Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Mleta mada anaamini kambona pekee ndiyo alikuwa na mchango chanya kwa hii nchi?. Mi navyojua walikuwepo wengi including wahindi. Sasa nashangaa debe ni kwa kambona tu! Nafikiri atakuwa ni ndugu/kabila lako povu lote hilo sio bure. Inawezekana Mwalimu hakufanya vya kutosha kama unavyotaka lakini changamoto zilikuwa nyingi kwa waanzilishi na yeye aliwahi kiri. Kubali Pinga mwl alifanikiwa kuleta umoja, nchi kuwa na lugha yake, kuwezesha raia kumiliki ardhi na kujenga uchumi/viwanda Muhimu Hivi vitu havipo hapa afrika. Bila kusahau watu wakubwa kama Mugabe alipendekeza aitwe baba wa afrika kwa mchango wake katika bara hili. Mi nafikiri hiyo inatosha, wa kuwalaumu sana kwa upande wangu ni Hawa wanaoendeleza kijiti ambao mikataba wanayofanya bora hata mtemi mangungo wa msovero! Ndiyo maana alikuwa hajui hata kusoma lakini wa sasa ni wasomi lakini ndiyo hivo!
Huo ndio ukweli wenyewe! Na kwa kuongezea kidogo, ni kwamba - HAYATI MWALIMU hakuwa YESU au kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kwamba - HAYATI MWALIMU hakuwa MTUME MUHAMMAD!

HAYATI MWALIMU alikuwa ni BINADAMU WA KAWAIDA na alikuwa ni mtu mwenye matamanio kama BINADAMU WENGINE.

Kwahiyo HAYATI MWALIMU aliongoza NCHI kwa kipindi kirefu sana, huku akiweka AKIBA kwa kizazi chake cha baadae. Sasa hiyo AKIBA mimi na wewe na wengine hatufahamu ni kiasi gani, lakini ni AKIBA YA KUTOSHA.

Hiyo AKIBA YA KUTOSHA inatosha kabisa kuhudumia kizazi chake chote na JAMII YA SERENGETI kwa ujumla. Kwahiyo sio AKIBA ndogo kama wengine wanavyodhani, ni AKIBA kubwa tena iliyosheheni kila aina ya BIASHARA inayofanyika duniani.

Na HAYATI MWALIMU mwenyewe amefanyika kuwa MSAADA MKUBWA kwa TAIFA LA TANZANIA 🇹🇿, ndio maana nafasi yake kama BABA WA TAIFA bado tutaendelea kuithamini na kuienzi hata kwa vizazi vitakavyokuja.

Vile vile, mbali na kuwa MSAADA MKUBWA kwa TAIFA LA TANZANIA 🇹🇿, amefanyika pia MSAADA KWA JAMII YA SERENGETI YAANI CHUI. HAYATI MWALIMU mwenyewe kwa jitihada zake mwenyewe, amewasaidia sana SERENGETI YAANI CHUI.

Hawa SERENGETI YAANI CHUI wametapakaa na kuenea dunia nzima, huku wakijihusisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi na kibiashara, na mwaka 2018, kipindi nipo UGANDA 🇺🇬 nilipata taarifa kuwa, hawa SERENGETI yaani CHUI wameshaingia mpaka nchi ya NEW ZEALAND 🇳🇿. Hii yote ni jitihada na matunda ya HAYATI MWALIMU mwenyewe.

Hawa SERENGETI yaani CHUI wapo vizuri sana, wengine tunajaribu jaribu tu, lakini ukweli ni kwamba bado muda kidogo hawa SERENGETI yaani CHUI wataanza kuonesha ile ORODHA YA SERENGETI YAANI CHUI waliohama TANZANIA 🇹🇿 na kwenda kuishi MATAIFA mengine, iwe ni kwa sababu ya kidiplomasia, kisiasa na hata kiuchumi.

