Wakudadavuwa - kwa muendelezo wa posti namba 1172! Kitu kingine ambacho walikuwa hawakifahamu hawa waliokuwa viongozi wa MATAIFA MATATU [ 3 ] YA RWANDA, BURUNDI na KONGO ni uwepo wa kundi lililojiita UGANDA LINE.
UGANDA LINE ni kundi lililojumuisha WATANZANIA waliosoma ELIMU YA MSINGI, ELIMU YA SEKONDARI na ELIMU YA CHUO KIKUU nchini UGANDA. Na ni watu ambao walikuwa wanaamini kuwa wao ni WASOMI kuliko WATANZANIA wengine.
Hili kundi la UGANDA LINE lilikuwa linajumuisha HAYATI MWALIMU, MISTER CLEAN na WAFANYAKAZI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU ambao walikuwa wamesoma ELIMU YA SEKONDARI na ELIMU YA CHUO KIKUU nchini UGANDA.
Kwahiyo yale mambo yote hawa viongozi wa MATAIFA MATATU [3] ya RWANDA, BURUNDI na KONGO waliyokuwa wakiyapanga na kuwaambia wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU yalikuwa yanamfikia HAYATI MWALIMU moja kwa moja na walikuwa wanatumia TAASISI ZA KIDINI kukamilisha adhma yao.
Vile vile kipindi cha VITA BARIDI hizi taasisi za kidini zilionesha rangi zao halisi. Yaani hizi taasisi za kidini zipo kwa ajili ya masilahi ya MATAIFA yao, kule zilipoanzishwa. Kwa mfano, KANISA LA ROMANI KATOLIKI linasimamia MASILAHI ya VATIKANI, ITALIA na MATAIFA yote yanayotumia LUGHA YA KIFARANSA! KANISA LA ANGLIKANI linasimamia MASILAHI ya UINGEREZA na MATAIFA yote ya JUMUIYA YA MADOLA! KANISA LA LUTHERANI linasimamia MASILAHI ya UJERUMANI! Kwahiyo, haya MATAIFA YA KIAFRIKA yalikuwa yanatumika kwenye kukusanya SADAKA, ZAKA na MICHANGO mbalimbali ili kufanikisha shughuli za kidini. Yaani wao ni HELA kwanza, halafu mambo mengine ni baadae. Hata hizi HUDUMA ZA KIJAMII ambazo huwa wanatoa, huwa wanatoa kwa GHARAMA na sio BURE!!
Sasa HAYATI MWALIMU na hawa waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU walikutana TABORA, mwaka 1991/92 na kuweka maazimio yaliyokuwa yanaitwa "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS".
"MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" yalikuwa ni MAAZIMIO YA SIRI kutokana na UNYETI wake. Lakini yalikuwa yanalenga ile DHANA YA KULINDANA yaani NILINDE NIKULINDE, SOTE TULINDANE.
Kwenye "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" walikuwa wamegusia masuala manne kama sio matano, kwa ujumla wake. Masuala hayo ni SIASA, UCHUMI, DINI na ULINZI.
Sasa kipindi MAAZIMIO YA TABORA yanafanyika, upande mwingine walikuwa wanatafuta kiini na suluhisho kwa haya MATAIFA MATATU [ 3 ]YA RWANDA, BURUNDI na KONGO.
AZIMIO LA KWANZA kwenye "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" lilikuwa ni suala la SIASA. Suala la SIASA ndio lililokuwa ni chimbuko la kuanzisha MFUMO WA VYAMA VINGI VYA KISIASA.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA TABORA yaani WETCU walipata fursa na kuanzisha CHAMA CHA KISIASA kilichoitwa [...], 1992. Kwa ustadi mkubwa na propaganda ya hali ya juu walikipeleka hicho CHAMA CHA KISIASA katika MKOA WA KILIMANJARO, iwe ni sehemu ambapo CHAMA kilizaliwa na kusajiliwa katika MKOA WA DAR ES SALAAM kwenye ofisi ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA SHINYANGA yaani SHIRECU na wao walipata fursa na kuanzisha CHAMA CHA KISIASA kilichoitwa [...], 1993. Kwa ustadi mkubwa na propaganda ya hali ya juu walikipeleka hicho CHAMA CHA KISIASA katika MKOA WA TABORA, iwe ni sehemu ambapo CHAMA kilizaliwa na kusajiliwa katika MKOA WA DAR ES SALAAM kwenye ofisi ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA. Hiki CHAMA CHA KISIASA kilimea sana VISIWANI ZANZIBAR na sehemu mbalimbali za MWAMBAO WA BAHARI YA HINDI.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA MWANZA yaani NCU waliona hakuna haja ya kuanzisha CHAMA CHA KISIASA ilhali VYAMA VYA KISIASA vingine vimeshapatikana. Kwa hiyo wao walisimamia masilahi yao kwanza na waliunga mkono CHAMA CHA KISIASA chenye ITIKADI NA SERA nzuri.
