Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana


Nimeisoma juujuu. Nikipata nafasi nitaisoma kwa makini. Kwenye muungano inaonyesha kuwa, yalikuwa matokeo ya msukumo wa kimataifa na sio grand scheme of things kama tulivyofundishwa madarasani au kama Nyerere alivyokuwa anaupigia debe. ...
 
Na hata hao waliopo hai, hawahojiwi kwa makusudi maana kuna tabaka linataka watoto wetu wafundishwe historia wanayoitaka wao wafundishwe na wala sio historia halisi ya nchi hii
 

Mkuu kitendo cha wewe kusema eti Ubepari ni "unyonyaji" kinaonesha wazi bado unawaza kwa kutumia propaganda za Kijamaa. Sio kweli kuwa Ubepari ni unyonyaji kama ilivyo sio kweli kwa wakomunisti na wasoshalisti hawaamini Mungu.

Ukisema kuwa ingekuwa ngumu kuondoa tawala za kichifu huu ni uongo, sio ujamaa ulioondoa tawala za kichifu bali ni system. Nchi hii system ikitaka jambo fulani lisiwepo halitakuwepo hivyo hivyo wangeondoa utawala wa kichifu.

Tatizo tukiwaza Ubepari tunauwaza kwa namna ambayo Mkoloni aliutumia hapa nchini, ndio maana mawazo ya ubepari ni unyonyaji yanakuja. Sisi tuliona mkoloni na siasa yake vyote havifai, hili lilikuwa kosa kubwa.

Kwa asili tu jamii za kitanzania nyingi ni mabepari, Ujamaa sio asili yetu. Ndio maana kulikuwa na matajiri wachache wanao hodhi uchumi wa jamii mfano machifu, wapigangoma hodari, waganga hodari na askari hodari bila kusahau wakulima na wawindaji hodari.

Hawa wote walipata mali na utajiri kwa kufanya kazi zao kwa bidii kubwa wala hawakuiba kwa wenzao.

Ujamaa umevuruga mfumo asilia kwa nguvu ndio maana jamii kubwa ni maskini inategemea "serikali itafanya" hata ajira leo hii tunategemea serikali, hayani matunda ya siasa ya kijamaa.

Narudia Ujamaa haukuleta umoja nchini, bali vyombo vya ulinzi na usalama ndio vimeleta huu umpja na amani tuliyonayo. Hata ndani ya Ubepari kwa vile tungekuwa na Jeshi imara na vyombo vya usalama makini bado tungekuwa na Umoja na Amani.

Kenya, Zambia walilega lega kwenye hivi vitu viwili ndio maana wamezidi kuanguka kijamii.

Leo hatuna Ujamaa Active ila tuna Umoja na Amani, vijana chini ya miaka 20 wanaishi pamoja, sio kwasababu wanaujua Ujamaa La! na sio kwa mapenzi yao La! ni kwa mapenzi ya System na vyombo vya usalama.
 
umeongea vema sana
 
Washindi huwa ndio wanaoandika Historia, na bahati mbaya sana mara nyingi huwa wanaindika jinsi wanavyojisikia.
nafkiri mwalimu alitaka kumfutilia jamaa mbali kwenye historia ya nchi na amefanikiwa
 
Kwa politics za miaka ya 1960’s, na hali halisi ya Tanganyika kipindi kile tungejiingiza kwenye ubepari hii nchi ingekufa.

Sio kweli, tatizo lilianza pale tulipolazimisha mabepari kufuata siasa za kijamaa. Wengine wakakosa vyanzo vya mapato na utajiri wakaamua kuiba serikalini na kuwa mafisadi.

Kwa mfumo wetu wa ulinzi wala taifa hili lisingekufa. Tuna mfumo imara sana kiulinzi na watu wanafanya kazi kubwa mimi na wewe tuweze ku comment hapa.

Hili halina uhusiano na huo Ujamaa wala Ubepari
 
Nyerere anatambulishwa na kipindi alichoishi. Wengine ni kama kinjekitile na risasi kugeuka maji, Shaka Zulu na vita vya Mfekane, Sumanguru na vita vya kimiujiza/kichawi
Dunia ya leo ni tofauti sana labda wangeishi leo wasingejulikana.
Hatuwezi kupuuza aliyofanya Nyerere wakati ule. Pia ni vizuri historia ingemtendea kila mtu haki.
Nyota ya Nyerere iling'ara kote duniani. Hapakuwa na nguvu ya kuizima.
Avumaye baharini ni papa lakini wengine wamo pia.
Ni bahati mbaya Kambona hakupata upenyo mbele ya Nyerere.
Ni Nyerere aliyepo katika media nyingi duniani na miongoni mwa wanafalsafa na si Kambona
Tunachoweza kufanya ni kuandika historia ya Kambona kwa kumtendea haki
Kila zama na kitabu chake.
 
