Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

a59dec92e540b3b9b8141d94b72c5555.png

Tofauti na kampuni nyingine zinazomilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ, hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ wa TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ndio wamiliki halali wa kampuni ya STANDARD MEDIA GROUP ya KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช.

Hii STANDARD MEDIA GROUP ya KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช ndio kampuni kubwa zaidi inayopatikana AFRIKA YA MASHARIKI inayohusu MASUALA YA UHANDISHI WA HABARI, MAGAZETI, RADIO NA TELEVISHENI.

Hii STANDARD MEDIA GROUP ya KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช ni moja ya kampuni zinazomilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ ambayo inatumika kama ni sehemu ya ajira kwa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ waliohamia KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช.

Vile vile, kama ilivyo kwa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ waliohamia UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ kuwa na timu ya mpira wa miguu inayoitwa EXPRESS FC na hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ waliohamia KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช wana timu ya mpira wa miguu inayoitwa KARIOBANGI SHARKS FC. Hizi timu zote mbili zinashiriki michuano ya LIGI KUU kwenye nchi husika.

Kwahiyo, hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ kwa upande wa nchi za UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ na KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช wamejitosheleza kwa kila kitu, ukizingatia MASUALA YA KIJAMII NA MAHUSIANO YA WATU na wataendelea kufanya UWEKEZAJI kama huo kwa MATAIFA YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ, BURUNDI ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ฎ, KONGO ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฉ, ZAMBIA ๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฒ, MALAWI ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ผ na MSUMBIJI ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฟ ili kukamilisha UWEKEZAJI KWA NCHI ZOTE ZA MAZIWA MAKUU yaani GREAT LAKES REGIONAL ECONOMY.
 
Jaribu tena kuangalia matokeo ya mechi za jana kwenye michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE [emoji460]. Lengo ni kuonesha timu zinazomilikiwa na WATANZANIA [emoji1241].

Timu ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] ni SEVILLA. Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] wanamiliki timu za mpira wa miguu zipatazo tatu [ 3 ] kwenye msimu huu wa mwaka 2021/22.

Na timu ambazo zinamilikiwa na SERENGETI yaani CHUI ni BAYERN MUNICH na CHELSEA. Kwahiyo hawa SERENGETI yaani CHUI wanamiliki timu za mpira wa miguu zipatazo tano [ 5 ] kwenye msimu huu wa mwaka 2021/22.

Na timu ambazo zinamilikiwa na WATANZANIA [emoji1241] wengine tofauti na jamii za SERENGETI yaani CHUI na MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] ni MALMO FF na WOLFSBURG.

Hizi timu za MALMO FF na WOLFSBURG wamiliki wake wanatoka MIKOA YA KASKAZINI MWA TANZANIA [emoji1241] yaani [ MANYARA, ARUSHA, KILIMANJARO ]. Hawa wamiliki wa hizi timu za mpira ndio tunaweza kusema wanamiliki UCHUMI kwa kiasi fulani, sio sana.

Vile vile ukiondoa hizo timu za mpira tajwa hapo juu, pia kuna timu ya mpira wa miguu ambayo inamilikiwa na SERIKALI YA TANZANIA [emoji1241]. Timu hiyo ni [...]. Sio vyema kuitaja mapema kwa sababu wahusika wenyewe yaani SERIKALI YA TANZANIA [emoji1241] wamefanya ni SIRI.

Kwahiyo kwa kuangalia mechi za juzi na mechi za jana tayari umeshafahamu timu za mpira wa miguu ambazo zinamilikiwa na WATANZANIA [emoji1241] kwenye michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE [emoji460].
Hahahaha hakika leo nimekuelewa barabara

Someone come here to rescue your buddy
 
Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee hapa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu Nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia baadae sana baada ya kusikia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya Kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya Nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona Kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake".
Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda Urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo Kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho Oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona.

Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio Kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere.

