Usitegemee furaha yako itoke kwa mwengine.Msataga ni wachawi nimegundua. Hawataki watanzania wote waishi kwa fraha na amani. Ni sawa na watoto wa mama mmoja ila baadhi hawapendi kuona wegine wakipendwa na mama yao. Acheni Roho mbaya. Mwenzenu mmeona kafa na kiroho chake
Ni kweli kabisa; sijasema wanafanana au wanatakiwa wafanane. Na kusema ukweli ni hiyo tofauti yao ndio inamfanya yeye kuwa mtu sahihi kuibeba ajenda yao kuliko mtu mwingine yeyote.Samia na Magufuli ni tofauti kubwa sana. Kama mbingu na ardhi.
Mbona ni kama watu wanafikiria nimesema Samia awe kama Magufuli? sijasema hivyo na siwezi kusema hivyo...Watashangaa sana Mwana mama atakapoanza kusimama mwenyewe bila kujiegemeza kwa yeyote.
Kwanza tayari ni kama amekwishaanza njia yake, kwa maamuzi machache anayofanya sasa hivi.
Hebu fikiria lugha yetu adhimu ya Kiswahili, yeye tayari kasema tofauti na yule aliyekuwa hataki kabisa kusikiliza kitu juu ya lugha nyingine mbali ya Kiswahili, kwa sababu zake mwenyewe.
Mwalimu Nyerere hakukataa lugha nyingine, pamoja na kwamba alikijenga sana Kiswahili.
Huyu naye anataka kuanzisha kundi la "gospel" ili amuwahi mama. Sidhani kama atakubali kulewa sifa kama mtukufu. Mama amefanya kazi na mtukufu na siyo kuwa hakuonja joto ya jiwe. Aliumia na hatapenda watu waumie kama alivyoumia yeye. Mama hatapenda watu wakose haki yao na hilo amelizungumza jana. Mtukufu alifurahi kuumiza watu, ilikuwa agenda yake na haitakuwa agenda ya mama
Watu wengine hamtakiwi kuingia kwenye biashara kabisa; kwamba mtu akipata hasara basi anatakiwa afunge biashara. Ingekuwa hili ni kweli kuna watu wasingeanzisha makampuni kabisa. Hoja ya "hasara" inaangaliwa kisiasa na si kibiashara. Kweli ni mfanyabiashara gani ambaye anaingia kwenye biashara bila kutarajia hasara au hata kupata hasara? Hata mkulima anayetaka kulima bila kutarajia kupoteza mavuno atashindwa kulima mwaka wa pili.Huyu mzee ni mpuuzi sana , Jiwe kaishakufa huelewi? Katuachia hasara ya mabilioni tusiseme ?View attachment 1737230
Na ndio maana watu walishangaa uwekezaji mkubwa kwenye industry inayopumulia mashine. Kununua Dreamliner kabla ya kupata uhakika wa kuweza kusafiri kwenda nje na kama hata hao abiria wapo. Na hiyo hasara ya 60 bilioni ina walakin hasa ukizingatia hali ya Corona duniani na gharama za uendeshaji wa hizo ndege ambazo sio mpya tena.
Amandla...
FM, hii hatari wanaitengeneza wenyewe. Sasa hivi walitakiwa waanze kujipanga kudai wanachotakiwa kudai.. wanatakiwa waujaribu uvumilivu wa Rais Samia.Hata kipindi cha maombolezo hakijaisha tayari mnaombea upinzani wajitoe kwenye uchaguzi wa 2025? Mheshimiwa Rais hajasema bayana kuwa mikutano ya hadhara ya kisiasa inaruhusiwa, hajafanya mabiliko yeyote kwenye Tume ya Uchaguzi, hajazungumzia Katiba Mpya, hajazungumzia specifically watu waliokuwa na kesi za kubambikwa, hajazungumzia uhuru wa vyombo vya habari, hajazungumzia uhuru wa kupata na kutafuta taarifa, hajazungumzia wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni, hajazungumzia mikataba, hajazungumzia yaliyo mpata Lissu ( Kama Rais), hajazungumziwa uendeshwaji wa Bunge ikiwa pamoja na wale wabunge wakuteuliwa wa "Chadema", hajazungumzia Covid na mambo mengine mengi tu ambayo wapinzani wamekuwa wakiyahoji.
Ni kweli baadhi ya wapinzani wamepongeza baadhi ya hatua alizochukua katika upokeaji wa taarifa za CAG na TAKUKURU lakini safari bado ni ndefu.
Amandla...
Yaani, mnaamini kabisa kuwa kila mtu aliyemuunga mkono JPM alikuwa ni Msukuma? Sijui tuuite huo ni ukabila wa namna gani. Kwa kifupi mimi siyo Msukuma...bado wasukuma mnawaza usukuma? mmeshkwa pabaya
tumuombe mwenyezi Mungu ampe hekima na busara mama yetu atuongoza kwa haki..
Mama akichukua mazuri ya JK na mazuri ya JPM akatuongoza basi nchi itapiga hatua haraka.. JK alikuwa na akili na mtazamo wa dunia ya sasa inavyotaka kufikia kwenye maendeleo, JPM alikuwa ni msimamizi na muangalizi mzuri kwenye rasimali na utendaji.. Mama akichukua vyote akavitumia kama silaha tutakwenda mbele...
Tatizo la CCM ni makundi, haya makundi ndio yanaweza kuwa kikwazo kwa mama, makundi yameota mizizi mpaka taasisi nyeti na kila kukicha yanaibuka makundi mapya..Ni wakati sasa wa viongozi wa haya makundi kuweka maslahi ya Taifa mbele na kuachana na minyukano yao...
Joby mujarabu! Endelea kushauri nchi yeti Kaka!Unatakiwa kuonesha "upumbavu" wangu; ila sijawahi kujali "kuvunjiwa" heshima. Inabidi unioneshe werevu wako ili nikupe heshima unayostahili.
Mkuuu, unaweza ukani pm huu ujumbe wa huyu TAGA MWANDAMIZI kwa ufupi!? Nimeshindwa kusoma mpaka mwisho!Yaani hapo umekula buku saba yako freshi uki present huu ushahidi wa bandiko
Kweli una muda na hauna kazi maalumu mpaka una muda wa kuandika kwa urefu wote huu, pole sana
Tafuta kazi ya ukweli ujikomboe kiakili..........
Yule msukuma mwenzenu alikuwa mkatili sana, furaha yake kubwa ilikuwa kuumiza wananchi,kuwapa makesi yasio na zamana kwa wale waliompinga au ambao sio wa upande wake, watu walikuwa wanatekwa ,Lakini ulikuwa wala umsikii kulizungumzia wala kufanya Chochote, so tunataka kiongozi ambae muungwana na mwenye kauli nzuri za utu, Madam President ni MTU sahihi Kutufanya watanzania tuwe na amani kwanza ya mioyo yetu, kwa kipindi chote cha Magu tumeishi kwa hofu mno jamaniHii ni imani tu...
Hulka yake haimruhusu kufokea. Kama jana amekaripia bila kufokea. Watu hawakatai kusahihishwa au kukaripiwa. Walichokuwa wanalalamikia ni kufokewa hadharani. Mheshimiwa nae akianza kufokea watu hadharani tutamshangaa na watu watamuuliza kulikoni?
Amandla...