Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

yeah Ilani na ajenda ni ile ile... mengine uliyosema ni kweli. Unless kuna Ilani nyingine itapitishwa...

Ni hivi, Mungu ameamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika kwa kumuondoa mtu dhalimu, yale maelezo yako ya post namba moja ni kujiweka vizuri kisaikolojia baada ya muovu uliyekuwa unamsujudia kuelekea motoni. Huyo unayetaka ajenda zake zifuatwe alikuwa anatamba kuwa kila zama na kitabu chake, kwa acha huyu mama naye afungue kitabu chake. Hizo ajenda zake subirini siku akikaaa msukuma mwingine.

Na kwa taarifa yako hakushinda kihalali kwenye uchaguzi, hivyo huyo mama hana ulazima wowote wa kufuata ajenda ambazo hata yeye anajua hazikupigiwa kura na watanzania wengi.
 
Ni kama watu wanajitahidi kuukataa ukweli. Wanaombea usiwe ukweli...Mama Samia hana ajenda yake Wala ahadi zake... Ameingia kumalizia ngwe ya pili Rais Magufuli. Sasa ataimalizaje bila kuangalia ahadi zao jwa wananchi?
Watu wanachoamini ni kwamba hatakuwa na agenda za kuua watu, kunyanyasa wapinzani kama vile hawako kisheria nchini, kuminya uhuru ambao uko kisheria, double standards.
Jamani jamani mzee wetu mbona huelewi jambo liko wazi kabisa.
Watu walichukia aproach za mzee yule ambazo ziliumiza wengi saana.
Unataka waanze kumpinga mama ili nini au kwa sababu iipi?
Nashangaa kukuona mzee wangu Pamoja na kuishi huko dunia ya kwanza baado huoni watu wanachosimamia hapa.
Unajitoa ufahamu kabisa kwa sababu ambazo hazituleti Pamoja kama taifa.
Akikosea atakosolewa lakin si sasa ambapo bado hakuna sababu.
Wewe una agenda yako ambayo bado mda kidogo itakua bayana.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani leo wanataka tuendelee kuamini kuwa chaguo lao limeingia madarakani sasa. Ndugu zetu hawa ndio wale huko nyuma na si mara moja wamekuwa wakisubiria kwa hamu "kitu" kitokee ili "mama" aingie madarakani. Tunawakumbuka hawa jinsi walivyosubiria kwa hamu wakati ule huku wakiposti picha za Makamu wa Rais kuwa ni suala la muda tu. Kama nitakavyoonesha katika makala yangu ya wiki hii (Gazeti la Raia Mwema) kwa baadhi ya watu kifo cha Magufuli hakikuja kwa mshtuko kivile; watu waliombea kisije kutokea lakini uwezekano wake ulikuwa mkubwa zaidi kuliko watu wengi walivyokuwa wanafikiria. Kwamba, sasa Rais Magufuli amefariki dunia basi ujio wa Mama Samia kwa ndugu zetu ni kama sala, dua, na maombi yao yamejibiwa. Katika kushangilia na kufurahia kwao ndugu zetu sasa wamekaa 'mkao wa kula' wakitegemea kuwa ndoto zao zote za Tanzania ya Samia zitatimia kwani haitokuwa ya Magufuli tena!

Yule mbaya wao, yule adui yao, yule kiongozi ambao hawakumtaka hayupo tena na sasa ameingia waliokuwa wamemtaka. Ndugu zetu hawa kwa uzuri au kwa ubaya sasa wamefikia mahali ya kutoa maelekezo, maombi, manuio, na hata matamanio yao chini ya Samia. Wanamuambia afanye nini kwanza, wanataka amtumbue nani kwanza, wanataka aanzie wapi kwanza ili waweze kuamini kuwa yuko nao. Wengine kwa wazi kabisa wanasema - tena siyo kusema wanamtaka aachane na 'mambo' ya Magufuli na akifanya hivyo basi wanaahidi kumuunga mkono na kuwa naye pamoja. Kwamba, hawatamnanga kama walivyomfanyia Magufuli na kuwa watampima Samia kwa jinsi gani anaenda mbali na siasa, mwelekeo, malengo na ajenda ya Magufuli. Ndugu zetu wanataka Samia awe "Rais" wao.