Na sio vibaya, kwa sababu hata jamii nyingine zinapaswa kuiga huu mtindo wa maisha ili zipate japo hata nafasi ya kujivunia, sio kila siku malalamiko na maneno ya kashfa kwa HAYATI MWALIMU, inabidi tubadilike.

Kwa upande wa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 walishabadilika na kuanza kuchukua hatua na matunda yake tumeshayaona.

Kwahiyo inatupasa tubadilike na kuchukua yale mazuri tu kutoka kwa HAYATI MWALIMU, kama mnataka kupiga hatua ya kimaendeleo ni lazima kushikana mikono na kusaidiana kila panapokuwa na ulazima.
 
Nina miaka kadhaa sijafuatilia REBOUNDS pale NBA.
Sasa umenipatia mtihani wa kuanza kuwafuatilia na kuwatambua wale WANYAMA wetu wawili ndani ya NBA.

876e70b2226e4043528bd8ebf180d379.png

3f2897dcc14bbe90e7d0fa9bd2a8cd6d.png

MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na SERENGETI yaani CHUI ndio JAMII MBILI ZA TANZANIA 🇹🇿 ambazo zinamiliki TIMU ZA MPIRA WA KIKAPU kwenye LIGI KUU YA MPIRA WA KIKAPU yaani NBA nchini MAREKANI 🇺🇲.

Timu ya mpira wa kikapu 🏀 ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁 ni [...] na timu ya mpira wa kikapu 🏀 ambayo inamilikiwa na SERENGETI yaani CHUI ni [...].

Sasa hivi ni mapema sana kutaja timu hizo kwa sababu ya kibiashara, lakini timu hizo ni miongoni mwa timu zilizoorodhozeshwa hapo juu.

-5800031039358348641_121.jpg

Na haijaishia hapo!! Hizi JAMII MBILI ZA TANZANIA 🇹🇿 - MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na SERENGETI yaani CHUI wameanza kutilia mkazo kwenye JAMII inayowazunguka, kwa kuchukua orodha ya kila KAYA na kuwaweka kwenye malengo ya baadae.

Kwa sababu hauwezi kuwa na timu za mpira wa kikapu 🏀 kwenye LIGI KUU YA MAREKANI 🇺🇲 halafu jamii unayotoka ni MASIKINI! Sasa ndio utakuwa unafanya mambo gani hayo.. 😁😁

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wapo kwenye muendelezo wa kusaidia kila KAYA kwa kuwapatia ajira watu wao kwenye kampuni ambazo wanazimiliki wao wenyewe.

Kwa upande wa SERENGETI yaani CHUI, wao wapo vizuri zaidi kwa sababu wao ndio wenye DOLA YA TANZANIA 🇹🇿 na wao ndio wenye CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM ⚒️. Kwahiyo SERENGETI yaani CHUI wana fursa nyingi sana ukilinganisha na jamii ya MWASHITA yaani SIMBA 🦁.

Lakini mwisho wa siku, sote tutakuwa sawa. WAINGEREZA 🇬🇧 huwa wanasema hivi - At the end of the time, we will all be on the same kingship .
 
Nimepata kitu hapo mkuu.
Hiyo ndio SIASA ambayo WAINGEREZA 🇬🇧 wanaita POLITICS! Hiyo ndio SIASA ambayo WARUSI 🇷🇺 wanaita POLITIKA.

060b7ee9f921055485017bcceb8a4359.png

Halafu pia, kauli mbiu ya TP MAZEMBE huwa ni kauli mbiu ya MWASHITA yaani SIMBA 🦁 ambayo huwa inasema hivi - " Impossible n'est pas MAZEMBE".

Kwa lugha ya KIINGEREZA 🇬🇧 huwa wanasema hivi - "Nothing impossible to MAZEMBE". Na kwa lugha ya KISWAHILI 🇹🇿 huwa wanasema hivi - "Hakuna kinachoshindikana kwa MAZEMBE".

Na kauli mbiu hiyo ipo hivyo hivyo kwa upande wa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 - "Hakuna kinachoshindikana kwa MWASHITA".

