Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Nimekuelewa, Shukrani sana, Mkuu Charles Mandela!

Hapo kwenye TIGRIS MNYAMA kufanya yake nilimaanisha labda huenda kamsaini BWANA MDOGO ufalmeni kwake.

Naam, Hapo kwenye mvua, kiangazi, na masika wamepewa mamlaka duniani na mbinguni, ....MATHAYO 16:18-19
 
Mkuu hapo kwenye mvua imekaaje sababu mwaka jana mvua zilikua hadimu sana au ilikua n adhabu?
MAMBO mengine yatabaki kuwa ni SIRI ya WATAWALA na sio vizuri kujadili kila kitu kwenye MITANDAO YA KIJAMII.
Lakin pia hi biblia wao wanasimamia vifungu vip?
Hawa WATU wamesoma darasani BIBLIA TAKATIFU na kuielewa, huwa wanaitwa WANATHEOLOJIA. Na wanatumia vitabu vyote vya AGANO LA KALE na AGANO JIPYA kuongoza NCHI.
Ngoja niishie hapo kwanza sababu maswal hayaishi
Maswali ni mengi sana, tena sana!! Na ukiendelea kuhoji ili kufahamu zaidi, huwa wanasema hivi - DUNIANI SOTE NI WAPITAJI au DUNIANI TUMEKUJA KUTEMBEA lakini SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 itabaki na CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ kitaendelea kuwepo.

CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA DUME na CHAMA KIKONGWE barani AFRIKA.

Wanavyosema CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA KIKONGWE barani AFRIKA huwa wanamaanisha kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA CHA KISIASA chenye umri mkubwa baada ya CHAMA CHA KISIASA cha LIBERIA 🇱🇷 kinachoitwa TRUE WHIG PARTY - TWP 🐘. Yaani kwa lugha nyingine tunaweza kusema hivi - CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA CHA KISIASA cha pili kwa umri baada ya CHAMA CHA TRUE WHIG PARTY - TWP 🐘.

Na wanavyosema kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA DUME huwa wanamaanisha kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ ni CHAMA CHA KISIASA chenye NGUVU KUBWA ya kuweza kusambaratisha hata FAMILIA, yaani ndugu na jamaa wakafarakana.

Familia ndio huwa hatua ya chini kabisa kwenye JAMII na huwa inahitajika uwezo, utashi na NGUVU YA DHIADA ya kuweza kuisambaratisha. Yaani WAINGEREZA 🇬🇧 huwa wanasema hivi - "FAMILY is the smallest unit within the society. It's just like a nucleus within the atom or molecule".

Kwahiyo kwenye TAIFA lolote lile huwa wanaanzia kwenye ngazi ya FAMILIA, MTAA, KATA, WILAYA, MKOA halafu TAIFA. Kwahiyo CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ kina uwezo, utashi na nguvu ya DHIADA ya kusambaratisha hata ngazi ya chini kabisa kwenye TAIFA, ambayo huwa ni FAMILIA.

Kwa kuyatambua hayo, ndio maana hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU huwa hawataki mchezo kabisa yanapokuja MASUALA yanayohusu FAMILIA zao.
 
Samahani, Na tena tafadhali sana, Mkuu Charles Mandela!

Nakusihi tena sana, Mkuu wangu, CHARLES MANDELA!
Ikiwa MANENO YALE hayakutiwa MHURI mpaka sasa, Basi nakusihi UTUFUNGULIE.

DEC 24, 2021. "Lakini wale WENYEVITI WA VYAMA VYA SIASA wengi wao ni MAMLUKI na WAHAMIAJI wa mkoa wa NYUMBU wakitokea mkoa wa KIBOKO na TEMBO". #931
 
Mwalimu hayupo pichani

3034331_2725964_msemaukweli255_20210328_105433_0.jpg

Rejea vizuri hiyo posti uliyoinakili hapo juu. Kwenye PICHA ya pamoja aliyopiga OSCAR SALATHIEL KAMBONA na MKEWE, HAYATI MWALIMU anaonekana amesimama pembeni yaani UPANDE WA KULIA wa BIBI HARUSI huku akiwa ameshika BEGA LA MTOTO aliyekuwa akisindikiza HARUSI.
 
Nimekuelewa, Shukrani sana, Mkuu Charles Mandela!
Ndio 🙏🏽
Hapo kwenye TIGRIS MNYAMA kufanya yake nilimaanisha labda huenda kamsaini BWANA MDOGO ufalmeni kwake.
Hapana! Yaani hao waliokuwa WASANII WA KUNDI LA WASAFI ni WATOTO ambao WAZAZI wao walihama MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA NA TABORA yaani ni kizazi cha MWASHITA yaani SIMBA 🦁.

Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema hivi - hao WASANII WA KUNDI LA WASAFI ni WATOTO ambao WAZAZI wao walikuwa ni miongoni mwa wale MWASHITA yaani SIMBA 🦁 waliohama kutoka MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA na TABORA na kwenda kuishi sehemu mbali mbali za TANZANIA 🇹🇿.

Na WASANII wote wa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wanatunzwa na kampuni za kibiashara ambazo zinamilikiwa na wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU.

Kwahiyo hawa WASANII wenye ASILI YA MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wataendelea kuwepo kwenye TASNIA YA MUZIKI kwa kipindi kirefu sana, labda VIWANGO vyao vishuke lakini sio kwa sababu za KIUCHUMI.

Kwa mfano tena, huyu ni MSANII mwingine maarufu sana nchini UGANDA 🇺🇬 anaitwa SHEEBAH KARUNGI. Wazazi wake ni miongoni mwa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 waliohamia nchini UGANDA 🇺🇬 wakitokea MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA na TABORA.



Kwahiyo huyu SHEEBAH KARUNGI ni miongoni mwa WASANII wanaotunzwa na kampuni ambazo zinamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU.
Naam, Hapo kwenye mvua, kiangazi, na masika wamepewa mamlaka duniani na mbinguni, ....MATHAYO 16:18-19
Ndio! Hao WATU ni HATARI sana.
 
Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee hapa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu Nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia baadae sana baada ya kusikia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya Kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya Nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona Kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake".
Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda Urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo Kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho Oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona.

Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio Kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere.

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa ambaye ni co-founder wa hii nchi kwangu mimi alichangia 50% ktk kutengeneza taifa hili sawa sawa na mwalimu, yaani ni kama vile "stive wozniak na stive jobs", steve jobs alitumia akili za stive wozniak na credit akajiapa yeye mwenyewe

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

UPDATE:
Watu wengi kwenye comments wanasema kwamba ujamaa ulituleta karibu, lakini ujamaa huo huo ndio uliotuletea umaskini, kwa hiyo logic yake ni kwamba mwalimu alichagua umaskini na umoja dhidi ya maendeleo ambayo hatuna uhakika kama yangetugawa, lakini kabla ya yote Kambona alimshauri kwamba kabla ya ku adopt ujamaa tuufanyie kwanza majaribio , tutengeneze vijiji vichache ambavyo vitaishi kijamaa ili tuone hii system itafanya kazi lakini mwalimu alikataa akaiingiza moja kwa moja bila kujua risks zake ni nini kitu ambacho kambona alishakiona


"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
refence:

====

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

Christopher Makwaia

WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.10.jpeg

1. Usuli
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe
KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"
Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School
KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School
KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpeg

6. Ualimu Alliance Sec. School
Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena
KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU
Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000
KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25282%2529.jpeg

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU
KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK
Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957
Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London
Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika
Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.12.jpeg

16. KAMBONA Arejea Bongo
KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje
Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE
KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964
Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966
Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967
Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond !!
Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.
Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA
Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK
Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani",1967
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.
Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968
Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:
"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968
Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA
NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969
Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini
Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:
1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!!.

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969
Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7 ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha).

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo. M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978
Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU( Mwasisi wa TANU).
OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo, wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani
Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua, anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo
KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967:
Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka:
"Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK
Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE
Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani,1992
Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!.

42. NYERERE Amjibu KAMBONA
NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA
Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA
KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997
KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007
Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:
Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:
ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!! - MICHUZI BLOG (issamichuzi.blogspot.com)

Oscar Kambona - Wikipedia
View attachment 1983785
Du! Kwa maelezo haya, nimeamini maneno ya Tundu Lissu kwamba Nyerere alikuwa na vinasaba fulani vya udikteta kwenye damu yake
 
Samahani, Na tena tafadhali sana, Mkuu Charles Mandela!

Nakusihi tena sana, Mkuu wangu, CHARLES MANDELA!
Ikiwa MANENO YALE hayakutiwa MHURI mpaka sasa, Basi nakusihi UTUFUNGULIE.

DEC 24, 2021. "Lakini wale WENYEVITI WA VYAMA VYA SIASA wengi wao ni MAMLUKI na WAHAMIAJI wa mkoa wa NYUMBU wakitokea mkoa wa KIBOKO na TEMBO". #931
Hakuna SHIDA yoyote kwenye MITANDAO YA KIJAMII kama mtumiaji au watumiaji wakitumia LUGHA YA STAHA. Ijapokuwa wakati mwingine inaweza kuleta SHIDA endapo baadhi ya mambo yakiwa hadharani. Kwahiyo kuna vitu vinatakiwa viwe na UKOMO hata kwenye kujadiliana.

