Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Yule msukuma mwenzenu alikuwa mkatili sana, furaha yake kubwa ilikuwa kuumiza wananchi,kuwapa makesi yasio na zamana kwa wale waliompinga au ambao sio wa upande wake, watu walikuwa wanatekwa ,Lakini ulikuwa wala umsikii kulizungumzia wala kufanya Chochote, so tunataka kiongozi ambae muungwana na mwenye kauli nzuri za utu, Madam President ni MTU sahihi Kutufanya watanzania tuwe na amani kwanza ya mioyo yetu, kwa kipindi chote cha Magu tumeishi kwa hofu mno jamani

Mbona hajamsamehe Kakoko?
 
Yule msukuma mwenzenu alikuwa mkatili sana, furaha yake kubwa ilikuwa kuumiza wananchi,kuwapa makesi yasio na zamana kwa wale waliompinga au ambao sio wa upande wake, watu walikuwa wanatekwa ,Lakini ulikuwa wala umsikii kulizungumzia wala kufanya Chochote, so tunataka kiongozi ambae muungwana na mwenye kauli nzuri za utu, Madam President ni MTU sahihi Kutufanya watanzania tuwe na amani kwanza ya mioyo yetu, kwa kipindi chote cha Magu tumeishi kwa hofu mno jamani
We ulikuwa na sababu zako tu za kuishi na hofu.. kha! Mbona wengine tuliishi kwa amani tu...
 
Hauwajui watanzania wewe!!! hawa jamaa wavivu, wanafiki, waongo? wasio wabunifu?

yaani mtu anakosa kutengebeza daraja, gari zinakwama siku tatu usimfokee??

wamama waja wazito wanakufa na vichanga just kwa sababu ya poor planning usiwafokee??

Nani alionewa kati ya waliofokewa???

aisee
FM anasema ati watajisikia vibaya; anatakiwa awaite pembeni na kuwauliza kwa upole...
 
Unateseka ukiwa wapi ndugu Mganga njaa?

Jk aliwaweza sana kuwaita hilo jina[emoji16]
20210328_153143.jpg
 
yeah Ilani na ajenda ni ile ile... mengine uliyosema ni kweli. Unless kuna Ilani nyingine itapitishwa...
Hizo Ilani zingekuwa zinatekelezwa... Mbona Tanzania ingekuwa ilishaendelea miaka mingi iliyopita. Unless unataka kusema kuwa zimeanza kutekelezwa kipindi cha JPM.
 
Kwa mara ya kwanza wewe mzee nimekuelewa, wapinzani wanacheza ngoma ya Rais mpya kuanzia kule twitter kwa kiongozi wao mpaka huku chini, sijui wataamka lini, they really do need to change their political approach ASAP, otherwise it will be too late for them.

Sio kusema tunasubiri siku 100 za kwanza, hizo siku zinaweza kwisha bado pasiwepo na anything concrete ya kwenda kuwaambia wananchi, naamini huyu mama ataacha baadhi ya mambo ya utawala uliopita kama uminyaji haki za binadamu na utawala bora (kama ambavyo tumeona ACT imeshinda uchaguzi mdogo Znz), mpaka hapo atakuwa ame score marks kwa wananchi.

Nilitegemea hao viongozi wa upinzani right from the go wamwambie Rais tunataka Katiba Mpya, alijue hili mapema asubuhi, sio kupoteza muda mwingi kumsifia na kumwambia afanye vitu vidogo vidogo atavifanya vyote, wananchi wata adopt Rais mchapakazi, baadae opposition wakija ku-change kudai Katiba, akili za wengi zitakuwa zimeshazoea sifa alizopewa mwanzo, mwishowe wataishia kupata wabunge kadhaa tu maisha yaendelee.
 

Na. M. M. Mwanakijiji

Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani leo wanataka tuendelee kuamini kuwa chaguo lao limeingia madarakani sasa. Ndugu zetu hawa ndio wale huko nyuma na si mara moja wamekuwa wakisubiria kwa hamu "kitu" kitokee ili "mama" aingie madarakani. Tunawakumbuka hawa jinsi walivyosubiria kwa hamu wakati ule huku wakiposti picha za Makamu wa Rais kuwa ni suala la muda tu. Kama nitakavyoonesha katika makala yangu ya wiki hii (Gazeti la Raia Mwema) kwa baadhi ya watu kifo cha Magufuli hakikuja kwa mshtuko kivile; watu waliombea kisije kutokea lakini uwezekano wake ulikuwa mkubwa zaidi kuliko watu wengi walivyokuwa wanafikiria. Kwamba, sasa Rais Magufuli amefariki dunia basi ujio wa Mama Samia kwa ndugu zetu ni kama sala, dua, na maombi yao yamejibiwa. Katika kushangilia na kufurahia kwao ndugu zetu sasa wamekaa 'mkao wa kula' wakitegemea kuwa ndoto zao zote za Tanzania ya Samia zitatimia kwani haitokuwa ya Magufuli tena!