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 kwa sasa hivi wapo vizuri sana KIUCHUMI na KIBIASHARA na kwa kadri siku zinavyozidi kusogea, hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 watahamia KENYA 🇰🇪 na kufanya NAIROBI kuwa ni MAKAO MAKUU YA KAMPUNI ZAO ZA KIBIASHARA.
 
Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee hapa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu Nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.

Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia baadae sana baada ya kusikia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.

kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya Kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya Nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.

Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona Kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake".
Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda Urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"

Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo Kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho Oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona.

Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio Kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere.

Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa ambaye ni co-founder wa hii nchi kwangu mimi alichangia 50% ktk kutengeneza taifa hili sawa sawa na mwalimu, yaani ni kama vile "stive wozniak na stive jobs", steve jobs alitumia akili za stive wozniak na credit akajiapa yeye mwenyewe

Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii

Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always

UPDATE:
Watu wengi kwenye comments wanasema kwamba ujamaa ulituleta karibu, lakini ujamaa huo huo ndio uliotuletea umaskini, kwa hiyo logic yake ni kwamba mwalimu alichagua umaskini na umoja dhidi ya maendeleo ambayo hatuna uhakika kama yangetugawa, lakini kabla ya yote Kambona alimshauri kwamba kabla ya ku adopt ujamaa tuufanyie kwanza majaribio , tutengeneze vijiji vichache ambavyo vitaishi kijamaa ili tuone hii system itafanya kazi lakini mwalimu alikataa akaiingiza moja kwa moja bila kujua risks zake ni nini kitu ambacho kambona alishakiona

"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
refence:

====

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!!

Christopher Makwaia

WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.10.jpeg

1. Usuli
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

2. Elimu Chini ya Mwembe
KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

3. Elimu ya "Middle School"
Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

4. Alliance Sec. School
KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

5. Tabora Boyz Sec. School
KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25281%2529.jpeg

6. Ualimu Alliance Sec. School
Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

7. KAMBONA akutana na NYERERE tena
KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

8. KAMBONA Ajiunga TANU
Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

9. KAMBONA Awaingiza TANU Watanganyika 100,000
KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.11%25282%2529.jpeg

10. KAMBONA Afungua Akaunti ya Kwanza ya TANU
KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

11. KAMBONA afuma "Governor's Scholarship" kusomea Sheria, UK
Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

12. KAMBONA Awa Mtangazaji wa 1 wa Kiswahili BBC 1957
Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

13. KAMBONA awa Mwenyekiti wa TANU London
Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.

14. KAMBONA na NYERERE Washeachumba Chuoni London
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

15. KAMBONA Amuoa MISS Tanganyika
Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.
WhatsApp%2BImage%2B2019-01-27%2Bat%2B19.28.12.jpeg

16. KAMBONA Arejea Bongo
KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

17. KAMBONA Awa Waziri wa 1 wa Mambo ya Nje
Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

18. KAMBONA Kipenzi cha 2 cha Wananchi baada ya NYERERE
KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

19. KAMBONA- Kiongozi PEKEE Aliyewakabili Waasi, 1964
Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manani hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.

Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yalizimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

20. KAMBONA Ashuhudia mchakato wa Muungano 1964
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

21. KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwaameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

22. NYERERE "Amchana" kiaina KAMBONA 77 ya 1966
Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

23. KAMBONA Ajiuzulu u-Waziri na U-Katibu Mkuu TANU 1967
Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

24. KAMBONA Atorokea Kenya, 1967 ki-James Bond !!
Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.
Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwq vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

25. NYERERE Aelezea "Kusepa" kwa KAMBONA
Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

26. KAMBONA Ajitetea UK
Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

27. OTTIN na MATTIYA KAMBONA "Wasukumiziwa Ndani",1967
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.
Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

28. KAWAWA "Amchana" KAMBONA Bungeni, 1968
Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:
"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

29. KAMBONA Amchana NYERERE nchini Nigeria, 1968
Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE na kumwita dikteta. KAMBONA akaonesha kukosa uzalendo kwa taifa lake pale alipozomoka, bila ushahidi, kwamba TZ imepeleka vifaa vya kijeshi Biafra badala ya Zimbabwe!.