Wameacha kujipanga na uchaguzi, hawataki tena kutengeneza ajenda yao itakayowashindia uchaguzi, na hawataki kupambana kisiasa kushindana na CCM nyuma ya Samia. Wanataka kutengeneza "mgombea" wao na kudandia ajenda mpya ya Samia. Kwa kweli, inabidi tuwarudishe kwenye mstari wao ili wajipanga na kupambana na hali zao. Ajenda ya Samia bado ni ya Magufuli! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, hana ajenda yake tofauti na ya Magufuli. Samia hajauza ajenda yake katika uchaguzi wowote na hajapigiwa kura ya peke yake nje ya Magufuli. Kwa maneno mengine ni kuwa - na yeye mwenyewe ameshaelezea wakati huu wa maombolezo - kuwa ajenda ya Magufuli ya "hapa kazi tu" ipo pale pale! Hili halijawafurahisha sana ndugu zetu kwani wanataka aikane ajenda ya mtangulizi wake, aibeze, aipangue na kuitupilia mbali kama yale mapapai yaliyoambukizwa korona! Samia achukue ajenda ya wapinzani na kutawala nayo nchi huku akitupilia mbali mambo yote ya Magufuli!

Hata hivyo, wananchi wametuma salamu zao wazi, kamili, na hadharani; wamemlilia Magufuli kwa sababu walimuelewa. Hawakujificha wala kuona haya kujitokeza kumuombolezea Rais wao na kumlilia. Walimuaga kama shujaa aagwavyo. Ndugu zetu hawakutarajia hili wala kulitegemea. Wanaamini ukosoaji wao ndio pekee umejaa ukweli, maneno yao ni ya kuaminika tu na madai yao ndiyo pekee yenye kukubalika. Hawatakiwi kupingwa wala kukataliwa kwani ukiwafanyia hivyo wewe si muumini wa demokrasia. Kwamba, demokrasia ni kukubali, kukumbatia na kutetea yote yasemwayo nayo. Kwamba njia pekee sahihi, bora na ya kukubalika ya kutawala nchi ni ile inayopendekezwa nao. Usipoifuata njia hiyo basi wewe ni hatari kwa maslahi yao.

Huu ndio mtego wanaomtegea Mama Samia; kwamba aingie kwenye anga zao vinginevyo hawatochelewa kumgeuka. Hawa hawa ambao leo wanamuita "ni mama yao" ndio hawa hawa watamgeuka na kuanza kutukumbusha "uzuri" wa Magufuli. Hawa hawa wenye kumsifia ndo hawa hawa watamshukia siku viongozi wao watakapotiwa pingu kwa makosa au watakapozuiliwa kufanya wavitakavyo. Hatokuwa tena Rais wao na walimuita Magufuli "Jiwe" hawa hawa wataanza kumuita mama huyo "Chuma" a.k.a "Iron Lady". Na Samia asipokaa nao na kuwasikiliza na kuwakubalia na kuwapa matakwa yao ndugu zetu hawa wataanza tena kuzunguka duniani kutuambia "Yule Mwanamke Hawezi Kutawala Tanzania Angalau Magufuli...".

Bahati nzuri tupo ambao bado tunaamini ajenda ya Magufuli bado ni ajenda yenye nguvu, ya uhakika, na salama zaidi kwa Tanzania kupiga hatua ya haraka ya maendeleo. Kuiacha ajenda hiyo ni kuwaacha Watanzania zaidi ya asilimia 80 pembeni. Kuiacha ajenda hiyo itakuwa ni kuirudisha nchi yetu nyuma miaka ishirini na ushee. Na ni wazi kuiacha ajenda hiyo ni kukubali kushindwa. Samia akiacha ajenda ya Magufuli wapo wenye Wana-Magufuli (Pro-Magufuli) ambao nao watamuacha. Lakini hata yeye akiamua kuiacha haina maana hakuna watu walioiona na kuikubali ajenda hiyo ambao wanaweza kuisimamia na kuifufua huko mbeleni. Aliyekufa ni Magufuli na si ajenda yake ya "Tanzania Tunaweza". Samia akilirudisha taifa katika kuombaomba na kutokujiamini tena, akilirudisha taifa katika kujishukushuku basi Tanzania itaenda kuwa katika ubaya kuliko tunaoufikiria.