Yule mbaya wao, yule adui yao, yule kiongozi ambao hawakumtaka hayupo tena na sasa ameingia waliokuwa wamemtaka. Ndugu zetu hawa kwa uzuri au kwa ubaya sasa wamefikia mahali ya kutoa maelekezo, maombi, manuio, na hata matamanio yao chini ya Samia. Wanamuambia afanye nini kwanza, wanataka amtumbue nani kwanza, wanataka aanzie wapi kwanza ili waweze kuamini kuwa yuko nao. Wengine kwa wazi kabisa wanasema - tena siyo kusema wanamtaka aachane na 'mambo' ya Magufuli na akifanya hivyo basi wanaahidi kumuunga mkono na kuwa naye pamoja. Kwamba, hawatamnanga kama walivyomfanyia Magufuli na kuwa watampima Samia kwa jinsi gani anaenda mbali na siasa, mwelekeo, malengo na ajenda ya Magufuli. Ndugu zetu wanataka Samia awe "Rais" wao.

Wameacha kujipanga na uchaguzi, hawataki tena kutengeneza ajenda yao itakayowashindia uchaguzi, na hawataki kupambana kisiasa kushindana na CCM nyuma ya Samia. Wanataka kutengeneza "mgombea" wao na kudandia ajenda mpya ya Samia. Kwa kweli, inabidi tuwarudishe kwenye mstari wao ili wajipanga na kupambana na hali zao. Ajenda ya Samia bado ni ya Magufuli! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, hana ajenda yake tofauti na ya Magufuli. Samia hajauza ajenda yake katika uchaguzi wowote na hajapigiwa kura ya peke yake nje ya Magufuli. Kwa maneno mengine ni kuwa - na yeye mwenyewe ameshaelezea wakati huu wa maombolezo - kuwa ajenda ya Magufuli ya "hapa kazi tu" ipo pale pale! Hili halijawafurahisha sana ndugu zetu kwani wanataka aikane ajenda ya mtangulizi wake, aibeze, aipangue na kuitupilia mbali kama yale mapapai yaliyoambukizwa korona! Samia achukue ajenda ya wapinzani na kutawala nayo nchi huku akitupilia mbali mambo yote ya Magufuli!

Hata hivyo, wananchi wametuma salamu zao wazi, kamili, na hadharani; wamemlilia Magufuli kwa sababu walimuelewa. Hawakujificha wala kuona haya kujitokeza kumuombolezea Rais wao na kumlilia. Walimuaga kama shujaa aagwavyo. Ndugu zetu hawakutarajia hili wala kulitegemea. Wanaamini ukosoaji wao ndio pekee umejaa ukweli, maneno yao ni ya kuaminika tu na madai yao ndiyo pekee yenye kukubalika. Hawatakiwi kupingwa wala kukataliwa kwani ukiwafanyia hivyo wewe si muumini wa demokrasia. Kwamba, demokrasia ni kukubali, kukumbatia na kutetea yote yasemwayo nayo. Kwamba njia pekee sahihi, bora na ya kukubalika ya kutawala nchi ni ile inayopendekezwa nao. Usipoifuata njia hiyo basi wewe ni hatari kwa maslahi yao.

Huu ndio mtego wanaomtegea Mama Samia; kwamba aingie kwenye anga zao vinginevyo hawatochelewa kumgeuka. Hawa hawa ambao leo wanamuita "ni mama yao" ndio hawa hawa watamgeuka na kuanza kutukumbusha "uzuri" wa Magufuli. Hawa hawa wenye kumsifia ndo hawa hawa watamshukia siku viongozi wao watakapotiwa pingu kwa makosa au watakapozuiliwa kufanya wavitakavyo. Hatokuwa tena Rais wao na walimuita Magufuli "Jiwe" hawa hawa wataanza kumuita mama huyo "Chuma" a.k.a "Iron Lady". Na Samia asipokaa nao na kuwasikiliza na kuwakubalia na kuwapa matakwa yao ndugu zetu hawa wataanza tena kuzunguka duniani kutuambia "Yule Mwanamke Hawezi Kutawala Tanzania Angalau Magufuli...".