30. TANU "Yamfyekelea mbali" KAMBONA
NEC ya TANU iliyokuwa ikiketi Tanga, tarehe 19.10.1968, ilimvua uanachama KAMBONA pamoja na wabunge wengine 8 "Vichwa-maji" waliohoji uhalali wa TANU kuwa juu ya Bunge. Wabunge hao ni W. Mwakitwange, M. Choga, S. Kibuga, J. Bakampenja, E. Anangisye, G. Kaneno na Dr. F. Masha.

31. NYERERE "Amchana" tena KAMBONA, 1969
Tarehe 12.1.1969 kwenye sherehe za Mapinduzi Znz, NYERERE "alimuwakia" KAMBONA na kusema- "KAMBONA ni mwizi na mhuni kisiasa.

32. KAMBONA Akejeliwa Mashuleni na Majeshini
Nyimbo nyingi za kumkejeli KAMBONA zilitungwa majeshini na mashuleni lakini zilizokuwa maarufu ni hizi 2:
1. KAOMBONA Kaolewa wapi....? Kwa Wazungu...Kisa nini?...Tamaa ya Mali!

2. Alimselema ...alija, akija KAMBONA chinja... chinjilia mbali..!!.

33. KAMBONA Adaiwa ni _"Mastermind"_wa Uhaini, 1969
Mwaka 1969, KAMBONA alidaiwa kuwa "Mastermind" wa uhaini. Mashitaka yalikuwa kwamba washtakiwa 7 wakishirikiana na KAMBONA kati ya Machi 1968 na Octoba 1969, walitaka kumuua Rais NYERERE na kuipindua serikali. Washtakiwa hao 7 ni (Bibi Titi Mohamed , Michael Kamaliza, Gray Mattaka, John na Eliya Chipaka, Capt A. Milinga na W. Chacha).

Kesi ilianza kurindima Jumatatu tarehe 6.6.1970 na ilisikilizwa na Jaji Mkuu Georges na iliendeshwa na AG Mark Bomani. Wanafunzi wa Sekondari Tambaza(F.V Arts akiwepo Othman Chande, Jaji Mkuu wa 7) walikuwa wakijongo vipindi kwenda kortin kushuhudia kesi hii iliyokuwa na mvuto wa aina yake.

Washtakiwa wote walitiwa hatiani kasoro A. Milinga na KAMBONA ambaye hakuwepo. M. Kamaliza na mwenzake walipigwa "mvua" 10 na wengine walifungwa maisha na Bibi Titi akapata msamaha 1972.

34. OTTIN MATTIYA Waachiwa 1978
Tarehe 5.2.1978, katika kusheherekea mwaka 1 wa kuzaliwa CCM, NYERERE, akitumia ibaracya 45 ya Katiba, aliwaachia huru OTTIN na MATTIYA pamoja na JOSEPH KASELABANTU( Mwasisi wa TANU).
OTTIN na MATTIYA, baada ya kugundua familia zao hazipo, wakaona Bongo hamna ishu nao wakaamua pia kusepa. Walivuka mpaka wa TZ na Kenya usiku Kininja kwani mpaka huo ulikuwa umefungwa kutokana na uhasama bainavya TZ na Kenya na wakaelekea UK.

35. NYERERE NA KAMBONA walikuwa majirani Msasani
Baada ya KAMBONA kuondoka nchini 1967, nyumba yake ikawa inakaliwa na Rais MILTON OBOTE kwa takribani miaka 10 baada ya kupinduliwa na Nduli IDD AMIN, 1971.

36. Vyama Vingi vyaanzishwa Bongo, KAMBONA ataka kurejea
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1992, KAMBONA akiwa London alisema, ije mvua, lije jua, anarejea kwenye Taifa lake. Serikali ikamuonya kuwa asithubutu na akijifanya fyatu au kichwa-maji akatia pua yake tu Bongo, "hakuna rangi ataacha kuiona".

37. KAMBONA Aitunishia msuli serikali, Atinga Bongo
KAMBONA aliamua kuwa kama "Mbwai, mbwai tu" hivyo akaonesha "Shoo za kibabe" na kurejea nchini akisafiria nyaraka za Umoja wa Mataifa zilizotolewa na serikali ya UK. Aliporejea hakukamatwa na badala yake, tarehe 4.9.1992, serikali ilimpa miezi 3 aweke sawa uraia wake kwakuwa ni Mmalawi! Miezi hiyo iliisha tarehe 4.12.1992 na serikali "ikaufyata" kwani haikumfanya kitu chochote!.

38. KAMBONA aeleza sababu za kutoroka, 1967:
Baada ya kurejea nchini, KAMBONA alikata kiu ya wote waliotaka kujua kilichopelekea asepe "Kwa Mama" ni nini ambapo alitiririka:
"Mimi na NYERERE tumetoka mbali. Sisi ndio tuliokuwa Viongozi wakuu wa TANU; Yeye Mwenyekiti, mimi Katibu Mkuu. NYERERE aliporudi toka China 1965 alitaka kuleta sera za China na mfumo wa chama kimoja. Nikapingana nae.."

39. KAMBONA Aeleza alichokuwa akifanya UK
Wiki 2 baada ya kurejea nchini, KAMBONA alitiririka kitu alichokuwa akifanya nchini Uingereza kwa miaka 25 aliyoishi huko ambapo alisema- "I did business. I used to go to the Arab countries but this did not last. I then depended on income support from Britain. Every Tuesday You take your book to the Post office...

40. KAMBONA atishia "Kumwaga ugali na mboga" kuhusu NYERERE
Badala ya kushugulikia uraia, KAMBONA akaendeleza bifu lake na NYERERE ambapo alisema anataka kufanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili aeleze ufisadi wa NYERERE. Mapadri na masheikh walimsihi sana lakini akashikilia msimamo wake.

41. KAMBONA Ambwelambwela Jangwani,1992
Tarehe 21.11.1992, viwanja vya Jangwani viliweka rekodi kutokana na umati mkubwa wa "wapenda ubuyu" uliojitokeza toka mida ya mchana kulisikia Jabali hilo litaeleza nini kuhusu Baba wa Taifa, Mwalimu NYERERERE.

KAMBONA aliwaboa sana 90% ya waliohudhuria kwani alidai, bila ushahidi, kuwa NYERERE, AMIR JAMAL na KAWAWA wameficha mamilioni ya fedha mabenki ya Ulaya. KAMBONA akaenda mbali na kudai NYERERE ni Mtutsi, KAWAWA na MKAPA ni watu wa Msumbiji na MALECELA ni Mcongoman!. Ikaonekana ni hekaya za Abunuwasi na hadithi za Esopo tu!.

42. NYERERE Amjibu KAMBONA
NYERERE, siku chache baadaye akiwa Msasani, aling'aka- "Mimi ni lofa. I dont have a single penny abroad, I can assure you. Kama RASHID na AMIR hawawekwi kundi la watu waaminifu duniani, labda neno uaminifu ni neno tu, halina maana. Hawa ni waaminifu sana. Pia, mimi sipendi kuhusishwa na mambo ya kijingajinga. Ni makosa kushindana na kundi la wapumbavu. Kambona alete ushahidi maana "any blessed fool could stand up there" na kusema chochote".

43. MAWAKILI wamchimba Mkwara-Mbuzi KAMBONA
Baada ya KAMBONA kutoa kashfa dhidi ya viongozi hao mashuhuri nchini, mawakili wa Viongozi hao walimpa siku 14 toka tarehe 8.12.1992 kuomba radhi au kutoa ushahidi.

KAMBONA aliwajibu kuwa _"Mtu mzima hatishiwi nyau"_na akachekesha watu pale alipodai _"Nondo" zake kuhusu "bank accounts" za viongozi hao amezisahau UK!.

