Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Yaani, mnaamini kabisa kuwa kila mtu aliyemuunga mkono JPM alikuwa ni Msukuma? Sijui tuuite huo ni ukabila wa namna gani. Kwa kifupi mimi siyo Msukuma...
Tatizo Mkuu ni kuwa shutuma hizi zilianza mapema na sikumbuki kama uliwahi kusema kuwa wewe sio msukuma wakati wa utawala wa Marehemu.

Amandla....
 
yaani, unafikiri kuna mtu anaweza kunituma kuandika kitu? yaani wiki hii tu tayari mmejua hakuna tena ubabe au kutishana maisha... ngoja awageuka mtamsemaaaa...
Atugeuke atu teke au atu uwe?
Kwani kuna kitu katu ahidi?
APA tatizo ni upendo kwa Mama au tatizo ni nini?
 
Ni kweli Samia ni ccm lakini katu hawezi kuchukua Tabia na mwenendo wa Magufuli , Samia hatoivunja Ilani ya ccm wala hataiweka ccm mfukoni
Ndio maana ccm itatawala milele.Yaa wewe kada wa chadema unaiombea mazuri ccm!
Wiki ijayo tunakwenda kumkabidhi chama ili aweze kukitia mfukoni mwake.Ccm ni ile ile tu aliebadilika ni nahodha
 
Hao wa

Na. M. M. Mwanakijiji

Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani leo wanataka tuendelee kuamini kuwa chaguo lao limeingia madarakani sasa...
Hao wapinzani ni namna yao ya kupumua chuki waliyokuwa nayo dhidi ya JPM.

Samia kama Rais atatekeleza yale yale aliyokuwa anatekeleza JPM kwa sababu ilani ni ile ile. Ila approach itakuwa tofauti sababu hapa duniani hakuna mtu ambaye ni kopi ya mwingine.

Kule twita yule mama yeye ni kumshambulia JPM tu lakini ukatili uliofanywa na babu yake kule Zanzibar wakati wa utawala wake hata siku moja hauzungumzii wala kumlaumu. Vilevile yule mama mwingine baba yake alikuwa waziri wakati wa kashfa ya meremeta ambapo mabilioni yaliibwa pengine ndizo anazokula hadi leo huko aliko anakoendesha mtandao wa kumkashifu JPM lakini hazungumzii huo wizi.

Watanzania wamegawanyika makundi mawili tu bila kujali vyama vyetu. Kundi la kwanza ni wezi/mafisadi na kundi la pili ni wale tunaopinga wizi/ ufisadi. Hao exiled maslahi yao ya wizi yaliathiriwa na JPM ndio sababu kuu ya kumchukia.
 
Nafikiri watu hawajamuelewa mleta uzi kwamba anachomaanisha Madame President alikua mgombea mwenza na aliihubiri ilani ya Hapa Kazi Tu hivyo ni ilani hiyo hiyo itakayofanya kazi mpaka 2025 atakapogombea na kuja na ilani yake.

Hii ni ukweli ila nafikiri approach zitatofautiana.

Binafsi nafikiri dalili kuu ya kwamba approach yake itakua tofauti ni kuachia mtandao (twitter).
 
Mimi nipo na [emoji897] naangalia hizi moves! Speculations, determinations, Political analysis atmosphere [emoji41] ...ngoja niongeze na [emoji477]
 
Hakuna utawala duniani unaoweza kufanana na mwingine. Hakuna. Hata Mao wa china alipofariki wafuasi wake waliahidi kufata nyayo zake lakini walishindwa kutokana na mazingira ya muda. Tusisahau pia hata Rais Nyerere alisema tuendeleze siasa, sera, utendaji na maono mema aliyosimamia na kuachana na mapungufu ya utawala wake. Thats the right way to go.
 
Mbona mgawanyo wa fedha uko sawa tu, yaani mlitegemea serikali isilipe watoa huduma, hivi mnadhani pesa ya serikali inachukuliwa kama tango shambani.Mnaowachafua wataibuka kidedea. Hongera sana mama kwa kumuagiza CAG na Gavana ili waongo waaibike, subirini ripoti na muwe tayari kupokea matokeo ya ukaguzi
 
Upumbavu wako ni pale unalazimisha watu wampinge samia ata kama kafanya jambo jema . Upinzani upo kwajili ya kukosoa pale penye makosa na kama pana mazuri wanaunga mkono pia upumbavu wako mwingne rais ni wa wananch wote co wa chama wew ulizoea jpm alivokua mchama ukaisi ni sahihi rais hatakiwi kuwa upande wowote ktk utendaj wake na wananch tunamuona ni rais wetu wote
Nachojua wapinzani wanaounga mkono kwenye yale wanayoona ni mazuri huwa wanaishia kuitwa wasaliti,upinzani huwa unasema kuwa wao kazi yao ni kukosoa na si kupongeza. Nakumbuka hadi Jk akawaambia mnaona mabaya tu mazuri hamuyaoni?
 
Mkuu mkurugenzi wa TPA ukiweka mwanajeshi utaleta nidhamu na uadilifu. Raisi JPM alikuwa anajua A-Z ya Ela tunayopata bandari ya Dar na alitamani itumike na nchi nyingi mpaka akazungumza na wafanyabiashara kutoka DRC walioanza kutumia bandari zingine.

Huko aliweka hao wanajeshi, akabadili mpaka mkuu wa kitengo Cha Port Security.Tatizo kubwa ni watu aliokuwa akiwaweka wengi hawakufanya yale aliyotaka walimuangusha.

Saizi itumike approach aliyokuwa nayo Mzee Kikwete ya kuwachukua Diaspora waliosoma Port Management na kufanya kazi kwenye bandari kubwa duniani waje walete matokeo chanya. Hata hapa nyumbani kuna watanzania wamesoma Port and Shipping Management vyuo vikubwa kama World Maritime University kwa udhamini wa serikali na wamerudi wapo serikalini tuwatumie.

Huu utaratibu wa kumtoa mtu Tanroad/Tanesco/Wizarani na kuwa mkurugenzi kama tunataka tuwe na bandari ya kisasa, inayozalisha na kuhudumia ukanda huu lazima tutumie watanzania wenzetu wenye utalaamu wa uongozaji bandari.
 
Back
Top Bottom