Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Bado tunapariwa kwanza. Tunatayarishiwa kikaango
 
Tupo katika "One man show" hamuoni tenda na mkandarasi anatoa yeye,na alipa yeye
 
Yawezekana hiyo hop ilikuwa inahatarisha usalama wa nchi. kwa vyovyote kutakuwa na sababu ya msingi kuwajua hivyo kama Tetesi hizi ni za kweli.
 
Kudhibiti Maandamano

Si umeona Leo Tundu Lissu na Hellen Kijo kisimba wameandamana wakiwa wameshika Mabango ndani ya Fence ya LHRC ingekuwa zamani ingekuwa Vurugu Mji Mzima

Maandamano yalianzia ndani ya Fence na yakaishia ndani ya Fence hiyo hiyo
haha hatari mnoo
 
Kuna wakati nikisoma coment za wadau hasa wale wanao support vitu ambavyo kwa akili ya kawaida unaona kabisa hapa serikali inakosea. Huwa nawaonaga hawana akili nahisi kwenye ubongo kumejaa hewa tu.
 
Maswali ya usaili jana TRA yamenilazimisha nisome huu uzi. Vinginevyo ningeupita hivi niende zangu MMU.
 
It was a just matter of time only! serikali haiwezi kufanya haya yanayoendelea na bado ukabaki kwenye mikataba na itifaki za kimataifa, utakuwa uzuzu na unafiki wa kiwango cha uzamivu!
 
Serikali ya Tanzania inadaiwa kujitoa kwa muda kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji yaani Open Goverment Partnership(OGP). Inadaiwa Serikali imeamua kujikita kwenye "kutumbua majipu" kwanza kabla ya kujikita kwenye uwazi.

OGP ilianzishwa mwaka 2011 na ilianza na Serikali 8 hadi 70 na Tanzania ilijiunga 2011 na kutekeleza mipango kazi ya kitaifa 3 hadi sasa (3 National Action Plans).

Ahadi 7 zilizokuwa kwenye Mpango Kazi wa 3 wa Kitaifa wa OGP ni

i) Kutungwa kwa Sheria ya Upatikanaji wa Habari(Access to Information Act)

ii) Bajeti kuwa wazi(Open Budgets)

iii) Taarifa mbalimbali za Serikali kuwa wazi(Open Data)

iv) Uwazi wa masuala ya ardhi ikiwemo taarifa za umiliki wa Ardhi nchi nzima kuweza kupatikana mtandaoni(Land Transparency)

v) Uwazi katika Sekta ya Madini

Ahadi za Nyongeza
(vi) Uwazi katika Sekta ya Afya kwa ujumla(Medical and Health Service Transparency)

(vii) Kuwepo kwa mifumo ya utendaji kazi wa Serikali iliyo wazi kabisa (Performance Management Systems)


Anaandika Mbunge wa Kigoma Ujiji, Zitto Kabwe:

Nimeshangazwa na uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP. Hivyo nimeamua kuwasilisha swali Bungeni kutaka maelezo ya Serikali, inayojipambanua kwa kupambana dhidi 11 ufisadi, kujiondoa kwenye jukwaa la Kimataifa linalopigania Serikali kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji.

Uwazi ( Transparency/Openness ) ni silaha muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na katika kuwezesha ufanisi Serikalini.

Licha ya kwamba Tanzania ilikuwa haitimizi ahadi zote kwenye Action Plans, lakini kulikuwa na msingi kwamba Nchi yetu inaamini katika Uwazi na Uwajibikaji. Uamuzi wa Serikali kujiondoa OGP unarudisha nchi yetu nyuma. Ni uamuzi ambao haukufikiriwa Sawa sawa.

Kujua Zaidi kuhusu OGP:

Msafara wa Kikwete Brazil Kwenye Mkutano wa OGP

OGP announces 15 subnational govt that will be part of a pilot program, Kigoma Tanzania one of them

Mpango Kazi wa Kitaifa wa kuendesha shughuli za Serikali kwa Uwazi Awamu ya Tatu (OGP NAP III)
Porojo tu,mbona kulikuwa hakuna uwazi wa mikataba hata wabunge hawajui undani hadi baadhi ya mawaziri hawajui.
Uwazi kwao ilikuwa one sided like a panga.
 
Back
Top Bottom