Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

ujamaa ulikua na maandalizi gani? ni either you do it au you dont hakuna kitu lichokua kinahitaji maandalizi kabla ya uhuru, tulikua tunaanza from scratch
Hata chiefdom system za tanganyika zilikuwa na modality ya ujamaa,ngoja somo la historia liludi probably wata rescue hiki kizazi kisichojua tulikokuwa na tunakoenda
 
Kambona hakuwa mjamaa alikuwa mbepari na fikra zake zilikuwa za kibepari na Kama hawangetofautiana na Nyerere tungekuwa mbali Sana na anayesema alikuwa mjamaa anajua kwa nn aliishi uhamishoni?
Unaposema Kambona alikuwa bepari, inabidi utaje kaanza kuwa bepqri mwaka gani?

Kwa sababu Kambona kawa introduced kwa Nyerere na Abbas Sykes. Akaja kuwa katibu Mkuu wa TANU.

Alishika nafasi hiyo kwa muda mrefu akihubiri sera za TANU.

Sasa ubepari wa Kambona umeanzia lini?

Baada ya kujiuzukunuongozi TANU au kabla?

Kuna mambo katika TANU Kambona na Nyerere - in fact Nyerere na viongozi wengibwa TANU- walipishana. Kubwq kqbisa lilikuwa suala la uzawq, qmbalo Nyerwre alilipinga maisha yaje yote mpaka siku za Idi Simba.

Hii ni moja ya sababu Nyerere alijiuzulu Uwaziri Mkuu wiki sita tu baada ya kuapishwa, akamuachia cheo Kawawa na kwenda mikoani kuimarisha TANU.

Kulikuwa na power struggle ndani ya TANU tangu Uhuru, na ilijikita zaidi kwenye mambo ya uzawa kulikonmambo ya itikadi.

Nasikitika watu wanapojadili tofauti za Nyerere na Kambona wanaongelea ubepari/ ujamaa zaidi ya hizi habari za uzawa.

Baadaye Kambona alivyojiuzulu uongozi TANU ndiyobalianza kusema sera za serikaki kwamba ni mbovu na akasema kufuta vyama vya upinzani ni jambo baya.

Lakini alivyokuwa TANU alitetea sana sera za TANU, ambazo hazikuwa za kibepari. Sasa ubepari wake ulikuwa opportunistic au halisi? Ulianza lini?

Soma kitabu cha Paul Bjerk nimekiweka hapa kaeleza hayo.
 
Hata chiefdom system za tanganyika zilikuwa na modality ya ujamaa,ngoja somo la historia liludi probably wata rescue hiki kizazi kisichojua tulikokuwa na tunakoenda
Actually Nyerere alipata theme ya Ujamaa iliyokuwa imewekwa pamoja kimaandishi na Chief mmoja wa Kichaga, akaipenda na kuifanya policy ya TANU.
 
Mimi mwenyewe naamini under KAMBONA taifa letu lingekuwa so powerful Africa kiuchumi ,kijamii na kisiasa

Mungu aliruhusu iwe tofauti kwa sababu zake tu but KAMBONA kwa kumsoma katikati ya ufinyu wa taarifa kumhusu naona alikuwa ni far better kwa Nyerere
 
Actually Nyerere alipata theme ya Ujamaa iliyokuwa imewekwa pamoja kimaandishi na Chief mmoja wa Kichaga, akaipenda na kuifanya policy ya TANU.
kambona akamuambia tutenge vijiji vichache tufanyie majaribio kwanza kabla ya ku adopt hii system, lakini nyerere kwa ujinga wake akaleta systeme na kuiingiza moja kwa moja
 
Mimi mwenyewe naamini under KAMBONA taifa letu lingekuwa so powerful Africa kiuchumi ,kijamii na kisiasa

Mungu aliruhusu iwe tofauti kwa sababu zake tu but KAMBONA kwa kumsoma katikati ya ufinyu wa taarifa kumhusu naona alikuwa ni far better kwa Nyerere
way too better, kambona alifuta facts nyerere aliongoza kwa mihemko
 
nitafarijika sana kama siku moja mzee Mohamed Said ataandika makala maalumu ya kumuelezea kambona kama vile anavyofanya katika kuwaandikia makala wazee wake wa kariakoo walioshiriki katika harakati za kisiasa kabla na baada ya uhuru.

najua uwezo huo unao ila hajajisikia tu kufanya hivyo. labda kwa kuwa kambona hakuwa mwenzetu kiimani.
Kwani Kambona alikua Mwislam mpaka Mzee Mohamed amwandikie Makala?
 
