Kwa miaka ile ya uhuru, ujamaa ulikuwa ni essential sana kwa jamii yetu kwasababu taifa lilikuwa ni changa na hatukuwa sawa.
Ujamaa ulileta hali ya usawa na umoja katika kujenga taifa. Tukawa na lugha moja ya kiswahili na leo unaona faida yake unakwenda mkoa wowote na kuongea na watanzania wenzako bila pressure.
Pia kwa nyakati zile kulikuwa na baadhi ya watanzania walishaanza elements za matabaka, watu kama wachagga walikuwa na mifumo ya uchief akina mangi ambao waliamini ndio top position na waliiheshimu but Hayati baba wa taifa alifanya jitihada sana kukemea watu kujiona sio sehemu ya umoja wa taifa imagine leo bila kuwapo umoja wa taifa, kungekuwa na jamii zinawadominate wengine kwa ubabe na kuhodhi rasilimali kisheria kabisa bila kupingwa. Ila leo hapa ukiongea huo upuuzi kwanza kila mtu atakuona Takataka.
Kwahiyo ninyi watoto wa kizazi hiki cha sasa mkiwa mnaambiwa haya mastory ya ajabu ajabu ya sijui nani alifanya nini tumieni na akili zenu kuangalia kipi kinatija kipi hakina.
Sasa mfano unataka kwenye historia tuwaongelee wazee waliokuwa wanataka kumpindua nyerere kama akina bibi titi akina nani sijui yule aliyefia kigamboni ambao wao sera yao wamebeba maneno ya udini ndani yake kuwa waislaam ndio waligombania uhuru wa taifa hili.... Sasa unajiuliza huyu mtu anataka kila mtu aishi kwa misingi ya dini anayoiamini yeye au tumualeweje?!
So ni ubinafsi. Unapomuongelea nyerere hebu jaribu kwanza kumjua. Yule mzee alichofanya ni kutuwekea misingi bora sana ya jamii, sera ya ujamaa kwa nyakati zile ilikuwa muhimu sana katika kutuimarisha kama taifa changa lililotoka katika usimamizi wa wakoloni, sasa tungelianza hili taifa na sera za kibaguzi za kabila fulani liwe juu ya makabila mengine si ajabu leo katiba ungesema wasukuma, wachagga au wahaya au wahehe, au wazanaki, au wagogo ndio jamii teule ambayo inatakiwa kuwa katika uongozi. Au basi katiba ingesema dini ya usislam ndio dini ya taifa wengine nyie ni makafiri mtasali kwa maelekezo ya viongozi wa dini ya kiislam.
Haya yote nyerere aliyazima mapema sana. Na hao watu ambao unasikia walifutwa katika vitabu vya history sio kwasababu hawakuwa na mchango katika mapambano na harakati za uhuru, ila walikuwa na ajenda zao binafsi na za kimakundi.
Nitakupa mifano, wakati nyerere anakwenda kudai uhuru wa Tanzania nzima, kuna chifu sijui mangi nani yule alienda kudai uhuru wa wachaga tu baaasi, yaani kilimanjaro nadhani na Arusha kuwe ni taifa huru wasihusiane na jamii zingine, sasa huu ufala wewe unataka uandikwe katika history.
Kuna wapigania uhuru walitaka mpindua nyerere na kuanza harakati binafsi wao wakataka nyaraka za uhuru zitambue Tanzania ni jamii ya kiislam kama vile kule Sudan, somali, wakati kwa miaka ile karibu 90% ya watanzania hawapo katika Imani moja wala uislam. Sasa unataka vitabu vya history viwaongelee wapuuzi kama hawa hata kama walikuwa na harakati?!
Nyerere hata anafariki tazama maisha yake na familia yake, hivi unaweza fananisha na familia za akina mwinyi, mkapa, kikwete, na huyu wa sasa, hivi hata wanafanania.... Tazama walivyojiweka mbali na siasa za sasa. Tazama namna hawajihusishi na maswala ya uongozi au kuwa kiherehere.
Hivi mfano hili taifa lingekuwa Baba wa taifa ni kikwete, hivi 90% ya watendaji wa serikali si wangekuwa wakerewe, na katika noti hata ridhiwani angewekwa kama mtoto wa taifa. Maana sio kwa tamaa zao.
So, as much as tutamsema huyu mzee lakini, tukubali ana mema yake na ametufikisha hapa kwa wema tu sio hila wala nia mbaya. Na tunamsingi mzuri sana wa kujipanga na kuwa taifa bora afrika.
Huyu wa sasa anakosea kuleta sera za kijamaa za miaka ile nyakati hizi ambapo haziendani na nyakati hizi za mifumo ya uchumi ya soko huria.
Na tusipende kutumia neno uchumi wa kibepari bali tuseme uchumi wa soko huria.....
Tuendelee kuheshimu n akuenzi mema ya Baba wa taifa mwalimu J. K. Nyerere, na tujitahidi kuondoa huu mfumo wa ujamaa wa kifukara tujenge ujamaa wa kisasa wa soko huria ambapo tutashare mitaji, mbinu, ili tupambane na mataifa jiarani katika kuwa super economy wa afrika.