Kule MKOA WA KILIMANJARO kuna watu wengi sana walihamia wakitokea MIKOA MINGINE.

Na nikupe SIRI nyingine ambayo huwa haisemwi hadharani ni kuwa - "Wale wenyeji wa asili wa MKOA WA KILIMANJARO huwa hawafiki hata laki tisa [ 900,000,000 ] na idadi iliyoongezeka baada ya hapo ni wageni".

Yaani kule kwenye MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO kwa kiasi kikubwa shughuli zote zimeshikiliwa na SERIKALI. Hii ilifanyika na inaendelea kufanyika kimkakati.

Hata hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na wao walipeleka WATU wao na waka akisi majina na tamaduni za huko. Ndio maana kuna WATU wengine wanaitwa wakina MREMA lakini ni MWASHITA yaani SIMBA 🦁. Vile vile kuna WATU wengine wanaitwa wakina LEMA lakini ni MWASHITA yaani SIMBA 🦁. Pia kuna WATU wengine wanaitwa wakina NJAU lakini ni MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na wana mawasiliano na MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU.

Na WATU wengine huwa wanafunga NDOA!. Sasa kwa MTU asiyeelewa kinachoendelea anaweza akadhani ni MSUKUMA na MCHAGGA ndio wanafunga NDOA, kumbe wote ni WASUKUMA 😂😂😂

Kwahiyo, haya mambo ndio huwa yanafanyika hivyo na hiyo ndio SIASA YA TANZANIA 🇹🇿 ambayo huwa inafanywa na CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️!!! Wengine huwa wanapoteza muda tu..

Kwa mfano, kuna KIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM [ UDSM ] aliwahi kuwa RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI na alikuwa anaitwa MREMA. Lakini ni MWASHITA yaani SIMBA 🦁 ambaye wazazi wake walihamia KILIMANJARO wakitokea MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA na TABORA.

Yule MREMA sasa hivi ana nafasi kubwa sana kwenye moja ya CHAMA CHA KISIASA lakini ni MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na MOYO wake upo CHAMA CHA WANANCHI - CUF ☀️. Kwahiyo wanaofahamu haya ni wachache na mpaka uambiwe ndio utaelewa.

Masuala mengine ni SIRI YA WATAWALA na sio vizuri kujadili kila kitu kwenye MITANDAO YA KIJAMII. Hata hapa tunajadili masuala ya KIJAMII kwa TAHADHARI kubwa sana, maana hata mimi mwenyewe naona kama tumepitiliza.
 
Huyo alikuwa mnafiki ndo maana aliikimbia nchi.
OSCAR SALATHIEL KAMBONA hakuwa MTU MNAFIKI bali alikuwa ni MTU MKWELI, lakini wakati mwingine kama unataka kupata MAFANIKIO inabidi ujifanye MJINGA, ndio utafanikiwa.

Sasa angalia hapa chini MSIMAMO WA MAKUNDI YA MICHUANO YA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA KWA NGAZI YA SHIRIKISHO.

7090372dd2dd4df368283ee8ddee4135.png


cc89a86b787ae4df4c09d76d259ebb1b.png


ae354c95f2eb30da81953f333b2445af.png


cb6fe57cf7f9348b8a954395ddb452d0.png

Kwenye KUNDI LA GRUPU D kuna timu ya mpira wa miguu inayoitwa ASEC MIMOSAS. Hii timu inatoka IVORY COAST 🇮🇪 na inamilikiwa na HAYATI MWALIMU na ilishawahi kutwaa UBINGWA WA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA, mwaka 1998.

Na hii timu ndio iliyowahi kutoa wachezaji mashuhuri sana BARANI AFRIKA na DUNIANI kwa ujumla. Wachezaji hao ni kama YAYA TOURE, KOLO TOURE na SOLOMON KALOU.

Kwahiyo, hii timu ya ASEC MIMOSAS ni timu kubwa sana na msimu huu itakuja TANZANIA 🇹🇿 kucheza mechi na SIMBA SC kwenye hatua za makundi.

Sasa hapa ndio utaona ya kwamba - OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa SAHIHI kwa madai yake dhidi ya HAYATI MWALIMU, lakini hakuwa na USHAHIDI wa kutosha, ndio maana alionekana ni MTU MUONGO aliyetoa SHUTUMA ZA UONGO dhidi ya HAYATI MWALIMU kwa sababu ya KIU YA MADARAKA.
 
b20787e0bceef741cfe79daea52f3120.png

Hii kampuni ya BEKO ni kampuni kubwa ULAYA 🇪🇺 na inafanya vizuri sana kwenye upande wa MASOKO. Na sasa hivi BIDHAA zao zimeshaanza kupatikana hadi TANZANIA 🇹🇿.

