Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

Bila shaka sasa Tanzania mpya iliyokuwa inameremeta kwa ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, sasa imegeuka kuwa Tanzania ya ujenzi wa vituo vya mafuta kiholela na kila sehemu!

Sheria inataka ujenzi wa kituo cha mafuta uwe mita 500 kutoka kimoja hadi kingine lakini sheria hii haifuatwi tena. Kuanzia mwaka 2021 vituo vya mafuta vinaota kama uyoga kwenye nchi yetu. Swali la kujiuliza kimetokea nini?

Mkoa wa Pwani ulikuwa unaongoza kwa ujenzi wa viwanda vingi sana lakini sasa hivi wakifanya utafiti upya watakuta unaongoza kwa ujenzi holela wa vituo vya mafuta.
Wewe hata kiwanda cha tofali huna unataka wenzio ndio wajenge viwanda? Nenda katuonyeshe mfano kwa kujenga cha kwako badala ya kubwabwaja nyuma ya keyboard
 
Acha kubwabwaja, kama unao ushahidi weka hapa.
It is an open secret mkuu.

Watu wanafahamu kinachoendelea bandarini ila hakuna tu mwenye guts za kuyaweka hadharani.

Unafanyika ukwepaji mkubwa wa kodi hapo bandarini na watu wanakaa kimya kwa sababu mbali mbali.

Hao wezi ndio tunaowaita matajiri na wafadhili wetu.
 
Unafanyika ukwepaji mkubwa wa kodi hapo bandarini na watu wanakaa kimya kwa sababu mbali mbali.
Jf iko kwa ajili ya Whistle blowers, kwa nini unashindwa kufanya hivyo badala yake unashutumu vitu ambavyo huna uwelewa navyo?
 
Acheni watu wajenge vituo kuna mda tz tunaweka sheria za ajabu, kama zile kuwe kuna umbali wa hospital ya serikali na duka la madawa
 
Jf iko kwa ajili ya Whistle blowers, kwa nini unashindwa kufanya hivyo badala yake unashutumu vitu ambavyo huna uwelewa navyo?
Unacholalamika hapa wewe ni nini??

Sina ninachoelewa au nini??

Maana kwa kuandika tu ina maana nafahamu uwepo wa hilo jambo.

Kama unalalamikia kuwa sifahamu jambo naloandika basi unakosea mkuu.

Nafahamu kabisa nachoandika na wala hata hakuna haja ya kuhitaji ushahidi kila mtu hapo bandarini na wasio bandarini wanajua kinachoendelea labda wewe tu.
 
Tatizo utaliona siku kituo kimojwapo kitakapowageuza halaiki ya watu wenye makazi jirani kuwa mishikaki.
Sioni tatizo,wewe jali kulisha familia yako.

Hizo ni ajira.
 
Hao wanaume wakajenge vituo mbali na makazi ya watu wanapoishi
Wanaume wanajenga vituo vya mafuta wewe unalalama, hivyo viwanda kajenge wewe kuna mtu kakukataza?
 
Tanzania watu wengi Wana mitaji lakini ubunifu ZIRO kabisa...... biashara zinafanywa kwa fasheni na mihemko.......mtu yoyote tu akibuni biashara na kuonekana inalipa kila mtu anaanza kuiga.....ndio maana ulaya wameweka sheria ya haki miliki....ili kila avune matunda ya ubunifu wake na wengine waumize vichwa
Ni Tanzania pekee
Wenye hela hawana wazo na muda, mwenye muda hana wazo wala hela, mwenye wazo hana hela wala muda 😂😂😂😂

Kwa hiyo wenye mitaji wanaigizana tu. 😂😂😂😂

Hatimaye biashara zinakuwa nyingi kuliko wateja. Hapo kinachofuata ni hujuma, migogoro na fitina 😂😂😂😂
 
Kama sikosei sheria inasema ni mita 200 toka MAKAZI ya watu,na sio kituo hadi kituo
 
Tanzania watu wengi Wana mitaji lakini ubunifu ZIRO kabisa...... biashara zinafanywa kwa fasheni na mihemko.......mtu yoyote tu akibuni biashara na kuonekana inalipa kila mtu anaanza kuiga.....ndio maana ulaya wameweka sheria ya haki miliki....ili kila avune matunda ya ubunifu wake na wengine waumize vichwa
Kweli kabisa
 
Tatizo utaliona siku kituo kimojwapo kitakapowageuza halaiki ya watu wenye makazi jirani kuwa mishikaki.
Mimi naendesha Tenka la Petroli kwa muda mrefu sasa sijawahi kugeuka Mshkaki, kazi ni kazi ndugu.
 
Mlalakuwa opp na jkt kuna sheli
Maringo pale sheli
Studio sheli,
Kuelekea moroco kuna vituo 2 kabla ya kukutana total
Pita njia ya tandale,goba mwendo wa vituo vya mafuta
Sahvi ukiwekeza kwenye kituo cha mafuta hujakosea

Ova
 
Njia ya tandale ukipita unaweza ukajiuliza huu ni wazim au nini yaani chocholo nayo inajengwa sheli😁😁
 
Back
Top Bottom