AZIMIO LA PILI kwenye "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" lilikuwa ni suala la UCHUMI. Hawa waliokuwa wajumbe na wahusika wa KIKAO CHA MAAZIMIO YA TABORA yaani TABORA DECLARATIONS MEETING walikuwa ni WATU wenye UKWASI kwa kipindi hicho na ndio waliofanyika kuwa wamiliki wa UCHUMI kwenye SEKTA zote zinazopatikana TANZANIA.
AZIMIO LA TATU kwenye "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" lilikuwa ni suala la DINI. Wale waliokuwa wajumbe wa KIKAO CHA MAADHIMIO YA TABORA yaani TABORA DECLARATIONS MEETING walikuja na maadhimio ya kuanzisha madhehebu yao ya kidini na kuachana kabisa na madhehebu ya kigeni. Hicho kipindi ndio kilikuwa ni chimbuko la MAKANISA YA KIEVANJILISTI au kwa lugha nyingine wanaita ni MAKANISA YA KIPENTEKOSTE.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA TABORA yaani WETCU walifanikiwa kuanzisha taasisi yao ya kidini ambayo ni KANISA LA [...] na hilo KANISA limeenea TANZANIA nzima.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA SHINYANGA yaani SHIRECU walifanikiwa kuanzisha taasisi yao ya kidini ambayo ni KANISA LA [...] na hilo KANISA limeenea TANZANIA nzima.
Wale waliokuwa wafanyakazi wa CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MKOA WA MWANZA yaani NCU na wao walifanikiwa kuanzisha taasisi yao ya kidini ambayo ni KANISA LA [...] na hilo KANISA limeenea TANZANIA nzima.
Na baada ya kusuasua kwa kipindi kirefu sana tangu mwaka 1968, ile iliyokuwa taasisi ya kiislamu ya TANZANIA yaani BAKWATA ilifanyika kuwa ni taasisi ya kidini iliyo chini ya SERIKALI YA TANZANIA ambapo kwa undani wake unawakuta wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU.
Yaani kwa lugha nyingine tunaweza kusema hivi - shughuli zote za kiuchumi za BARAZA LA KIISLAMU LA TANZANIA yaani BAKWATA zinasimamiwa na wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU kupitia kampuni zao za kibiashara.
Baada ya hapo - AZIMIO LA NNE lilikuwa ni kuimarisha ULINZI wa ndani na nje ya NCHI dhidi ya maadaui. Kwa kipindi kile HAYATI MWALIMU alitoa fursa kwa wenyeji wa hii MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA na TABORA ya kujiunga na MAJESHI YA ULINZI NA KUJENGA TAIFA ikiwemo JESHI LA POLISI, JESHI LA WANANCHI [ JWTZ ], JESHI LA MAGEREZA, JESHI LA ZIMAMOTO na JESHI LA UHAMIAJI.
Yaani hicho kipindi kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa upande wa TANZANIA, kwa sababu kuna baadhi ya WATU walihama makabila na kubadilisha majina ya ukoo, wengine walibadilisha dini na hata uraia wa nchi kwa nia ya kuimarisha ULINZI NA USALAMA.
Baada ya kuimarisha ULINZI NA USALAMA WA NDANI YA NCHI - HAYATI MWALIMU alihamia kwenye zile NCHI TATU [ 3 ] ZA RWANDA, BURUNDI NA KONGO na kilichofuata ni historia!!