Hii kampuni huwa inatengeneza VIFAA VYA KUTUMIA MAJUMBANI yaani WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita ni DOMESTIC PRODUCTS kama FRIJI, BLENDA ZA KUTENGENEZEA JUISI, OVENI, PASI ZA KUNYOOSHEA NGUO, SABUNI ZA KUFULIA na mambo mengine mbali mbali.

e8d74f4d42450a159ff581c49f6a6bec.png

Yaani hii kampuni ya BEKO ndio inaleta USHINDANI kwa kampuni ya KENWOOD, vile vile hii kampuni ya BEKO ndio wadhamini wakuu wa timu ya mpira wa miguu ya FC BARCELONA inayoshiriki LIGI KUU nchini UHISPANIA 🇪🇸 pamoja na timu ya mpira wa kikapu ya FENERBAHÇE S.K. inayoshiriki LIGI KUU nchini UTURUKI 🇹🇷.

e8f8c2a7a5e6c0a1eed396ceb93d000a.png

Sasa hii kampuni ya BEKO wamiliki wake wanatoka TANZANIA 🇹🇿 na ni WATANZANIA WEUSI ambao ni [...]. Aah!! Sasa mambo mengine inabidi yawe na UKOMO hata kwenye MITANDAO YA KIJAMII.

Lakini hao wanaomiliki kampuni ya BEKO ni WATANZANIA 🇹🇿 ambao UKWASI wao umetoka hapa hapa TANZANIA 🇹🇿 na chini ya UTAWALA WA CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️.

Kwahiyo hii inatuonesha ya kwamba - kwenye TAIFA LA TANZANIA 🇹🇿 ili ufanikiwe kwenye SEKTA yoyote ile, iwe ni KIUCHUMI au hata KISIASA au hata kwenye MAISHA YA KILA SIKU ni lazima ujifanye MJINGA MJINGA au FALA kwa wakati fulani. Ndio utafanikiwa 🙏🏽🇹🇿🙏🏽

Sasa hii ni AKILI YA KAWAIDA ambayo baadhi ya WATU wengi huwa hawana, akiwemo OSCAR SALATHIEL KAMBONA mwenyewe na hao WASUKUMA waliopo ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️.
 
Mkuu, CHARLES MANDELA!

Nimekubali yaishe, Mkuu SURENDRENATH nimemvulia KOFIA na SALUTI MILIONI nimempigia.

Si kwa CVs zile, aisee!
=LONDON SCHOOL OF ECONOMICS.
=HAVARD SCHOOL OF LAW.
=KING'S COLLEGE LONDON [LL.B & LL.M].
=ATTORNEY GENERAL.
=ASSISTANT ATTORNEY GENERAL.
=MINISTER OF JUSTICE.
=MINISTER OF FOREIGN AFFAIRS.
=COMMON WEALTH SECRETARY FOR 15 YEARS.
=KNIGHT GRAND CROSS AT S.T MICHAEL & S.T GEORGE.
=VIP (THE SAME AS MWASHITA THERE AT BUKINGHAM PALACE)

Kwa CV KALI SANA kama hizo, Hata jina SHIDA ni zaidi ya SHIDA yaani.

Mkuu wangu anatisha kama nini, Anatisha sana mithili ya TIGRIS na LEO.
 
Huyu ni mwamba ambaye historia yake inafichwa
OSCAR SALATHIEL KAMBONA - mwanafunzi, rafiki wa karibu na baadae ADUI mkubwa wa HAYATI MWALIMU.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa ni MWAMBA wa chama cha TANU na SERIKALI YA TANZANIA [emoji1241] kwa ujumla.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa ni MWANASIASA namba mbili kwa ushawishi baada ya HAYATI MWALIMU.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alizaliwa mkoa wa RUVUMA mwaka 1928, baba yake alikuwa ni MCHUNGAJI wa KANISA LA ANGLIKANI na mmoja kati ya wachungaji wa kwanza wa KIAFRIKA nchini TANZANIA [emoji1241].

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alianza kwa kufundishwa chini ya MTI na shule ya awali alisoma shule ya MTAKATIFU BARNABASI huko kwao na baadae aliendelea na masomo ya SEKONDARI katika shule ya ALLIANCE iliyopo DODOMA.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa ni mwanafunzi mwenye uwezo mkubwa darasani, kwa vile baba yake alikuwa hana uwezo wa kulipa ADA YA SHULE, OSCAR alitumia mbinu ya kujifunza na kuweza kusali kwa LUGHA YA KIINGEREZA [emoji636] na kumshawishi ASKOFU - MUINGEREZA amlipie ADA YA SHULE.