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa ambaye ni co-founder wa hii nchi kwangu mimi alichangia 50% ktk kutengeneza taifa hili sawa sawa na mwalimu, yaani ni kama vile "stive wozniak na stive jobs", steve jobs alitumia akili za stive wozniak na credit akajiapa yeye mwenyewe

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

UPDATE:
Watu wengi kwenye comments wanasema kwamba ujamaa ulituleta karibu, lakini ujamaa huo huo ndio uliotuletea umaskini, kwa hiyo logic yake ni kwamba mwalimu alichagua umaskini na umoja dhidi ya maendeleo ambayo hatuna uhakika kama yangetugawa, lakini kabla ya yote Kambona alimshauri kwamba kabla ya ku adopt ujamaa tuufanyie kwanza majaribio , tutengeneze vijiji vichache ambavyo vitaishi kijamaa ili tuone hii system itafanya kazi lakini mwalimu alikataa akaiingiza moja kwa moja bila kujua risks zake ni nini kitu ambacho kambona alishakiona


"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
refence:

====

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

Christopher Makwaia

WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.10.jpeg

1. Usuli
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwร  na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe
KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"
Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School
KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa ยฃ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School
KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpeg

6. Ualimu Alliance Sec. School
Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena
KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU
Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000
KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25282%2529.jpeg

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU
KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK
Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957
Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London
Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika
Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.12.jpeg

16. KAMBONA Arejea Bongo
KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje
Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE
KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964
Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966
Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967
Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond !!
Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.
Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA
Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK
Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani",1967
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.
Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968
Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:
"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968
Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA
NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969
Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini
Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:
1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!!.

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969
Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7 ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha).

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo. M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978
Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU( Mwasisi wa TANU).
OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo, wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani
Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua, anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo
KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967:
Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka:
"Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK
Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE
Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani,1992
Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!.

42. NYERERE Amjibu KAMBONA
NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA
Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA
KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997
KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007
Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:
Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:
ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!! - MICHUZI BLOG (issamichuzi.blogspot.com)

Oscar Kambona - Wikipedia
View attachment 1983785
Kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Lakini kitu kimoja dhahiri ni kwamba wanaoathirika na siasa ni wananchi either positively or negatively
 
Hao STANDARD MEDIA GROUP wako vizuri sana nawakubali vilivyo.

Nilikuwa nikizipata mubashara habari za machafuko ya KENYA kunako DISEMBA 2007 kupitia MEDIA zao.

Hawa STANDARD MEDIA huwa wana MAKALA nzuri sana za KIMATAIFA zihusuzo MASUALA YA JAMII na SIASA.

WAHU, Kumbe ni NYANYA yake NAMELESS !?
Couple yao nzuri.

Na MR. TI-CHII ni Mnyama LEO !? Sikuwa nafahamu, Ila NYIMBO zake ni COMEDY tosha zinaburudisha sana na wakati mwingine hutuacha MBAVU taabani.

Namkumbuka jamaa huyu TI-CHII na WANYAMA wengine wa KENYA walipokuwa wakifanya yao pale OGOPA DJs.

JAGUAR ni chaguo langu bora kabisa hili, Ukiachana na NAMELESS, NYOTA NDOGO, AMANI, na NYASHINSKI.

Namkumbuka sana Mnyama huyu JAQUAR kwenye ngoma zake za KIGEUGEU na KIOO, Aliua sana humu.

KUDOS, CHARLES MANDELA!
 
Hahahaha hakika leo nimekuelewa barabara

Someone come here to rescue your buddy




Jaribu kusikiliza mahojiano ya MWANASIASA wa TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ anayeitwa TUNDU ANTIPAS LISSU, alikuwa haelewi kuwa hicho kituo cha televisheni cha KTN kinamilikiwa na WATANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ yaani MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ na hata huyo mwanahabari anayefanya nae mahojiano ni MKENYA mwenye ASILI YA TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ na yeye huyo mwanahabari ni MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ.
 
Hao STANDARD MEDIA GROUP wako vizuri sana nawakubali vilivyo.

Nilikuwa nikizipata mubashara habari za machafuko ya KENYA kunako DISEMBA 2007 kupitia MEDIA zao.

Hawa STANDARD MEDIA huwa wana MAKALA nzuri sana za KIMATAIFA zihusuzo MASUALA YA JAMII na SIASA.

WAHU, Kumbe ni NYANYA yake NAMELESS !?
Couple yao nzuri.

Na MR. TI-CHII ni Mnyama LEO !? Sikuwa nafahamu, Ila NYIMBO zake ni COMEDY tosha zinaburudisha sana na wakati mwingine hutuacha MBAVU taabani.

