Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee apa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.
Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia badae sana baada ya kuskia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.
kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.
Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake". Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"
Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona
Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere
Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa
Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii
Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always
"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
Oscar Kambona - Wikipedia