandla...
 
March 28, 2021
Utawala mpya Tanzania : Je, Rais Samia Suluhu Hassan atafuata nyayo za hayati John Pombe Joseph Magufuli : PART I

Prof. David O. Monda teaches political science at City University of New York's Guttman College

Je, Rais Samia Suluhu Hassan atafuata nyayo za hayati John Pombe Joseph Magufuli : PART II

Source : KTN News Kenya
 
Kwa mshangilio huo,inawezekana hata 2025 wasishiriki uchaguzi mkuu. Watamuacha mama Samia apite
Bado Wana Imani kubwa Sana na ccm
Hata kipindi cha maombolezo hakijaisha tayari mnaombea upinzani wajitoe kwenye uchaguzi wa 2025? Mheshimiwa Rais hajasema bayana kuwa mikutano ya hadhara ya kisiasa inaruhusiwa, hajafanya mabiliko yeyote kwenye Tume ya Uchaguzi, hajazungumzia Katiba Mpya, hajazungumzia specifically watu waliokuwa na kesi za kubambikwa, hajazungumzia uhuru wa vyombo vya habari, hajazungumzia uhuru wa kupata na kutafuta taarifa, hajazungumzia wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni, hajazungumzia mikataba, hajazungumzia yaliyo mpata Lissu ( Kama Rais), hajazungumziwa uendeshwaji wa Bunge ikiwa pamoja na wale wabunge wakuteuliwa wa "Chadema", hajazungumzia Covid na mambo mengine mengi tu ambayo wapinzani wamekuwa wakiyahoji.

Ni kweli baadhi ya wapinzani wamepongeza baadhi ya hatua alizochukua katika upokeaji wa taarifa za CAG na TAKUKURU lakini safari bado ni ndefu.

Amandla...
 
Mkuu hii ndio makala yenyewe au ni sehemu ya makala? Angalau kwa hotuba ya leo SSH sio JPM hata kwenye matamshi mfano tutaongeza wigo,tu(ni)
Ni kweli SSH ni ccm kama alivokuwa JPM ila kumsifia leo haimaanishi hatokosolewa kesho!
Umesema kweli. Nadhani ndoto za kuwa hatakosolewa kwa sababu ni mwanamke au anaongea kwa upole zitabakia kuwa ndoto tu. Na sidhani kama hata yeye mwenyeww atafurahia kuzungukwa na "praise team" peke yake. Ataona kama ni dharau fulani.

Amandla...
 
Fanya utafiti kidogo juu ya hali ya aviation industry duniani kabla hujaihukumu ATCL. Airlines zote zinapumulia machine!
Na ndio maana watu walishangaa uwekezaji mkubwa kwenye industry inayopumulia mashine. Kununua Dreamliner kabla ya kupata uhakika wa kuweza kusafiri kwenda nje na kama hata hao abiria wapo. Na hiyo hasara ya 60 bilioni ina walakin hasa ukizingatia hali ya Corona duniani na gharama za uendeshaji wa hizo ndege ambazo sio mpya tena.

Amandla...
 
Kwa kweli ana matatizo huyu Mzee. Au wanamuonea wivu Mama. Mh Samia kaanza vizuri sana. Jana ilikuwa gumzo kila mahali kuhusu yeye, wananchi kila kona wanasema wanafurahishwa nae. Sasa wale watu wa Jiwe wanasikia wivu [emoji41]. Ndio wanataka kulazimishia Samia ni Jiwe! HAPANA. Mama ni tofauti kabisaaa. Hapa tumepata na si kupatikana kama mwanzo.
 
Huyu naye anataka kuanzisha kundi la "gospel" ili amuwahi mama. Sidhani kama atakubali kulewa sifa kama mtukufu. Mama amefanya kazi na mtukufu na siyo kuwa hakuonja joto ya jiwe. Aliumia na hatapenda watu waumie kama alivyoumia yeye. Mama hatapenda watu wakose haki yao na hilo amelizungumza jana. Mtukufu alifurahi kuumiza watu, ilikuwa agenda yake na haitakuwa agenda ya mama
 
Nimetamani sana kulisoma na kulimaliza hili andiko lako, lakini haya maneno uloanza nayo yameonyesha kuna walakini.

"Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani"
mweeh.. sasa kwani siyo maneno ya kweli? mbona wapo na walishajipambanua hadharani?
 
Back
Top Bottom