Namkumbuka jamaa huyu TI-CHII na WANYAMA wengine wa KENYA walipokuwa wakifanya yao pale OGOPA DJs.

JAGUAR ni chaguo langu bora kabisa hili, Ukiachana na NAMELESS, NYOTA NDOGO, AMANI, na NYASHINSKI.

Namkumbuka sana Mnyama huyu JAQUAR kwenye ngoma zake za KIGEUGEU na KIOO, Aliua sana humu.

KUDOS, CHARLES MANDELA!

0786ea0bb027503176fb61e77d32cf2c.png


5abb0f5b837f09e58e107465829984df.png

Hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ yaani wale waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU wamejitahidi kuwekeza sana nchini KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช na UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ.

Na ukiondoa kampuni za usafirishaji wa abiria pamoja na mizigo za SIMBA COACH, TAHMEED pamoja na MASHCOOL, hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ ndio wamiliki halali wa kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo inayoitwa MODERN COAST.

Hii kampuni ya MODERN COAST inaweza kuwa ni kampuni ya pili au kampuni ya tatu kwa ubora nchini KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช, kwa sababu ni kampuni ambayo inafanya kazi zake za kibiashara kwenye nchi zipatazo nne [ 4 ], ambazo ni KENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช, UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ na TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ kwa upande wa AFRIKA YA MASHARIKI wapo vizuri sana kiuchumi na kibiashara.
 
Mkuu, Charles Mandela!
Ukipata wasaa, Naomba unigusie kitu kuhusu MR. SAULI.

Hivi MR. SAULI ni Mnywaru kweli au ni MHABESHI ?

Kama USOMALI vile kama UKUSHI vile, Nisimuelewi elewi huyu MR. SAULI.
 
Kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
Uko sahihi kabisa! Lakini WAINGEREZA ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ง huwa wanasema hivi - "An empty gallon doesn't make any noise". Yaani kwa lugha ya KISWAHILI ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ tunaweza kusema hivi - "Debe tupu, halina mshindo".

Kwahiyo kwenye SIASA ni lazima uwe uko vizuri KIUCHUMI na KISIASA ili uwe na MTAJI WA KISIASA. Hali hii ndio itakufanya kuwa na uhalali wa kukaa meza moja ya majadiliano na kutafuta muhafaka.

Tofauti na hapo, sidhani kama utakuwa na uhalali wowote wa kufikia muhafaka kwenye jambo lolote lile linalohusu SIASA.

Kwahiyo jambo la msingi na muhimu ni kutafuta UCHUMI, mambo mengine yatakuja yenyewe na hapo ndio utakuwa na uhalali wa kusema ya kwamba - kwenye SIASA hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
Lakini kitu kimoja dhahiri ni kwamba wanaoathirika na siasa ni wananchi either positively or negatively
Siku zote wanao athirika na maamuzi ya kisiasa au uzembe wa kisiasa ni WANANCHI WA KAWAIDA lakini hawa MWASHITA yaani SIMBA ๐Ÿฆ yaani wenyeji wa MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA NA TABORA hii dhana wanaenda kuifuta, kwa sababu wao wanajitahidi sana kuwekeza kwenye sekta mbali mbali kiasi ambacho wanafanyika kuwa ni msaada kwa watu wao wenyewe.
 
Mkuu, Charles Mandela!
Ukipata wasaa, Naomba unigusie kitu kuhusu MR. SAULI.

Hivi MR. SAULI ni Mnywaru kweli au ni MHABESHI ?

Kama USOMALI vile kama UKUSHI vile, Nisimuelewi elewi huyu MR. SAULI.

46fee65869a4ab8d36631d12f29e40c5.png


Yaani sijui niseme nini! Lakini ule UKWELI WA MAMBO NA UHALISIA WA MAZINGIRA, RAIS PAUL INGABIRE KAGAME WA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ ni IDEAL PERSONELLY [ IP ] yaani ni MTU aliyeandaliwa kwa kutengenezwa WASIFU ili kwenda kuitawala RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ.