Bahati nzuri tupo ambao bado tunaamini ajenda ya Magufuli bado ni ajenda yenye nguvu, ya uhakika, na salama zaidi kwa Tanzania kupiga hatua ya haraka ya maendeleo. Kuiacha ajenda hiyo ni kuwaacha Watanzania zaidi ya asilimia 80 pembeni. Kuiacha ajenda hiyo itakuwa ni kuirudisha nchi yetu nyuma miaka ishirini na ushee. Na ni wazi kuiacha ajenda hiyo ni kukubali kushindwa. Samia akiacha ajenda ya Magufuli wapo wenye Wana-Magufuli (Pro-Magufuli) ambao nao watamuacha. Lakini hata yeye akiamua kuiacha haina maana hakuna watu walioiona na kuikubali ajenda hiyo ambao wanaweza kuisimamia na kuifufua huko mbeleni. Aliyekufa ni Magufuli na si ajenda yake ya "Tanzania Tunaweza". Samia akilirudisha taifa katika kuombaomba na kutokujiamini tena, akilirudisha taifa katika kujishukushuku basi Tanzania itaenda kuwa katika ubaya kuliko tunaoufikiria.

Tunapozungumzia ajenda ya Magufuli tusichanganye na namna Magufuli alivyotaka kuitekeleza ajenda hiyo. Samia asiwe kama Magufuli; hatutaki azungumze kama Magufuli au afanye kila kitu kama Magufuli. Kila mtu ameumbwa tofauti na ana hulka tofauti. Mama Samia anaweza kuitekeleza na kuipeleka mbele Tanzania bila kufanya kila kitu kama Magufuli. Na hapa ni muhimu Mama Samia awaweke sawa wote; wale wanaoombea asiwe kama Magufuli na wale ambao wanataka awe zaidi ya Magufuli; ni lazima atengeneza njia yake mwenyewe bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli wala kujaribu kuvaa viatu vyake. Ni lazima awaweke sawa wale wanaotaka achague Makamu wa Rais ambaye ataweza kufanya naye kazi, atakayeweza kumuamini, na ambaye likitokea lolote basi anaweza kuishikilia nchi. Na muhimu zaidi ni lazima awe mtu ambaye aliamini katika ajenda ya Magufuli na si NJE ya hapo. Mama Samia awe huru kumteua Makamu wa Rais anayeweza kushirikiana naye na kusimama naye; kuwa msiri wake, na afanye hivyo bila kuangalia Jinsia au Dini ya mtu huyo na kwa maoni yangu ni lazima awe mtu ASIYEUTAKA URAIS au aliyewahi kuonesha kiu na hamu ya kuwa Rais.

Kama nilivyosema hapo juu ajenda ya Magufuli ndiyo inaongoza nchi hadi 2025. Kama Mama Samia au MwanaCCM yeyote mwingine ana ajenda nyingine basi huyo ajiandae 2025. Mama Samia anaweza kuwa na ajenda yake; lakini hiyo itabidi aiandae 2025 (na wengine tayari tupo nyuma yake kwani tayari tunamuaini kwa vile tu alikuwa nyuma ya Magufuli). Kwa sasa hata hivyo, yeye na uongozi mzima wa nchi unatakiwa kuendelea na ajenda ya Magufuli. Na ili afanikiwe ni lazima ipange serikali yake kwa namna yake yeye na jinsi anavyoweza kuona inamfaa kuongoza nchi kuelekea 2025. Si lazima arithi na kuendelea na kila kiongozi aliyeteuliwa na Magufuli; wale ambao anaona wanapwaya au tayari walishaona wanapwaya ni lazima AWAPANGUE bila aibu. Sasa hivi ni lazima atume ujumbe wa haraka kuwa HAKUNA aliyesalama kwenye cheo chake; kila mtu ni lazima astahili kuwepo kwenye serikali yake. Na katika kufanya hivyo ndio anaweza KUSAHIHISHA makosa ya Magufuli, kujenga katika MAFANIKIO yake na kuongoza kuelekea MALENGO yote yaliyokuwa yanawezekana chini ya AJENDA YA MAGUFULI.