44. KAMBONA Aunda TADEA
KAMBONA aliunda chama cha TADEA ambacho hakikuleta upinzani wowote wa maana.

45. KAMBONA afariki London, 1997
KAMBONA alifariki jijini London mwaka 1997 na mwili wake kuletwa nchini na kupokelewa na ndugu zake na kiongozi wa serikali, Mh. J.M. KIKWETE, Waziri wa Mambo ya Nje. Rafiki yake NYERERE hawakuwahi kuonana toka atoroke mwaka 1967 na wala hakwenda kwenye mazishi yake.

46. RAIS KIKWETE Akutana na Mke wa KAMBONA, 2007
Tarehe 28.6.2007 katika hotel ya Kilimanjaro Kempisk, Rais wa awamu ya nne, Mh. JK alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 50 ya BBC KISWAHILI. Mh. JK, akiwa na mcheshi na mwenye bashasha kama kawaida yake, alikutana na kusalimiana na Bi. FLORA KAMBONA ambaye alikuwa mgeni mahsusi kwani mmewe, KAMBONA ndiye aliyekuwa Mtangazaji wa 1 wa BBC Kiswahili, 1957.

46. MWISHO:
Huyu ndiye OSCAR SATIEL DAVID KAMBONA aliyekuwa chanda na pete na Mwalimu NYERERE lakini mwisho wakawa maadui wasio na mfanowe!.

Tafakuri Tunduizi:
ATIKALI HII YA KUKATA NA SHOKA ina Tafakuri Tunduizi 100!!!

OSCAR KAMBONA: KIONGOZI MAHIRI, MTANASHATI NA RAFIKI KIPENZI WA MWALIMU NYERERE ALIYEISHIA KUWA ADUI YAKE MKUBWA!!! - MICHUZI BLOG (issamichuzi.blogspot.com)

Oscar Kambona - Wikipedia
View attachment 1983785

Hizi tunaziita Wikileaks tatizo la nchi hii lilianzia hapa mtu mmoja kuhodhi mawazo ya wengi. Ujamaa umetufikisha wapi. Unaona Mwanga kidogo unaletwa na Kikwete lakini too late. Mawazo ya Kikwete ni ya kiliberali na kwa maoni yangu yanaleta afya njema kwa siasa za Tanzania. Tanzani ukibana kama unaharibu sana tena sana. Ukiruhusu mawazo mengi unavuna mengi kutoka kwao.
 
Mwashita yaani Simba

IMG_20211114_231226_9~2.jpg

Hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wao wanajivunia vitu vyao wenyewe, ndio maana wanapiga hatua siku kadri ya siku.

WAINGEREZA 🇬🇧 huwa wanasema hivi - "For a society to develop, it needs something to be proud of".

Hiyo kwenye picha ni BODY SPRAY yaani ni MARASHI yaliyotengenezwa na kampuni ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁.

Kampuni hiyo inaitwa FRESH DEODORANT na inatengeneza mpaka BODY PERFUMES ambazo wanasambaza kwa MATAIFA YA ULAYA 🇪🇺 NA AMERIKA.

Kwahiyo kama ilivyo kwa upande mwingine wa SERENGETI yaani CHUI, hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 na wao wanatumia MARASHI yao wenyewe.
 
Mwashita yaani Simba

IMG_20211116_101309_8.jpg

Hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 ndio wamiliki halali wa kampuni inayotengeneza sabuni za DALAN. Hiyo kampuni inapatikana nchini UTURUKI 🇹🇷 na wanasambaza bidhaa zao nchi zote za ULAYA 🇪🇺 na baadhi ya nchi za AFRIKA ikiwemo TANZANIA 🇹🇿 yenyewe.
 
Mwashita yaani Simba

IMG_20211117_131104_8.jpg

Hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 ndio wamiliki halali wa kampuni inayotengeneza bidhaa na sabuni za COVEX.