Baadae alimaliza SHULE YA SEKONDARI YA ALLIANCE na kufaulu kwenda SEKONDARI YA JUU katika SHULE YA WAVULANA YA TABORA, huko sasa ndipo alipokutana na HAYATI MWALIMU.

Wakati huo HAYATI MWALIMU alikuwa tayari ni MWALIMU na alikuwa anafundisha SHULE YA KIKATOLIKI YA MTAKATIFU MARIA iliyopo TABORA MJINI.

Basi baada ya kumaliza SHULE YA SEKONDARI YA JUU katika SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA YA TABORA, alipata ufadhili wa kujiunga na CHUO KIKUU CHA MAKERERE kilichopo nchini UGANDA [emoji1254].

Baada ya masomo ya CHUO KIKUU, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alifanikiwa kuchukua SHAHADA YA UALIMU na alirudi DODOMA kufundisha SHULE YA SEKONDARI YA ALLIANCE, shule aliyosoma.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alivyokuwa SHULE YA SEKONDARI YA ALLIANCE alipanda vyeo mpaka kufikia kuwa MWALIMU MKUU kwa kipindi kifupi tu.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuja kukutana na HAYATI MWALIMU kwa mara ya pili mwaka 1954, kwenye mkutano wa TAIFA WA WAALIMU uliofanyika DAR ES SALAAM baadae mwaka 1955, akajiunga na TANU iliyokuwa imezaliwa mwaka 1954.

Kipindi hicho TANU ilikuwa haina PESA ZA KUTOSHA, kwahiyo OSCAR SALATHIEL KAMBONA alifanya kazi kwa kujitolea na kwa bidii ya hali ya juu.

Alizunguka nchi nzima kuonana na machifu na wanavijiji na kwa kipindi cha mwaka mmoja alifanikiwa kuongeza wanachama wengi sana ndani ya CHAMA CHA TANU.

Mwaka 1957, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alipata UFADHILI WA MASOMO na kwenda kusoma UINGEREZA [emoji636], na wakati mmoja HAYATI MWALIMU akiwa UINGEREZA [emoji636] kwenye harakati za UHURU alilala chumba cha OSCAR KAMBONA alipokuwa chuoni.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alifunga NDOA na MISS TANGANYIKA - FLORA MORIYO mwaka 1960 na alisimamiwa na HAYATI MWALIMU mwenyewe.


Akiwa KATIBU MKUU WA TANU kwa kushirikiana na HAYATI MWALIMU mwenyewe, waliongoza TANGANYIKA kupata UHURU, mwaka 1961.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa ni KIONGOZI MCHESHI na alikuwa anakubalika sana na WAZEE WA DAR ES SALAAM na watu wengi walidhani baada ya HAYATI MWALIMU kumaliza wakati wake basi OSCAR SALATHIEL KAMBONA atakuwa ni RAIS ajaye.

Umaarufu wake uliongezeka mwaka 1964, wakati JESHI LA TANZANIA [emoji1241] lilipotaka kufanya MAPINDUZI, OSCAR SALATHIEL KAMBONA kama WAZIRI WA ULINZI alienda JESHINI na kuwatuliza ASKARI wa wakati huo. Huku RAIS HAYATI MWALIMU na MAKAMU wake, RASHID MFAUME KAWAWA walichukuliwa na kupelekwa mafichoni na WATU WA USALAMA.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alienda JESHINI akaongea na ASKARI, akasikiliza matakwa yao na kufanya usuluhishi. Madai yalikuwa ni kupandishwa mishahara na nafasi za JESHI zilizokuwa zinashikiliwa na WAZUNGU wapewe WAZAWA yaani WATANZANIA WEUSI.

Ijapokuwa kulikuwa na uvumi ya kwamba baadhi ya WAKUBWA WA SERIKALI, VYAMA VYA WAFANYAKAZI walipanga njama na JESHI ili wampindue HAYATI MWALIMU.

OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa ni maarufu sana JESHINI, walimuamini na wakatulia. Cha kushangaza ni kwamba - MAJESHI YA KENYA [emoji1139] NA UGANDA [emoji1254] pia na wao walifanya migomo kama hiyo, siku mbili baadae na madai yalikuwa ni yale yale.