Hii ni kwa sababu AJENDA YA SAMIA ni bado AJENDA YA MAGUFULI hadi 2025.

#TukonaSamia2025.
Hawa unaowaita "ndugu zetu" ni wewe mwenyewe. Wewe ni miongoni mean watu ambao wamedurahia sana kifo cha mpendwa wetu ila unajifanya kujiweka kando na kusema "hawa ndugu zetu" kutaka kuaminisha watu unazungumzia wapinzani na kwamba wewe si mmoja wao.
Nadhani ni wakati sasa wa kuacha unafiki. Unavaa ngozi ya kondoo wakati ndani ni mbwa mwitu mkali.
Watu tunakujua vizuri. Unachofanya ni kujaribu kwenda na upepo, jambo ambalo halikusaidii sana kwa sasa.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kabisa; sijasema wanafanana au wanatakiwa wafanane. Na kusema ukweli ni hiyo tofauti yao ndio inamfanya yeye kuwa mtu sahihi kuibeba ajenda yao kuliko mtu mwingine yeyote.
Nani alieandika wanafanana? Usilete ujuha wako wa kizamani wa kucheza na maneno.

JF wote wa zamani tunakufahamu unafik wako.
 
Sasa kama Tanzania ya Samia ni ya Magufuli, sisi tufanyeje?

Mbona nyie watu wa CCM na hasa chawa wa The late Magu mnajishtukia sana? Shida ni nini?

Kubalini mambo yamebadilika, mkiweza hamishieni tu pambio kwa Bi. Mdashi.

Kakoko si aliteuliwa na Magu, hata kwenye ubadhirifu wa mwaka jana kwenye report ya CAG ilionekana? Alichukuliwa hatua gani? Huyu Jaffo si muda wote akiwa kwenye maziara kila baada ya maneno 10 anataja Magufuli!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Wamepotezana! Bado mzimu wa Magu utawaandama sana. Ukweli ni kwamba Magu hayupo na hatakuwepo tena na wasijaribu kupingana na mapenzi ya Mungu.
Mungu anataka tumsifu na kumwabudu yeye na kwake kila goti litapigwa na si kwa mwanadamu awaye yote.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Acha wenge na ujinga wewe mzee!
Lini magufuli alikubali kwamba kuna kesi za kubambikia ambazo hazieleweki?
Lini magufuli alionesha kutuunganisha zaidi ya kutugawanya kama taifa?
Lini magufuli alikubali taarifa sahihi za mkaguzi mkuu wa serikali ziwekwe hadharani na akazifanyia kazi zaidi ya kutaka kujionyesha kuwa kila sekta kapata faida?

Narudia tena kukwambia acha kujitoa ufahamu kwa sababu zako binafsi!

Utawala wa mama yetu Samia una matendo ya haki na uwajibikaji tofauti na buldoza ambaye kazi yake ilikuwa kusifiwa tu hata kama kanya nje mchana wa saa sita.

Magufuli hata kwenye shirika la ndege alipenda kujisifia kuwa kapata faida ambapo ilikuwa kinyume!

Alivuruga umoja wa kitaifa ila mama kaja kutuunganisha ndio maana unaona makundi yote ndani ya taifa hili kuanzia na wapinzani wapo pamoja na mama.

Kama bado ungali ukiona huu ni utawala unafanana na utawala wa Magufuli basi utakuwa na tatizo la akili.

Nenda miembe ukatibiwe...
Bado ana wenge nadhani hata akuona picha ya Magu anaipigia magoti kuisujudia !

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni kwamba at least as of now tunaanza kuona mwanga flani..hakuna tena hotuba za kibabe...hakuna kutishiana maisha. Hakuna hotuba za kejeli na kujimwambafyi. Mama samia toka ameapishwa mpaka leo amesimamia misingi ya utawala bora na kufuata katiba. Anajaribu kila awezalo kubalance mambo yet unaleta propaganda zako za kishenzi kwamba hakuna lililobadilika na kuwa everything is the same. Nakuhakikishia this is the beginning of the new era/regime na kama usipobadilisha attitude yako you will soon loose relevance katika jamii ya wasomi wa makala zako na hao wanaokutuma wataacha kukutuma tena maana you will have lost your purpose and eventually be of no any use to them.
Tell him ! Anatafuta namna ya kupenyeza mapambio ndo maana anataka kutuaminisha Samia na Magufuli ni kitu kimoja. Idiot !

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom