Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

Tanzania ya viwanda yageuka kuwa Tanzania ya vituo vya mafuta

Kama vile umeona mji ninaoishi ukitoka nyumbani Hadi ufike sokon mjini sehem ya nusu saa unazipita sheli za mafuta 7 zipo kwenye makazi ya watu zimekaribiana hua nawaza siku moja ikilipuka sijui itakuaje.
Vituo havilipuki kirahisi hivyo
 
Tanzania tuna changamoto sana kwenye suala la kuamua innovative and sustainable development goals, ndio maana kila mtu akijenga nyumba anafikiria kutengeneza frame mbele ya nyumba, the same hata watu wenye pesa kadhaa siku hizi wanadhani ukiwa na millioni 200 the only thing to do ni kuweka vituo vya mafuta wakati the fact is in next 20 to 30 years, matumizi ya mafuta na fossils fuel yatapungua sana hasa kwenye kuendeshea mitambo na engine.

Pia ndio maana serikali bado inaweka tozo na kodi kwenye miamala ya simu na benki alafu mwisho wa mwezi waaanza kukimbizana na watu kuhusu kodi, endapo watu wengi wangekuwa wanalipia kwa njia za mitandao ingewasaidia wao kwenye kujua na pesa kiasi ngapi ambazo watu wana trade tena kwa taarifa sahihi kabisa.
Una point kubwa sana, ila kwa upande mwingine kibiashara anaweza kuwa anajua usemacho ila baada ya hio miaka 20/30 atakuwa kashantengeneza pesa ya kutosha na hali ikilazimisha atahamia huko kwenye nishati mpya.
 
Vituo vya mafuta mpaka njia ya kuelekea msakuzi,Acha watu wafanye tu

Ova
 
Hayo ndio mafisadi yenyewe mkuu yanayotufanya tuhenyeshwe na tozo.

Yenyewe hayalipi kodi tunabanwa sisi vidagaa.
 
500m = urefu viwanja 5 vya mpira. Shida iko wapi sasa

Bila shaka sasa Tanzania mpya iliyokuwa inameremeta kwa ujenzi wa viwanda kila kona ya nchi, sasa imegeuka kuwa Tanzania ya ujenzi wa vituo vya mafuta kiholela na kila sehemu!

Sheria inataka ujenzi wa kituo cha mafuta uwe mita 500 kutoka kimoja hadi kingine lakini sheria hii haifuatwi tena. Kuanzia mwaka 2021 vituo vya mafuta vinaota kama uyoga kwenye nchi yetu. Swali la kujiuliza kimetokea nini?

Mkoa wa Pwani ulikuwa unaongoza kwa ujenzi wa viwanda vingi sana lakini sasa hivi wakifanya utafiti upya watakuta unaongoza kwa ujenzi holela wa vituo vya mafuta.
 
Hayo ndio mafisadi yenyewe mkuu yanayotufanya tuhenyeshwe na tozo.

Yenyewe hayalipi kodi tunabanwa sisi vidagaa.
Utalia sana, utalalamika sana, si ndio chama chako kinayabariki
 
Tanzania watu wengi Wana mitaji lakini ubunifu ZIRO kabisa...... biashara zinafanywa kwa fasheni na mihemko.......mtu yoyote tu akibuni biashara na kuonekana inalipa kila mtu anaanza kuiga.....ndio maana ulaya wameweka sheria ya haki miliki....ili kila avune matunda ya ubunifu wake na wengine waumize vichwa
 
Back
Top Bottom