Ndani ya BARAZA LA MAWAZIRI - OSCAR SALATHIEL KAMBONA ndio alikuwa ni mtu anayeweza kubishana na HAYATI MWALIMU na kupingana kwa hoja! Wengine waliwahi kusema kuwa OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa anaona analingana na HAYATI MWALIMU kwa hadhi.

Na mtu mwingine aliyeweza kufanya hivyo alikuwa ni ABDALLAH FUNDIKIRA aliyekuwa WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA kwa wakati huo, tena ni kwa sababu alisoma na HAYATI MWALIMU katika CHUO KIKUU CHA MAKERERE nchini UGANDA [emoji1254].

ABDALLAH FUNDIKIRA alijiuzuru nafasi yake ya UWAZIRI baada ya kupishana kauli na HAYATI MWALIMU. [ Itaendelea.. ]
 
Mkuu, CHARLES MANDELA!

Nimekubali yaishe, Mkuu SURENDRENATH nimemvulia KOFIA na SALUTI MILIONI nimempigia.

Si kwa CVs zile, aisee!
=LONDON SCHOOL OF ECONOMICS.
=HAVARD SCHOOL OF LAW.
=KING'S COLLEGE LONDON [LL.B & LL.M].
=ATTORNEY GENERAL.
=ASSISTANT ATTORNEY GENERAL.
=MINISTER OF JUSTICE.
=MINISTER OF FOREIGN AFFAIRS.
=COMMON WEALTH SECRETARY FOR 15 YEARS.
=KNIGHT GRAND CROSS AT S.T MICHAEL & S.T GEORGE.
=VIP (THE SAME AS MWASHITA THERE AT BUKINGHAM PALACE)

Kwa CV KALI SANA kama hizo, Hata jina SHIDA ni zaidi ya SHIDA yaani.

Mkuu wangu anatisha kama nini, Anatisha sana mithili ya TIGRIS na LEO.
Hawa WATAWALA huwa wanazungukwa na WATU wasomi sana, hata HAYATI MWALIMU mwenyewe alikuwa na WATU WASOMI waliokuwa wakimsaidia kuongoza NCHI.
 
IMG_20211228_004339.jpg

Mfano mwingine mzuri ni kuhusu ABEID AMAAN KARUME na familia yake yote kwa ujumla. Huyu ABEID AMAAN KARUME ndiye aliyekuwa RAIS WA KWANZA WA SERIKALI YA ZANZIBAR na MWENYEKITI WA CHAMA CHA KISIASA kilichokuwa kinaitwa AFRO SHIRAZI.

ABEID AMAAN KARUME ndiye aliyekuwa RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR na MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA TANZANIA 🇹🇿, baada ya MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

ABEID AMAAN KARUME alizaliwa Tarehe 4, Mwezi wa nane [ 8 ], Mwaka 1905 maeneo fulani yanaitwa MWERA katika MJI WA ZANZIBAR na aliongoza SERIKALI YA ZANZIBAR kuanzia mwaka 1964 mpaka pale UMAUTI ulivyomkuta Mwaka 1972, Mwezi wa nne [ 4 ] na Tarehe 7.

ABEID AMAAN KARUME aliuawa kwa shambulio la RISASI akiwa anacheza bao pale MAKAO MAKUU YA OFISI YA CHAMA CHA AFRO SHIRAZI.

Kifo chake bado ni FUMBO mpaka leo, kwa sababu kuna taarifa nyingine zinasema kuwa USULTANI ulihusika kama ni sehemu ya kulipiza kisasi baada ya MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

Taarifa nyingine zinachagizwa na ASILI yake ya kuzaliwa, kuna taarifa nyingine zinasema ya kwamba - ABEID AMAAN KARUME alizaliwa NYASALAND ambayo ndio NCHI YA MALAWI 🇲🇼 kwa sasa na alifanya kuhamia ZANZIBAR. Kwahiyo kuna MAMBO YA NDANI kabisa yaliyopelekea kifo chake.

ABEID AMAAN KARUME alifariki dunia mwaka 1972 na alizikwa katika MBUGA YA WANYAMA YA SELOUS, maeneo fulani yanaitwa MKANGIRA. Lakini kuna taarifa nyingine zinasema kuwa ABEID AMAAN KARUME alizikwa ZANZIBAR, yaani bado ni FUMBO na hukana taarifa ya UHAKIKA kwenye JAMII inayohusu ABEID AMAAN KARUME.

Familia ya ABEID AMAAN KARUME ilipitia misukosuko mingi sana baada ya kuondokewa na BABA, ambaye ndiye aliyekuwa RAIS WA SERIKALI YA ZANZIBAR. Lakini walisimama IMARA kama familia iliyoongozwa na MKE WA HAYATI, BIBI FATMA KARUME.