Tunapozungumzia ajenda ya Magufuli tusichanganye na namna Magufuli alivyotaka kuitekeleza ajenda hiyo. Samia asiwe kama Magufuli; hatutaki azungumze kama Magufuli au afanye kila kitu kama Magufuli. Kila mtu ameumbwa tofauti na ana hulka tofauti. Mama Samia anaweza kuitekeleza na kuipeleka mbele Tanzania bila kufanya kila kitu kama Magufuli. Na hapa ni muhimu Mama Samia awaweke sawa wote; wale wanaoombea asiwe kama Magufuli na wale ambao wanataka awe zaidi ya Magufuli; ni lazima atengeneza njia yake mwenyewe bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli wala kujaribu kuvaa viatu vyake.

Ni lazima awaweke sawa wale wanaotaka achague Makamu wa Rais ambaye ataweza kufanya naye kazi, atakayeweza kumuamini, na ambaye likitokea lolote basi anaweza kuishikilia nchi. Na muhimu zaidi ni lazima awe mtu ambaye aliamini katika ajenda ya Magufuli na si NJE ya hapo. Mama Samia awe huru kumteua Makamu wa Rais anayeweza kushirikiana naye na kusimama naye; kuwa msiri wake, na afanye hivyo bila kuangalia Jinsia au Dini ya mtu huyo na kwa maoni yangu ni lazima awe mtu ASIYEUTAKA URAIS au aliyewahi kuonesha kiu na hamu ya kuwa Rais.

Kama nilivyosema hapo juu ajenda ya Magufuli ndiyo inaongoza nchi hadi 2025. Kama Mama Samia au MwanaCCM yeyote mwingine ana ajenda nyingine basi huyo ajiandae 2025. Mama Samia anaweza kuwa na ajenda yake; lakini hiyo itabidi aiandae 2025 (na wengine tayari tupo nyuma yake kwani tayari tunamuaini kwa vile tu alikuwa nyuma ya Magufuli). Kwa sasa hata hivyo, yeye na uongozi mzima wa nchi unatakiwa kuendelea na ajenda ya Magufuli. Na ili afanikiwe ni lazima ipange serikali yake kwa namna yake yeye na jinsi anavyoweza kuona inamfaa kuongoza nchi kuelekea 2025.

Si lazima arithi na kuendelea na kila kiongozi aliyeteuliwa na Magufuli; wale ambao anaona wanapwaya au tayari walishaona wanapwaya ni lazima AWAPANGUE bila aibu. Sasa hivi ni lazima atume ujumbe wa haraka kuwa HAKUNA aliyesalama kwenye cheo chake; kila mtu ni lazima astahili kuwepo kwenye serikali yake. Na katika kufanya hivyo ndio anaweza KUSAHIHISHA makosa ya Magufuli, kujenga katika MAFANIKIO yake na kuongoza kuelekea MALENGO yote yaliyokuwa yanawezekana chini ya AJENDA YA MAGUFULI.

Hii ni kwa sababu AJENDA YA SAMIA ni bado AJENDA YA MAGUFULI hadi 2025.

#TukonaSamia2025.
Wote tupo na
Nimetamani sana kulisoma na kulimaliza hili andiko lako, lakini haya maneno uloanza nayo yameonyesha kuna walakini.

"Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani"
Huyu mwandishi akasome katiba,kama imeandikwa kwa lugha ya kiingereza akamtafute yule mkalimani wa dodoma,amtafsirie.Mama Samia ni Rais Wa Tanzania na halazimiki kufuata mienendo au sera za watangulizi wake wote.Pia hivi karibuni atakuwa mwenyekiti mpya wa chama chake CCM.Anaweza hata kubadilisha kwa kupitia ngazi husiks baadhi ya sera za Chama chake.
 
Watu wanachoamini ni kwamba hatakuwa na agenda za kuua watu, kunyanyasa wapinzani kama vile hawako kisheria nchini, kuminya uhuru ambao uko kisheria, double standards.
Jamani jamani mzee wetu mbona huelewi jambo liko wazi kabisa.
Watu walichukia aproach za mzee yule ambazo ziliumiza wengi saana.
Unataka waanze kumpinga mama ili nini au kwa sababu iipi?
Nashangaa kukuona mzee wangu Pamoja na kuishi huko dunia ya kwanza baado huoni watu wanachosimamia hapa.
Unajitoa ufahamu kabisa kwa sababu ambazo hazituleti Pamoja kama taifa.
Akikosea atakosolewa lakin si sasa ambapo bado hakuna sababu.
Wewe una agenda yako ambayo bado mda kidogo itakua bayana.
Wao wanafikiri ukiwa mpinzani hata vitu vya msingi ni kupinga huo ndio ugonjwa wa Watanzania walio wengi Mama Mungu amempa hicho kiti inabidi tumpe moyo na tujipongeze kwa kumpata rais mwanamke wa kwanza Tanzania.
 