Hiyo kampuni inapatikana nchini UTURUKI 🇹🇷 na wanasambaza bidhaa zao nchi zote za ULAYA 🇪🇺 na baadhi ya nchi za AFRIKA ikiwemo TANZANIA 🇹🇿 yenyewe.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wamewekeza MITAJI MIKUBWA sana nje ya TANZANIA 🇹🇿 kuliko ndani ya TANZANIA 🇹🇿.

Vile vile kwa nchi ya UTURUKI 🇹🇷, hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wanamiliki timu ya mpira wa miguu ambayo inashiriki LIGI KUU YA UTURUKI 🇹🇷 na timu hiyo inafahamika kwa jina la [...]. Sio vyema kuitaja mapema timu hiyo kwa sababu za kibiashara lakini timu hiyo inafanya vizuri kwenye LIGI KUU YA UTURUKI 🇹🇷.

Pia hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 wameathirika pakubwa sana KIUCHUMI na KIBIASHARA kufuatia janga la COVID-19 lililoikumba ULAYA 🇪🇺 na DUNIA kwa ujumla pamoja na VIKWAZO VYA KIBIASHARA vilivyowekwa kwa nchi ya UTURUKI 🇹🇷 miezi kadhaa iliyopita.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA 🦁 tayari wameshaingia kwenye biashara za kimataifa yaani GLOBAL TRADE na wanatambulika moja kwa moja na JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA 🇪🇺 yaani EUROPEAN UNION.
 
nyie vilaza wawili hapo juu, acheni kusoma majarida/vijitabu vinavyozungumzia masuala ya conspiracy theories, mnapotoshana sana.

baada ya kosoma comment zenu kwenye hii thread, nimebaini nyinyi ni vipofu wawili mnaosaidiana kuvuka barabara. mnazingua.

halafu wewe charles hayo matakataka yako unayotujazia kwenye uzi huu ni bora uyapeleke facebook.jf sio mahala pake.
 
Hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] ndio wamiliki halali wa kampuni inayotengeneza bidhaa na sabuni za COVEX.

Hiyo kampuni inapatikana nchini UTURUKI [emoji1250] na wanasambaza bidhaa zao nchi zote za ULAYA [emoji1099] na baadhi ya nchi za AFRIKA ikiwemo TANZANIA [emoji1241] yenyewe.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] wamewekeza MITAJI MIKUBWA sana nje ya TANZANIA [emoji1241] kuliko ndani ya TANZANIA [emoji1241].

Vile vile kwa nchi ya UTURUKI [emoji1250], hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] wanamiliki timu ya mpira wa miguu ambayo inashiriki LIGI KUU YA UTURUKI [emoji1250] na timu hiyo inafahamika kwa jina la [...]. Sio vyema kuitaja mapema timu hiyo kwa sababu za kibiashara lakini timu hiyo inafanya vizuri kwenye LIGI KUU YA UTURUKI [emoji1250].

Pia hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] wameathirika pakubwa sana KIUCHUMI na KIBIASHARA kufuatia janga la COVID-19 lililoikumba ULAYA [emoji1099] na DUNIA kwa ujumla pamoja na VIKWAZO VYA KIBIASHARA vilivyowekwa kwa nchi ya UTURUKI [emoji1250] miezi kadhaa iliyopita.

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] tayari wameshaingia kwenye biashara za kimataifa yaani GLOBAL TRADE na wanatambulika moja kwa moja na JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA [emoji1099] yaani EUROPEAN UNION.
.
giphy.gif
 
MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] na SERENGETI yaani CHUI ndio JAMII MBILI ZA TANZANIA [emoji1241] ambazo zinamiliki TIMU ZA MPIRA WA KIKAPU kwenye LIGI KUU YA MPIRA WA KIKAPU yaani NBA nchini MAREKANI [emoji1258].

Timu ya mpira wa kikapu [emoji459] ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] ni [...] na timu ya mpira wa kikapu [emoji459] ambayo inamilikiwa na SERENGETI yaani CHUI ni [...].

