Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Tanzania yajiondoa kwenye Mkakati wa Uwazi, Ushiriki na Uwajibikaji(OGP)

Serikal inaendeshwa kwa kodi zetu wananchi, hivi fisiem mnataka kutuficha nin?

IQ ya pombe ni mzigo kwa kila Mtanzania, binafsi nmeshindwa kuubeba kitaambo!
 
nadhani hili ndio lile alilooteshwa GENT, maana nshapata mshtuko hapa ngoja niwahi hospitali nahisi pressure,

aiseee tumekwisha..!!! [emoji22]
 
bunge uchwara lipo tu, wakati lenyewe ndilo lililoridhia itifaki hiyo. huu ni upumbavu Wa binge, udhaifu Wa spika na ujinga Wa ccm.
 
Magufuli ni raisi aliyefeli vibaya sana hana jipya anapaswa kuongozwa sio kiongozi.
 
Mungu yupo!
Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
Don`t be rash with your mouth, and don`t let your heart be hasty to utter anything before God; for God is in heaven, and you on earth. Therefore let your words be few.
 
Serikali imejitoa katika Mpango wa uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) hatua ambayo inazua wasiwasi kuhusu utekelezaji wa sera ya uwazi iliyoasisiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Kulingana na Gazeti la Mwananchi la kila siku, hatua hiyo ya kujitoa kwa Tanzania ilitarajiwa kutangazwa wakati wowote na Kamati ya Uongozi ya mpango huo inayokutana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea New York, Marekani.

Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2011 na hivyo kuwa nchi ya pili barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini ambayo ilikuwa ya kwanza kusaini makubaliano hayo yanayotaka nchi kuondokana na kasumba ya kuendesha mambo kwa usiri kati yake na wananchi.

Zaidi ya nchi 70 duniani zimesaini mpango huo unaohimiza dhana ya uwazi na ukweli.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa mstari wa mbele kuunga mkono mpango huo na alifanikisha mkutano wake uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini 2015 ikiwa miezi michache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.

Wakuu wa mpango huo wanakutana New York nchini Marekani wakijadiliana mambo mbalimbali ikiwamo ajenda inayoangazia kuongezeka kwa hali ya kutoaminiana kati ya Serikali na wafanyabiashara.

Pia, wanaangalia njia zinazopaswa kuchukuliwa ili pande hizo ziweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania bado haijaweka hadharani juu ya hatua yake iliyochukua ya kujitoa kwenye mpango huo. Pia, haikuweza kufahamika mara moja kama maofisa wake walioko mjini New York watapeleka ujumbe uliochukuliwa nyumbani na Serikali.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Augustine Mahiga yuko New York akimwakilisha Rais John Magufuli mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Alipoulizwa kuhusiana na hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alikataa kueleza lolote lakini akasema kuwa Serikali itatoa ufafanuzi wake muda utakapowadia.

“Nisikilize, sisi (Serikali) tutalieleza hilo tutakapoona inafaa,” alisema Waziri Kairuki ambaye hakukanusha wala kukiri lolote.

Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Aziz Mlima alikiri kuhusu Tanzania kujiondoa katika mpango huo.

“ Ndiyo ni kweli lakini ni kwa muda tu kwa sababu Serikali inataka kuutathmini mpango huo kama unaendana na masilahi ya Taifa,” alisema.

“ Kuna mambo tunahitaji kwanza kuyatekeleza kabla ya kutekeleza mpango huu,” alisema.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi utawala wa Rais Magufuli unapenda kujikita zaidi katika utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora barani Afrika (APRM).

Kabla ya kujitoa katika mpango huo wa OGP, Tanzania ilikuwa tayari imepitia hatua mbili za utekelezaji na sasa ilikuwa ikijiandaa kutekeleza mpango mkakati wa tatu uliokuwa uanze 2016/17-2017/18.

Katika mipango hiyo, Tanzania ilikuwa imeainisha maeneo saba ya kuweka mkazo ikiwamo Sheria ya Kupata Habari, Bajeti ya Uwazi, Uwazi katika ardhi na madini.

Akizungumzia mpango huo mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Faraja Kristomus alisema wengi waliitazama OGP kama mpango wa nje zaidi na kukosa uungwaji mkono katika taasisi za kiserikali.

Katika makala zake zilizochapishwa na gazeti la Citizen, Kristomus ameandika kuwa wizara iliutazama mpango huo kama chombo chenye urasimu na haukusaidia kukaribisha mageuzi.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hatua ya Tanzania kujiondoa katika mpango huo ni ishara nyingine ya kuanguka kwa demokrasia na uwazi serikalini.

“Kitendo cha kujiondoa ni kuiambia dunia kuwa hatuko tayari kwa uwazi,” alisema.

" Swali la Kizushi: WATU WASIO JULIKANA NI WALE WATU WALIOKUJA KUTOKA ILE NCHI JIRANI KUFANYA ILE SHUGULI?"
 
Methinks mpango wa OGP ni mshale wa nyongeza katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi, sawa na vyombo huru vya habari, uhuru wa maoni na uwazi katika masuala yote yanayohusu umma. OGP haiwezi kuathiri mapambano dhidi ya maovu yoyote. Tukubali tu kwamba tumepata uongozi wenye upungufu na mamlaka zimeona njia pekee ya kuuhami na kuusaidia ni hii ya kurudi kwenye 'dark ages'. Swali, je haya yote yana baraka za ccm inayodai inaongoza nchi? I doubt.
Kuna mfano halisi hata mmoja wa mafanikio ya ogp? Kama hakuna kaa kimya!
 
Mbaguzi kaburu mweusi na chuki zake za kutisha. Hataki maovu yake dhidi ya raia wasio na hatia yajulikane. Udikteta uchwara anataka kuuficha usitoke nje ya nchi.

Hivi kuna watu mpaka sas hivi wanamshangaa huyu jamaa na uendeshaji wake wa nchi.....mie niliacha hadi kumfwatilia kwa tumuache amalize tu mda wake aende nae kuchunga mifugo kwao ndo turudi hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hofu na taharuki kubwa zimetanda nchini dikteta uchwara anafanya kila awezalo kuficha maovu yake. Serikali ndani ya giza nene.

Magumu ya kuendeshea serikali gizani?
 
Hofu na taharuki kubwa zimetanda nchini dikteta uchwara anafanya kila awezalo kuficha maovu yake. Serikali ndani ya giza nene.
Siku unaamuka wenzako tunamalizia ujenzi wa airport. Achia mbali panga boy kuongezeka. Kaa hapo hapo. Wajanja tumeujua uzuri uzuri wa Kazi za Magu.
 
Natamani kujua kikao kilichofikia maamuzi haya kilikaa lini na wapi na nani aliyekuwa kinara katika kufikia maamuzi haya ya kidikteta.

Ulivyo vya ajabu kesho raisi akikana hii habari na wewe unageuka upande uleule aliopo raisi duh vituko kwa kweli
 
Back
Top Bottom