Kwa tafsiri ya lugha ya KIINGEREZA ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ง huwa wanasema hivi - IDEAL PERSONELLY [ IP ] is a kind of personal characteristics that has been designed and trained for special purposes including LEADERSHIP.

Na kwa tafsiri ya lugha ya KIINGEREZA ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ง huwa wanasema hivi - IDEAL FAMILY [ IF ] is a kind of family where by its family members do not exist in REALITY. And IDEAL FAMILY composed of IDEAL PERSONELLIES [ IPs ].

Kwahiyo ukiondoa hiyo dhana ya mambo ya kusema ya kwamba MISTER SAULI ni MNYARU au MHABESHI au MSOMALI au hata MKUSHI ni dhana ambayo haitasaidia kwa sababu sio yeye anayetawala TAIFA LA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ na wala hausikii kwa mambo yaliyotokea RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ na yanayoendelea kufanyika kwenye SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ.

RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ ni BOSHENI na wenye SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ wapo TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ na washika dau au wadau wa SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ wapo TANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ. Wengine mnatembea nao bila ya kufahamu! Wengine mnakula nao kwenye migahawa na hoteli bila ya kufahamu! Wengine mnafanya nao mazoezi kwenye viwanja vya mpira wa miguu bila ya kufahamu!

Lakini yote kwa yote, wenye SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ tangu waasi wa RPF [ RWANDA PATRIOTIC FRONT ] walivyochukua NCHI ni WATANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ na hao WATANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ndio wenye JESHI LA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ yaani RWANDA DEFENSE FORCE [ RDF ]. Kwahiyo SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ ni SERIKALI ambayo inaendeshwa KIJESHI na sio SERIKALI YA KIRAIA.

Na waliokuwa nyuma ya yale yote yaliyofanyika RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ ni WATANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ waliosoma UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ kwa upande wa SHULE YA SEKONDARI na CHUO KIKUU CHA MAKERERE. Kwahiyo ni VERY BRIGHT PEOPLE and they know what they are doing ๐Ÿ™๐Ÿฝ

Kipindi cha MAUAJI YA KIMBARI ya miaka ya 1994 kulikuwa na HAYATI MWALIMU aliyesoma CHUO KIKUU CHA MAKERERE nchini UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, kulikuwa na MISTER CLEAN aliyesoma CHUO KIKUU CHA MAKERERE nchini UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, kulikuwa na MISTER ABILITY aliyesoma SHULE YA SEKONDARI nchini UGANDA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ na wengine wengi ambao historia itawakumbuka.


35a82e58517950f6f730dbd945bc1985.png


Hata huyu mama JEANETTE KAGAME ni IDEAL WIFE TO MISTER PAUL INGABIRE KAGAME, ni wanamke mwenye familia yake na watoto wake na wanakutana na PAUL KAGAME kwenye shughuli na kazi za kiofisi tu, baada ya hapo kila MTU anakwenda kutimiza majukumu yake ya kifamilia kwenye familia yake.

Na kitu cha kushangaza ni WATU ambao hawajawahi kukutana kimwili, wao hukutana kiofisi tu baada ya hapo kila MTU anafanya yake.

Sasa ni nani aliye nyuma ya SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ? Jibu ni JESHI LA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ [ RDF ]! Na ni nani aliyenyuma ya JESHI LA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ [ RDF ]? Ukiwafahamu walio nyuma ya JESHI LA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ [ RDF ] ndio utakuwa umefahamu WANYARWANDA au WATU WENYE SERIKALI YA RWANDA ๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ.
 
Mpaka sasa sijaona ukiieleza japo nchi mmoja tu mpaka sasa iliyo piga kihatua tokea enzi za uhuru kwa kukumbatia ubepari.

Halafu kwenye hizi harakati husitegemee kila mtu ataandikwa kuna wengine wataendelea kuwa mashujaa wasio imbwa. Mfano Mandela sifa nyingi anapewa yy ila wale walio endeleza harakati kipindi yupo ndani mbona hawaimbwi sana?

Kwame Nkurumah nae hivyo hivyo vip wale wenzake unawasikia? vip Kenyatta?je Fidel Castro naye? So wote hamuwezi kuimbwa, kuna mmoja ata atanyanyuka na wengine mtakuwa chini.
 
