Hawa ndio zao, inabidi kuishi nao jinsi walivyo. Huwa wanabishia kila kitu kwa kiburi halafu bila aibu wanakifuata baadaye. Angalia historia yao, yaani hamna kitu kibaya kama maskini mwenye kiburi.
Wachukulie kama jinsi uwe na kaka mkubwa wako kijijini, hajabahatika kutoka ili aone mataa ya mjini, siku zote yupo huko huko halafu umemshinda kielimu na kiuchumi, sasa unakuta anabishia kila pendekezo lako bila hata kulitafakari, kusudi aonekane mbabe.
Inabidi kwendana naye japo kwa kutumia akili nyingi, unamletea pendekezo kiujanja janja ukitegemea lazima atalipiga chini, lakini unaiweka kwa jinsi yenye hatimaye atafuata.
Wapo slow sana kwenye kuelewa chochote, inachukua nguvu nyingi sana kuwaelimisha kwa kila pendekezo. Lakini kwa vile ni ndugu na majirani, tumeunganishwa kwenye kiuno, hamna jinsi ila kuishi nao hivyo.