Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana


Alisema mwenyewe kuwa anataka nchi iwe na vyuo vikuu vichache vitakavyotoa majenerali. Iwe na vyuo vya kati kutoa makapteni. Na shule za msingi kutoa utitiri wa wapiganaji. Mfumo huu umepitwa na wakati kwani ata mtu asiye na ajira lakini akiwa na kisomo cha juu anamchango mkubwa kwa jamii kuliko mbumbumbu.

Hata Uingereza alipoiga mfumo huo mambo yamebadilika. Kwa mfano mwaka 1975, asilimia kumi tu ilikwenda University. Kwa miaka ya sasa ni zaidi ya asimilia 40.
 
kweli zamani ni zamani ina maana hakuwaza elimu kwa watu wote in general
 
Nimesoma hivi vitabu ni ukweli mtupu tungekuwa mbali sana
source (chanzo)
*"Bibi Titi and the Treason Trial of 1970," in The East African, Nairobi, Kenya, 10–16 November 1999
*Godfrey Mwakikagile, chapter 13, "Coup Attempts Against President Julius Nyerere.
*Wikipedia
 
share apa hvo vitabu kama unavyo
 
Papy sio kweli kwamba ndio jibu sahihi. Jibu sahihi ingekuwa wao kuwa na kama European Model.

Ambapo makazi (shelter), kazi (empoyment au unemployment), Afya kwa kila mtu (Universal Health Service of course you have to pay through insurance if you work). Lakini itakusaidia sana mbeleni.

Ukimaliza hayo (basic human neeeds) unakuja kwenye Elimu.

Elimu ya ukweli inakufumbua macho, kuiona Dunia tofauti, masoko, oppotunities, gap in the markets, your potential, your abilities to act and react to changing, fluid situation.

Sijui uelewa wako kuhusu neno ujamaa, (Socialism). Kwa kifupi ni undugu, kushirikiana kwa mambo makumbwa ambayo mtu mmoja mmoja hawezi kuyafanya.

Ujamaa is natural, in all human society. Mmasai akienda kuwinda anahitaji washikaji ili arudi salama. Vijiji vyote Tanzania ili ku-survive vinahitaji aina fulani ya social security (Ulinzi Shirikishi, kumsaidia mgonjwa, kupeana kazi, kuwasaidia maskini).

Sababu ziko wazi. Ukiwa tajiri pekee kijijini bila kuwasaidia wengine siku moja utavamiwa na walalahoi na hakuna atayekusaidia.

Ujamaa (Socialism) is old as human and animals. All for greater gòod of society.
 
sawa lakini baadae walimnyanyasa kambona mpaka akakimbia nchi kitu ambacho mwalimu hakupaswa kufanya ,alafu cha ajabu zaidi ni kwamba sijaona sehemu inasema oscar alikua na uchu wa madaraka au alitaka kumreplace mwalimu

Hindsight is 20/20. Lakini kuna ukweli kwamba jina lake, mchango wake, maoni yake, muhimu yawe recognised. He was giant of not only Tanzania politics but African politics.

It was sad to read how he live in London in Council Estate with jobs za kubangaiza. Kwanini asingeishi Afrika like Nigeria for example.

His talent, vision, ideas deserve a Place.
 
Kwa kifupi ulipangwa kwa Maslahi ya UK. Waje kuufuta baadaye. Kambla ya kuweka masharti fulani.
 
Mada nzuri sana. Hivi kwani tumetoka kwenye ujamaa?
 
Ubepari ukiendeshwa holels holela ni majanga tu.

Hata ujamaa usiposimamiwa vizuri ni kilio tu. Ndani ya ujamaa Mnaanzisha viwanda, mabenki halafu usimamizi hakuna. Mtegemee maumivu. Kama tulivyoishia kuviuza na mara ingine kwa hasara.

Kama vitu alivyoanzisha Nyerere vingepata usimamizi, tungekuwa tunaongea mengine saa hizi. Ilitakiwa vilindwe, ubunifu uwepo, ushindani uwepo, na nk.

Vitu vingi vilivyoanzishwa nahisi vilikufa kizembe zembe tu - hujuma za wafanyakazi/ viongozi, uzembe zembe, ukosefu wa teknolojia mpya,
 
nafkiri aliona hatokua salama ndani ya nchi yoyote ya afrika and the funny thing ni kwamba aliishi maisha ya ukata sana lakini huku nyumbanni nyerere & co. walisema kwamba jamaa alikimbia na mkwanja wa kutosha
 

What did you smoke? Ujamaa isn't natural and isn't that old. If it was, we could have seamlessly fitted in without the use of force.
 

Kwenye Ujamaa utasimamia nini? Majengo? Zilikuwepo banks, lakini watu walishindwa kuweka pesa kwa sababu ya kipato. Sasa utasimamia nini? Kulikuwepo na viwanda, lakini havikuwa na uzalishaki mzuri. Sasa ulitaka watu wasimamie kugawana kipande cha sabuni.
 
mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake". Ukweli mtupu viongozi ni lazima wawe na utaratibu wa kusikiliza! Lakini vilevile wananchi wengi wanapenda ushabiki sana angalieni sasa kuna watu wanashabikia kila kitu hata mabaya kwa nchi!
 
Fafanua zaidi mkuu.

Hakuna mtu aliyewahi kuishi kwenye Ujamaa. Hata Nyerere mwenyewe hakuwai. Wakati wa utawala wake misaada kutoka kwa mabepari ilikuwa kwenye asilimia 50. Ina maana hata mshahara wake ulitegemea mfumo wa kibepari. Na bila misaada hiyo asingeweza kujenga hospitali au mashule.
 

Viongozi wanataka umaarufu kwa kuendeleza umasikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…