Suala la KATIBA MPYA ni ajenda iliyopo mezani kwa upande wa VYAMA VYA KISIASA VYA TANZANIA [emoji1241] na sio ajenda ya KITAIFA.
Pole sana!!
Takwa la katiba mpya ni ajenda ya kisiasa?
Umesahau mara hii kuwa tume ya Warioba walihoji watanzania sio wanachama wa vyama vya siasa na wakasema wanataka katiba mpya?

Akili hizi ndizo zinajidai kumchambua Mwl Nyerere?
 
Pole sana!!
Takwa la katiba mpya ni ajenda ya kisiasa?
Umesahau mara hii kuwa tume ya Warioba walihoji watanzania sio wanachama wa vyama vya siasa na wakasema wanataka katiba mpya?

Akili hizi ndizo zinajidai kumchambua Mwl Nyerere?
Tulishasema humu tangu mwanzo au jaribu kupitia yale yaliyojadiliwa huko nyuma. Au jaribu kudai KATIBA MPYA kama majirani zetu WAKENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช walivyofanya.

KATIBA MPYA siku zote na itaendelea kuwa ni majumuisho ya mapendekezo yote ya kisheria kwenye kila SEKTA kwa MASILAHI YA UMMA WA WATANZANIA ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ WOTE.

Kwahiyo ni vyema na ni sahihi kupitia madhaifu au changamoto za kisheria kwenye kila SEKTA ili baadae tupate ufumbuzi wa kisheria na hatimae kuwa na majumuisho yote ya kisheria kwenye kila SEKTA na kuwa na KATIBA MPYA ambayo imesheheni UKWELI NA UWAZI.





Jaribu tena kuangalia na kutizama mchakato wa KATIBA MPYA kwa majirani zetu WAKENYA ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช ulivyofanyika mpaka kukamilika. Huo ndio utaratibu mzuri na utaratibu wakuigwa kwa TAIFA lolote lile linalohitaji mabadiliko ya KATIBA.
 
Mpaka sasa sijaona ukiieleza japo nchi mmoja tu mpaka sasa iliyo piga kihatua tokea enzi za uhuru kwa kukumbatia ubepari.

Halafu kwenye hizi harakati husitegemee kila mtu ataandikwa kuna wengine wataendelea kuwa mashujaa wasio imbwa. Mfano Mandela sifa nyingi anapewa yy ila wale walio endeleza harakati kipindi yupo ndani mbona hawaimbwi sana?

Kwame Nkurumah nae hivyo hivyo vip wale wenzake unawasikia? vip Kenyatta?je Fidel Castro naye? So wote hamuwezi kuimbwa, kuna mmoja ata atanyanyuka na wengine mtakuwa chini.
Siku hizi kuna watu wengi sana wenye akili ndogo! Wanataka historia itaje hadi aliekuwa anampigia pasi Mwl Nyerere!!

We jionee maajabu mtu aliesema kazaliwa mwaka 1995 anasema eti amefanya uchunguzi kaona Kambona anafaa kuwa baba wa taifa?! Na majitu yame like kibao!!!!

Mimi Kambona aliporudi miaka ya tisini nilishakuwa timamu, Nyerere alikuwa hai pia. Vyombo vya habari wakati huo vilikuwa huru kuliko sasa, sikusikia Kambona akijieleza la maana lolote na aliachwa huru aongee chochote popote pale!
 
Siku hizi kuna watu wengi sana wenye akili ndogo! Wanataka historia itaje hadi aliekuwa anampigia pasi Mwl Nyerere!!

We jionee maajabu mtu aliesema kazaliwa mwaka 1995 anasema eti amefanya uchunguzi kaona Kambona anafaa kuwa baba wa taifa?! Na majitu yame like kibao!!!!

Mimi Kambona aliporudi miaka ya tisini nilishakuwa timamu, Nyerere alikuwa hai pia. Vyombo vya habari wakati huo vilikuwa huru kuliko sasa, sikusikia Kambona akijieleza la maana lolote na aliachwa huru aongee chochote popote pale!
Vijiwe vya kahawa vina waharibu watu wengi sana mmoja wapo huyu mwenye hii thread.
 
Back
Top Bottom