sawa lakini baadae walimnyanyasa kambona mpaka akakimbia nchi kitu ambacho mwalimu hakupaswa kufanya ,alafu cha ajabu zaidi ni kwamba sijaona sehemu inasema oscar alikua na uchu wa madaraka au alitaka kumreplace mwalimu
 
lakini mwisho wa siku TZ tumekua nchi ya kibepari kama alivyotaka kambona na tumefanya vizuri zaidi ndani ya ubepari kuliko ujamaa kitu ambacho kambona alishatoa signal mapema kama tunaenda chaka lakini hawakumsikiliza sio siri kiuchumi tuko miaka ya 2005
 
Lkn at the end USA ideology zao ndio jibu sahihi. Ujamaa umekazia kuwatawala watu, ikiwemo kuwakandamiza kiuchumi, kumbuka mifumo ya kijamaa uruhusiwi kufikiri zaidi ya anaekutawala, utakiwi kuwa na utajiri au elimu kuliko anaekutawala. Ubepari umekazia uhuru wa kiuchumi KILA mtu avune kadri awezae kwani kadri mtu anavyovuna ndipo ajira, kodi uongezeka maradufu
 
Kuleta ideology failure za Mwalimu Zama hizi ni sawa na kuweka viatu kwenye friji. Ideology za Mwalimu zilifaa Zama za giza na sio sasa za global vision.
 

Kusema ubepari ni unyonyaji ni ufilisi wa fikra.ubepari unazalisha ajira,unaongeza makusanyo makubwa ya Kodi,unakuza uchumi,
 
Ulifaidi vipi elimu? Wakati wake aliweka sera za kuwa na watu wachache wenye elimu ya juu, hata mataifa yenye watu wachache barani yalitupita kuwa na wasomi
Long time no see! Kimsingi mwalimu alituacha sehemu nzuri sana kimaendeleo na kielimu.
Elimu: Uendelezaji wa elimu katika nchi ni jambo la hatua kwa hatua. Ukikurupuka na kuamua ''kufyatua'' vyuo vikuu kama walivyofanya sasa una hasara. Hasara kubwa ni kupata ma-graduate waliyo incompetent na nchi kuelemewa na vijana wasiyo na ajira. Mwalimu alikuwa anaendeleza elimu hatua kwa hatua.
Maendeleo: Nyerere alituachia misingi mingi bora ya maendeleo hasa kwenye sekta ya viwanda na mashirika ya umma. Labda ''kosa'' alilofanya ni kutojua kuwa mwafrika hawezi kusimamia na kuendeleza mali ya umma. Niliwahi kutembelea nchi za Scandinavia na kukuta mfumo wao hauna tofauti kubwa sana na ule Nyerere aliokuwa anajaribu kuujenga. Tofauti ni kuwa wananchi wa Scandinavia ni wachapa kazi na waaminifu kwenye kusimamia mali ya umma.
 
Kusema ubepari ni unyonyaji ni ufilisi wa fikra.ubepari unazalisha ajira,unaongeza makusanyo makubwa ya Kodi,unakuza uchumi,
Ubebari ni unyonyaji! Ndugu yangu jaribu kutembelea nchi za Scandinavia ndiyo utajua ukweli wa msemu huu. Kule mfumo wao unaweza kudhani ni ujamaa wa aina fulani lakini wananchi wake wana maisha mazuri sana kuliko hata Marekani.
 
Ubebari ni unyonyaji! Ndugu yangu jaribu kutembelea nchi za Scandinavia ndiyo utajua ukweli wa msemu huu. Kule mfumo wao unaweza kudhani ni ujamaa wa aina fulani lakini wananchi wake wana maisha mazuri sana kuliko hata Marekani.
Asiye fanya Kazi na asile, ubepari utengeneza mazingira sawa kwa nyote kufanikiwa,kuwa masikini au kuwa tajiri ni maamuzi yako.
 
Asiye fanya Kazi na asile, ubepari utengeneza mazingira sawa kwa nyote kufanikiwa,kuwa masikini au kuwa tajiri ni maamuzi yako.
Siyo kweli kuwa filosofia ya ubebari ni asiyefanya kazi na asile. Kwenye ubebari unaweza kuwa mchapa kazi mzuri sana sana lakini ukashia kuishi maisha ya kifukara mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…