Sasa hivi ni mapema sana kutaja timu hizo kwa sababu ya kibiashara, lakini timu hizo ni miongoni mwa timu zilizoorodhozeshwa hapo juu.

Na haijaishia hapo!! Hizi JAMII MBILI ZA TANZANIA [emoji1241] - MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] na SERENGETI yaani CHUI wameanza kutilia mkazo kwenye JAMII inayowazunguka, kwa kuchukua orodha ya kila KAYA na kuwaweka kwenye malengo ya baadae.

Kwa sababu hauwezi kuwa na timu za mpira wa kikapu [emoji459] kwenye LIGI KUU YA MAREKANI [emoji1258] halafu jamii unayotoka ni MASIKINI! Sasa ndio utakuwa unafanya mambo gani hayo.. [emoji16][emoji16]

Kwahiyo hawa MWASHITA yaani SIMBA [emoji881] wapo kwenye muendelezo wa kusaidia kila KAYA kwa kuwapatia ajira watu wao kwenye kampuni ambazo wanazimiliki wao wenyewe.

Kwa upande wa SERENGETI yaani CHUI, wao wapo vizuri zaidi kwa sababu wao ndio wenye DOLA YA TANZANIA [emoji1241] na wao ndio wenye CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM [emoji3537]. Kwahiyo SERENGETI yaani CHUI wana fursa nyingi sana ukilinganisha na jamii ya MWASHITA yaani SIMBA [emoji881].

Lakini mwisho wa siku, sote tutakuwa sawa. WAINGEREZA [emoji636] huwa wanasema hivi - At the end of the time, we will all be on the same kingship .
.
giphy.gif
 
nyie vilaza wawili hapo juu, acheni kusoma majarida/vijitabu vinavyozungumzia masuala ya conspiracy theories, mnapotoshana sana.

baada ya kosoma comment zenu kwenye hii thread, nimebaini nyinyi ni vipofu wawili mnaosaidiana kuvuka barabara. mnazingua.

halafu wewe charles hayo matakataka yako unayotujazia kwenye uzi huu ni bora uyapeleke facebook.jf sio mahala pake.
WATU wengi huwa wanapotoshana, lakini huo ndio UKWELI HALISI 🙏🏽
 
Sasa ukitaka kufahamu timu ya mpira wa kikapu 🏀 ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁, angalia vizuri hiyo VIDEO hapo juu.

Hiyo VIDEO ni REMIX ya nyimbo ya WIZ KHALIFA inayokwenda kwa jina la BLACK AND YELLOW.

Sasa kwenye hiyo VIDEO, kuna sehemu WIZ KHALIFA ameonekana amevaa BOSHORI NYEUSI yenye NEMBO au LOGO yenye RANGI NYEKUNDU.

Hiyo NEMBO au LOGO yenye RANGI NYEKUNDU inawakilisha timu ya mpira wa kikapu 🏀 ambayo inakwenda kwa jina la [...]. Hiyo ndio timu ya mpira wa kikapu 🏀 ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁.

Na kwa upande wa SERENGETI yaani CHUI na wao huwa wanafanya hivyo hivyo, na wao pia wana WASANII wao sehemu mbali mbali duniani ukijumuisha na HOLLYWOOD 🎬.

Na mara nyingi WASANII huwa wanatumika kufikisha ujumbe kwa njia ya TUNGO yaani MASHAIRI au kwa njia ya VIDEO yaani PICHA.

Sasa angalia hiyo VIDEO vizuri ndio utaweza kutambua kile ninachokueleza, kama kweli wewe ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu 🏀 yaani NBA, utaifahamu hiyo timu ambayo inamilikiwa na MWASHITA yaani SIMBA 🦁.
 
no no no...siangalii ujinga.
giphy.gif
Sasa kufuatia hii COMMENT yako, utakuwa umeelewa ni timu gani ambayo inamilikiwa na SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 kwenye matokeo ya mechi za UEFA CHAMPIONS LEAGUE ⚽ zilizoorodhozeshwa kwenye posti namba 706.
 
Back
Top Bottom