Wazee waliokuwepo kipindi hicho wananafasi kubwa sana ya kutoa historia ya nini hasa chanzo cha wawili hawa kutoelewana ila wamekaa kimya sana
 
Zamani nilikuwa na mawazo kama mtoa post ila baada ya kusoma taarifa nyingi zaidi na kutembelea baadhi ya nchi za Afrika nikaona Mwalimu ni shujaa wa muda wote pamoja na makosa yake yote. Hapa Afrika karibu kila nchi ina ukabila, ukanda na ubaguzi. Mfumo uliowekwa na Mwalimu ni adimu mno na tofauti kabisa na nchi nyingi. USA hadi imekuwa kitu kimoja palitokea vita kali ya wenyewe kwa wenyewe. Lakini Mwalimu aliweza kutuunganisha bila kumwaga damu. Nadhani kizazi cha sasa pamoja na viongozi wetu tuachane na lawama za mambo yaliyopita tujikite kuendeleza mazuri na kila mmoja kufanya wajibu wake. MUNGU IBARIKI TANZANIA. KIDUMU CCM
 
Umewaza upande mmoja tuu.kuna mengi Sana ambayo bila ujamaa tungekuwa nchi tofauti
 
Zamani nilikuwa na mawazo kama mtoa post ila baada ya kusoma taarifa nyingi zaidi na kutembelea baadhi ya nchi za Afrika nikaona Mwalimu ni shujaa wa muda wote pamoja na makosa yake yote. Hapa Afrika karibu kila nchi ina ukabila, ukanda na ubaguzi. Mfumo uliowekwa na Mwalimu ni adimu mno na tofauti kabisa na nchi nyingi. USA hadi imekuwa kitu kimoja palitokea vita kali ya wenyewe kwa wenyewe. Lakini Mwalimu aliweza kutuunganisha bila kumwaga damu. Nadhani kizazi cha sasa pamoja na viongozi wetu tuachane na lawama za mambo yaliyopita tujikite kuendeleza mazuri na kila mmoja kufanya wajibu wake. MUNGU IBARIKI TANZANIA. KIDUMU CCM
pamoja na hayo lakini mwalimu hakua peke yake ktk harakati za nchi hii wapo watu ambao wamefichwa na jamii inatakiwa kuwafahamu, sio kuwaficha kwasababu tu walipingana na mwalimu kimtizamo, Oscar kambona na Mwalimu wanashea 5050 katika ukombozi wa nchi hii lakini Kambona hakumbukwi kwa chochote! Mawazo ya Nyerere hayakua mapana na marefu kama ya Kambona japo wote waliipigania TZ, kiufupi kumchafua kambona ndio kulimfanya nyerere awe juu! Aliyeweka Nyerere day ni nani na alikua na maana gani kwanza??
 
ntakitafuta na nitakisoma lakini, kwa uliachinda hapa kambona alikua anapigania maslahi yetu, na ni kwanini ndugu zake waliteswa na kuuwawa kwa kitu wasichohusika nacho??
Mkuu maoni yako ni mazito hivyo unapaswa kuambatanisha ushahidi wa hayo maandiko uliyosoma na kufikia kutoa tamati hii juu ya Nyerere na Kambona.

Inatakiwa ujifunze kwa Kiranga ameweka maoni yake na kuambatanisha maandiko (andiko) kama ushahidi.
Wewe umeweka kama hearsay stories.
 
Nashukuru umeona mkuu.Tufanye mjadala wa kisomi zaidi kuliko wa hearsay.

I am much obliged for your endorsement.
 
Back
Top Bottom