Sasa hapa ndio utaona UTASHI WA KISIASA KWA WATU WA PWANI, familia ya HAYATI KARUME ilitulia kama MAJI KWENYE MTUNGI na ilikuwa ni tofauti kabisa na matarajio ya WAZANZIBARI waliokuwa wengi.

MKE WA HAYATI KARUME, BIBI FATMA KARUME aliweza kulea WATOTO wake wote wawili ambao wanajulikana kwa majina ya AMAAN na ALLY.

Huyo AMAAN ndiye aliyekuja kuwa RAIS WA SITA [ 6 ] WA SERIKALI YA ZANZIBAR ambaye alikuwa anaitwa kwa majina yake yote, AMAAN ABEID KARUME.

AMAAN ABEID KARUME alifanikiwa kuwa RAIS WA SERIKALI YA ZANZIBAR kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 na alifanikiwa kushinda UCHAGUZI MKUU WA ZANZIBAR kwa KURA ZA UNYONGE WA KISIASA yaani WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita ni POLITICAL PATRONAGE VOTES.

Ijapokuwa kuna taarifa nyingine zinasema kuwa - AMAAN ABEID KARUME alishinda kwa KURA ZA UMAARUFU WA KISIASA yaani WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita ni POPULAR MAJORITY VOTES lakini kwa taarifa za UKWELI NA UHAKIKA ni kwamba - AMAAN ABEID KARUME alishinda KITI CHA URAISI WA ZANZIBAR kama ZAWADI au SHUKRANI ya UVUMILIVU WA KISIASA baada ya kuondokewa na BABA yake [ ABEID AMAAN KARUME ] kwa shambulio la RISASI.

Kwahiyo familia ya HAYATI KARUME iliinuka tena kwenye MEDANI ZA KISIASA baada ya miaka zaidi ya ishirini na tano [ 25 ], yaani tangu mwaka 1972 alipouawa ABEID AMAAN KARUME mpaka mwaka 2000 alipoapishwa MTOTO wake wa kiume, AMAAN ABEID KARUME kuwa RAIS WA SITA [ 6 ] WA SERIKALI YA ZANZIBAR. Huo ndio UVUMILIVU WA KISIASA KWA WATU WA PWANI!! Narudia tena, huo ndio UVUMILIVU WA KISIASA KWA WATU WA PWANI!!

Huu UVUMILIVU WA KISIASA KWA WATU WA PWANI ndio wanao wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU yaani MWASHITA au kwa jina lingine wanaitwa SIMBA 🦁.

Hiyo FAMILIA YA HAYATI KARUME wasingelikuwa na UVUMILIVU WA KISIASA, pengine leo wangelikuwa na hali mbaya zaidi ya KIUCHUMI na KISIASA kuliko hata familia ya ADAM SAPI MKWAWA na familia ya OSCAR SALATHIEL KAMBONA na wengine wengine wa kufanana na hao.

Lakini kutokana na UVUMILIVU WA KISIASA walionao hao WATU WA PWANI, hiyo FAMILIA YA HAYATI KARUME ilidondoka mwaka 1972 na baadhi ya WATU walidhani ndio ingelikuwa ni mwisho wao! Lakini baadae kwenye miaka 2000, FAMILIA YA HAYATI KARUME iliinuka tena na kutoa RAIS WA SITA [ 6 ] WA SERIKALI YA ZANZIBAR.

Na sasa hivi FAMILIA YA HAYATI KARUME wamejijenga sana - iwe ni KIUCHUMI na hata KISIASA. Hii FAMILIA YA HAYATI KARUME ina UKWASI wa kutosha, sema haiwezi kulingana na FAMILIA YA HAYATI MWALIMU.

Lakini ukija kwa upande wa TANZANIA 🇹🇿 nzima, miongoni mwa familia kumi [ 10 ] zenye UWEZO WA KIUCHUMI na KISIASA, hauwezi kuacha kuitaja FAMILIA YA HAYATI KARUME 🙏🏽🇹🇿🙏🏽.

Sasa hii ndio SIASA! Narudia tena hii ndio SIASA! Na kwenye SIASA kuna waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa. Lakini msingi mzuri unaanzia kwenye FAMILIA. FAMILIA ndio nyenzo katika mafanikio ya kujenga TAIFA.

Na MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU walijijenga, wamejijenga na wanaendelea kujijenga kupitia MTINDO huo wa UVUMILIVU WA KISIASA.

e4c832dd72ef187bfa021f47b1c86d96~2.jpg

Hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU ndio miongoni mwa WATANZANIA WEUSI waliowekeza kwenye NCHI ZOTE ZA AFRIKA YA MASHARIKI.

