Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Siyo kweli kuwa filosofia ya ubebari ni asiyefanya kazi na asile. Kwenye ubebari unaweza kuwa mchapa kazi mzuri sana sana lakini ukashia kuishi maisha ya kifukara mno.
Kuchapa Kazi sio kupata.Unaweza ukachapa Kazi bila maarifa ya kupata.Kwenye ubepari mzunguko wa pesa ni Mkubwa purchasing power ni kubwa Sana biashara yeyeto inatoka
 
Kuchapa Kazi sio kupata.Unaweza ukachapa Kazi bila maarifa ya kupata.Kwenye ubepari mzunguko wa pesa ni Mkubwa purchasing power ni kubwa Sana biashara yeyeto inatoka
Unajua maana ya ''kuchapa kazi''? Kuchapa kazi ni term inayo-include vipengele vingi ikiwa ni pamoja na maarifa. Kuchapa kazi minus maarifa maana yake siyo kuchapa kazi.
 
Unajua maana ya ''kuchapa kazi''? Kuchapa kazi ni term inayo-include vipengele vingi ikiwa ni pamoja na maarifa. Kuchapa kazi minus maarifa maana yake siyo kuchapa kazi.
Sasa Kama unachapa Kazi na mzunguko mzuri wa pesa zipo mtaani unakuwa vipi masikini sasa.vibarua vimejaa tele, viwanda Kama uyoga, watu wanapesa mfukoni hapa unakuwa vipi masikini sasa.
 
Umeandika utumbo wa kiwango cha lami..

Uko biased sana. Asingekuwa yeye kungekuwa na wengine.. [emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Ubebari ni unyonyaji! Ndugu yangu jaribu kutembelea nchi za Scandinavia ndiyo utajua ukweli wa msemu huu. Kule mfumo wao unaweza kudhani ni ujamaa wa aina fulani lakini wananchi wake wana maisha mazuri sana kuliko hata Marekani.

Ubepari ndio unawafanya wanapata huduma zote za kijamii. Ni ubepari ndio unakuza uchumi wao sio huu Ujima
 
Sasa Kama unachapa Kazi na mzunguko mzuri wa pesa zipo mtaani unakuwa vipi masikini sasa.vibarua vimejaa tele, viwanda Kama uyoga, watu wanapesa mfukoni hapa unakuwa vipi masikini sasa.
Hapo ''chacha''! Tashwish yako inaonyesha somo limekuingia. Unakuwa maskini kwa sababu ubebari ni unyama. Utafanya vibarua sana, utamenyeka sana lakini malipo utapewa kidogo. Kumbuka unaweza kukuta viwanda vinamilikiwa na watu wachache na wao ndiyo hupanga malipo.
 
Umasikini unaletwa na sera mbovu za ujamaa za kuwafanya matajiri wawe masikini ili watawaliwe
 
Nyerere alikuwa ni kiongozi mzuri lakini UJAMAA was a disaster: An unmitigated disaster.
 
Waliokuwa wanapeleka maneno kwa Mzee Nyerere dhidi ya Kambona ni wakina Peter Siyovelwa na Emilio Mzena: Hawa ndiyo waliofanya fitina dhidi ya Kambona, hasahasa Siyovelwa ambaye ndiye alikazia sana jamaa ashughulikiwe.

Lakini upande mwingine wa shilingi wazungu walikuwa hawataki kutoka Tanzania na kuachishwa kazi zao. Earl Seaton anasema moja ya masharti aliyopewa Nyerere kwenye Uhuru wa Tanganyika ni kuhakikisha kwamba hawatawafukuza wafanyakazi wa Tanganyika wenye asili ya Uingereza. Katika hili walifanya kabisa hadi makubaliano ambayo yaliwekwa kwenye karatasi, hivyo haikuwa rahisi kwa Nyerere kuwaondoa.

Yote tisa, kuna mengi yamefichika hapa: Kambona kama waziri alikuwa na nguvu sana wakati uasi unatokea, na kama angekuwa anautaka Uraisi wa Tanganyika basi asingemchelewesha Nyerere. Matukio ya kwenye uasi yanadhihirisha kabisa kwamba Kambona alikuwa ni mtu muungwana. Haingii akilini mtu apange uasi halafu yeye mwenyewe ndiyo asaidie kuwapigia simu waingereza kuja kusaidia kuuzima huo uasi.

Kitu kimoja ambacho nadhani waandishi wengi wanakisahau na kutokitilia mkazo ni kwamba majaribio ya uasi yalifanyika kwenye nchi zote tatu (Tanganyika, Kenya na Uganda), ambazo zilikuwa ni koloni la taifa moja (Uingereza) na majeshi hayo yote (King African Rifles) yalitengenezwa na wao wenyewe. Kikubwa na kinachoshangaza ni kwamba haya mapinduzi yalifanyaka katika kipindi cha mwezi moja: And GUESS WHAT, madai ya wanajeshi kwenye nchi zote tatu yalikuwa yanafanana.
 
kambona sio mtu aliestaili ile treatment, hakua mtu aliekua akipigania madaraka wala hakua mtu wa uchu na madaraka alipigania TZ ile ile aliyokua anapigania nyerere bega kwa bega na mwalimu wote walikua na nia njema ila mwalimu was a fool to the core! kutofautiana tu mtazamo jamaa akamtesa sana mwenzake, mwalimu alikua kiongozi mbaya zaidi kuwahi kutokea Tanzania hii up to nw, he meant well but he persuased the wrong policies foolishly
 
1964 uasi ulitokea Afrika Mashariki yote, pamoja na Mapinduzi ya Zzanzibar, katika kipindi kifupi sana.

Kuna kitabu kimoja, nafikiri ni "Nyerere of Tanzania" cha William Edgett Smith, kinaelezea jinsi Mkapa alivyokuwa anampelekea maneno Nyerere kwamba Kambona anamsengenya, Nyerere akawa anayapuuza tu mwanzoni.Hata Nyerere mwenyewe hakuamini kwamba ugomvi wake na Kambona utakuwa mkubwa hivyo hapo mwanzoni. Ila inaonekana Kambona alianza kumponda Nyerere, na wapambe hawakupenda.

Kuhusu uasi, watu wanasema Kambona alipanga uasi, ila kama unavyosema, haiyumkiniki.Angepanga, alikuwa na nafasi nzuri ya kufanya mapinduzi ya kijeshi, kwani kuna wakati Nyerere alikimbia Ikulu.
 
Hivi kuna uhusiano kati ya huo uasi wa kijeshi wa mwaka 1964 na mapinduzi ya Zanzibar?

Ina maana Kambona alisaidia kutuliza uasi ila aliunga mkono mapinduzi ya Zanzibar yaliyopangwa na rafiki yake Hanga?
 
Siyo kweli kuwa filosofia ya ubebari ni asiyefanya kazi na asile. Kwenye ubebari unaweza kuwa mchapa kazi mzuri sana sana lakini ukashia kuishi maisha ya kifukara mno.

Hoja si kufanya kazi, hoja ni kufanya kazi zenye tija na ndio ubepari unavyotaka.

Sio mtu una amka tu na kuanza kulima lima bila kujua utauzia wapi na kwa nani, sio mtu unakurupuka tu kuomba kazi mahali ili hali hujui hata mahitaji yako yanakuitaji uwe na kipato kiasi gani.

Lazima ujue hivi ndio ufanikiwe la sivyo utabaki kulalamika unanyonywa kumbe ni ujinga binafsi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…