Kwa upande wa RWANDA walifanikiwa kuitoa SERIKALI iliyoongozwa na JUVÉNAL HABYARIMANA na kumuweka PAUL INGABIRE KAGAME kama ni KIONGOZI KIVULI. Sema kwa sintofahamu uliyokuwa imetanda kipindi kile, WATUSI ambao ndio wachache kwa TAIFA LA RWANDA walionekana kuwa sehemu salama zaidi kuliko watu wengine.
PAUL INGABIRE KAGAME ni NEMBO YA URAISI yaani IDEAL PERSONEL PRESIDENT na aliandaliwa kwenda kuitawala RWANDA, lakini wanaoongoza SERIKALI YA RWANDA ni JESHI LA RWANDA yaani RWANDA DEFENSE FORCE [ RDF ] na walio nyuma ya JESHI LA RWANDA ndio wenye SERIKALI YA RWANDA.
Kwa kutizama na kuangalia PICHA vizuri au kwa wale wataalamu wa "KUNYUMBUA PICHA" yaani "FACIAL DESCRIPTION IDENTIFICATION" - hao ndio wanao ongoza SERIKALI YA RWANDA na hizo SURA zote zipo TANZANIA.
Kwa upande wa BURUNDI walifanikiwa pia kuitoa SERIKALI iliyoongozwa na CYPRIEN NTARYAMIRA. Ilikuwa ni kipindi cha majonzi sana, ukizingatia alikuwa ni KIONGOZI KIJANA na aliyekuwa amebeba matumaini kwa wananchi walio wengi. Lakini tangu mwaka 1994 - SERIKALI YA BURUNDI ilikuwa imeshikiliwa na JESHI.
Kwa upande wa SERIKALI YA BURUNDI na yenyewe inataka kufanana kimuundo na SERIKALI YA RWANDA, kwani zote ni SERIKALI ambazo zinaongozwa KIJESHI.
Hiyo SURA YA KATIKATI ipo TANZANIA na kwa wale wataalamu wa "KUNYUMBUA PICHA" yaani "FACIAL DISCRIPTION IDENTIFICATION" - hiyo SURA YA KATIKATI ipo TANZANIA.
Baada ya kutoka RWANDA na BURUNDI, mabadiliko ya KISIASA yaliendelea mpaka KONGO na kufanikiwa kumuondoa aliyekuwa RAIS WA KONGO - MOBUTU SESE SEKO na kumuweka LAURENT DÉSIRÉ KABILA kuwa RAIS WA KONGO.
Baada ya kukiuka MAKUBALIANO YA REMERA, aliyekuwa RAIS WA KONGO - LAURENT DÉSIRÉ KABILA alifanikiwa kutolewa kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi na SERIKALI ilioongozwa JOSEPH LAURENT KABILA.
Sasa, kwa kipindi hicho ambacho mambo yote yalikuwa yakifanyika - wale waliokuwa wafanyakazi wa VYAMA VYA USHIRIKA VYA NCU, SHIRECU na WETCU ndio waliokuwa wanufaika wakubwa wa mabadiliko ya KISIASA kwa MATAIFA YA RWANDA, BURUNDI na KONGO. Kwahiyo walijijenga KIUCHUMI kutokana na VITA NA SIASA zilizokuwa zikiendelea kwenye NCHI ZA MAZIWA MAKUU hususani kwenye MATAIFA YA RWANDA, BURUNDI na KONGO.
Vile vile wale wajumbe wote waliopitisha "MAAZIMIO YA TABORA" yaani "TABORA DECLARATIONS" walifanyika kuwa ni miongoni mwa JAMII zinazotengeza ule MFUMO WA SIASA ZA MAFIGA MATATU ukiongeza ile JAMII YA WATU WA PWANI ambayo ndio JAMII inayoongoza kuwa na VIONGOZI wengi ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM.
Kwahiyo "AZIMIO LA TABORA" yaani "TABORA DECLARATION" ndio iliyotoa TASWIRA MPYA NA MUELEKEO WA TANZANIA kama TAIFA tangu mwaka 1991/92 mpaka leo.