Haya MAMBO ndio WATU wengine wanapaswa kuiga, kwa sababu sio vibaya na wala sio dhambi kuiga jambo zuri kutoka kwa mwenzio.
 
-5979825542964292863_121.jpg

Hii ni NEWS FEED TELEGRAM ya TBC1 na kwa siku ya leo wanauliza swali kama hili - Leo ni maazimisho ya MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR. Nini kinakuvutia sana visiwani ZANZIBAR?

-5979981948493344002_121.jpg

Sasa kinachovutia sana VISIWANI ZANZIBAR ni aina ya UVUMILIVU WA KISIASA unaopatikana kwenye VISIWA VYA UNGUJA na PEMBA.

-5980082596756958542_121.jpg

Kwenye PICHA hapo juu anaonekana ni RAIS WA SASA WA SERIKALI YA ZANZIBAR, Dkt HUSSEIN ALLY MWINYI ambaye ni MTOTO wa RAIS MSTAAFU WA SERIKALI YA TANZANIA, Ndugu ALLY HASSAN MWINYI.

Huyu Dkt HUSSEIN ALLY MWINYI ambaye ndiye RAIS WA SERIKALI YA ZANZIBAR alishinda UCHAGUZI MKUU kwa njia ya SANDUKU LA KURA ambazo zilikuwa ni KURA ZA UMAARUFU WA KISIASA yaani WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita ni POPULAR MAJORITY VOTES na sio KURA ZA MARUHANI kama WATU wengi wanavyodhani.

Hali hii ilikuwa ni tofauti kabisa na UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2000 ambapo AMAAN ABEID KARUME alishinda KITI CHA URAISI kwa KURA ZA UNYONGE WA KISIASA yaani WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita ni POLITICAL PATRONAGE VOTES. Lakini mwisho wa siku, wote wamefanikiwa kuwa MARAIS WA SERIKALI YA ZANZIBAR kwa vipindi tofauti.

Sasa hii inatoa taswira gani kwa upande wa SIASA ZA ZANZIBAR? Hii inatoa taswira ya UVUMILIVU WA KISIASA ambao unatokana na UTASHI WA KISIASA walionao WATU WA PWANI.

Yaani kwa lugha nyingine tunaweza kusema hivi - hawa WATU WA PWANI wanakitumia CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ kukwea MNAZI, kitu ambacho kimekuwa ni kigumu sana kufanikiwa kwa JAMII nyingine.

Na hii ndio SIASA! Narudia tena hii ndio SIASA ambayo inafanyika ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️ na TANZANIA nzima kwa ujumla wake.
 
IMG_20220116_100255_923.jpg

Hii ni NEWS FEED TELEGRAM ya JAMIIFORUMS, niliipata tangu jana. Lakini leo ndio nimepata muda mzuri wa kuweza kuangalia na kusoma vizuri.

Hiyo PICHA hapo juu inaonesha SHULE KUMI [ 10 ] zilizofanya vizuri katika MTIHANI WA KIDATO CHA NNE, mwaka 2021 na SHULE iliyoongoza ni KEMEBOS kutoka MKOA WA KAGERA.

Hii SHULE YA KEMEBOS kutoka MKOA WA KAGERA ni SHULE ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU hawapo kwenye MICHEZO tu, bali wapo hadi kwenye SEKTA YA ELIMU na SHULE zao zinafanya vizuri KITAIFA.

IMG_20220116_100358_899.jpg

Jaribu tena kuangalia hiyo PICHA hapo juu! Hiyo PICHA inaonesha ORODHA YA WANAFUNZI BORA waliofanya vizuri katika MTIHANI WA KIDATO CHA NNE na SHULE inayoonekana kutoa WANAFUNZI wengi kwenye ORODHA YA WANAFUNZI BORA ni SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MTAKATIFU FRANSISI yaani ST. FRANCIS GIRLS SECONDARY.

Sasa ni nini kipo nyuma ya MAFANIKIO ya hii SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MTAKATIFU FRANSISI yaani ST. FRANCIS GIRLS SECONDARY?

Na nani anamiliki hii SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MTAKATIFU FRANSISI yaani ST. FRANCIS GIRLS SECONDARY?

Haya MASWALI ndio SIASA yenyewe na MAMBO mengine sio mazuri kuyajadili kwenye MITANDAO YA KIJAMII kwa sababu ya UNYETI wake. Lakini JAMII YA SERENGETI yaani CHUI wanafanya SIASA ZA KIWANGO cha juu sana.
 
Back
Top Bottom