Ni kama watu wanajitahidi kuukataa ukweli. Wanaombea usiwe ukweli...Mama Samia hana ajenda yake Wala ahadi zake... Ameingia kumalizia ngwe ya pili Rais Magufuli. Sasa ataimalizaje bila kuangalia ahadi zao jwa wananchi?
Mzee mimi nje ya mada kidogo. Kuna watu wameanza kampeni ya kumchafua Magufuli baba yetu ili waifute legacy yake wanadanganya watu mitaani eti nae alikuwa fisadi. Nisaidie awa watu tupambane nao vipi maana wanakera sana, najua wewe una thinking capacity kubwa unaweza shauri kitu. thanks
 
Kwa hiyo hao watanzania wanaodanganywa hawakuishi enzi za Magu wakaona aliyoyafanya?
Ni kama juzi kwenye msiba wake tunaimbiwa uzalendo wa Magu kama vile tumezaliwa siku aliyokufa.
Yaani kana kwamba watu hawana akili ya kujudge mpk waambiwe na fulani.
Ukweli utasimama daima kwamba alikuwa na makando mengi mno ndio maana wakatumia msiba wake kumshafisha na bado ndani ya siku moja kaburini mambo yake yanawekwa bayana ya kutochukua hatua kwa baadhi ya watu hata pale iliostahili.
 
Pambana na hali yako mwenyewe
 
Mzee mimi nje ya mada kidogo. Kuna watu wameanza kampeni ya kumchafua Magufuli baba yetu ili waifute legacy yake wanadanganya watu mitaani eti nae alikuwa fisadi. Nisaidie awa watu tupambane nao vipi maana wanakera sana, najua wewe una thinking capacity kubwa unaweza shauri kitu. thanks
Interesting[emoji848]
 
Unakumbuka wakati JK anamkabidhi JPM nchi namna JK alivyokuwa anasemwa na hao chadema wakasema bandari imejaa makontena ya JK? twiga anapanda ndege, sheli za oilcom ziliitwa za rizwan nk

Leo Chadema shujaa wao ni JK.

Ipo siku sio mbali wataimba mazuri ya JPM awa awa Chadema. Subiri Samia aanze minyoosho acha wamjaribu.

Usiwe na mashaka kabisa na matusi ya Chadema ni ya muda tu wala yasikuumize. JPM ameacha legacy kubwa sana itaenda vizazi vingi.
 
Ni kama watu wanajitahidi kuukataa ukweli. Wanaombea usiwe ukweli...Mama Samia hana ajenda yake Wala ahadi zake... Ameingia kumalizia ngwe ya pili Rais Magufuli. Sasa ataimalizaje bila kuangalia ahadi zao jwa wananchi?

Wala issue sio ajenda, bali watu wanajua baradhuli hayupo tena. Hizo ajenda za kujenga nchi zipo toka enzi ya mkoloni, hakuna lolote special sasa hadi ujifanye kuanzisha uzi.

Huu uzi wako ni kama unataka kumtishia huyo mama alazimike kufuata mambo ya Magu. Kwa jinsi alivyokuwa na kiburi cha madaraka, iwapo ni yeye angekuwa kachukua hiyo nafasi, angeendeleza ajenda za mtangulizi wake? Ww sema unajitutumua kulazimisha watu waone kama alikuwa na ajenda sana, kumbe dhalimu tu.
 
Kwa hiyo hao watanzania wanaodanganywa hawakuishi enzi za Magu wakaona aliyoyafanya?
Ni kama juzi kwenye msiba wake tunaimbiwa uzalendo wa Magu kama vile tumezaliwa siku aliyokufa.
Yaani kana kwamba watu hawana akili ya kujudge mpk waambiwe na fulani.
Ukweli utasimama daima kwamba alikuwa na makando mengi mno ndio maana wakatumia msiba wake kumshafisha na bado ndani ya siku moja kaburini mambo yake yanawekwa bayana ya kutochukua hatua kwa baadhi ya watu hata pale iliostahili.

Kwenye msiba ndio tumeona reality ni kiasi gani Magufuli alikuwa anakubalika na wananchi wengi, pamoja na upotoshaji mkubwa uliofanywa na chadema mitandaoni.

watu tunampenda Magufuli for life ata mmchafue vipi..tunajua alivyotupenda na kutupigania
 
Back
Top Bottom