Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

yaani vingine vinajengwa njia hazina magari kuna bodaboda tu. au ndiyo mifumo ya kutakatisha pesa chafu
 
Kwani kuna tatizo gani vikiota kama uyoga?

Kwani umeona ni vituo vya mafuta tuu? Takribani kila kitu kuanzia magorofa hadi uwekezaji wa biashara..

Hiyo ni ishara uchumi unakua,watu wnanunua magari ,wanajenga nk ndio maana huwezi sikia maduka yakifungwa..
 
Je, ni kweli sheria inataka umbali uwe mita 500..?
Sijawahi kuisikia au imefutwa,vituo vingi vinarahisisha shughuli za usafiri hakuna tena haja ya kujaza fulu tanki na yale mambo ya zamani ya kuhangaika usiku kutafuta vituo sasa hivi vituo vingi ni 24hrs wafanyakazi ni shifti mbili hadi tatu.

Siasa za majungu na kijipendekeza zilienda na Mwendozake.
 
Swali moja kuu je kodi inalipwa TRA kama inavyotakiwa. ??
 
Watu wana vibali vya ujenzi halafu unaita holela?
 
yaani vingine vinajengwa njia hazina magari kuna bodaboda tu. au ndiyo mifumo ya kutakatisha pesa chafu
Yaa naona ka utakatishaji kameanza kurudi kwa kasi kutokana na walamba asali kupewa rungu.
 
Eti Tanzania iliyokuwa inameremeta!Hivi huu ujinga mnautoaga wapi??Hivyo viwanda vyenu viko wapi?Kweli viwanda kama vilikuwepo vinaweza kufilisika kwa muda wa miaka miwili kama vilikuwa vinajiendesha kwa njia halali?
 
Haya mamilioni ya Bodaboda lazima yagemwe.😁

Watu wenye mawazo ya Kikomunisti tupa kule.
 
nadhani ni nchi ya tozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…