PostGE2025 Tanzania yakubali Masharti ya Commonwealth kuleta Wachunguzi Huru wa Matukio ya Uchaguzi 2025

PostGE2025 Tanzania yakubali Masharti ya Commonwealth kuleta Wachunguzi Huru wa Matukio ya Uchaguzi 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ikumbukwe awali serikali ya Tanzania ilikataa kuupokea ujumbe wa Chakwera.

View attachment 3554737

Masharti waliyopewa na Mkutano wa Commonwealth uliopita 71, Dec 5, 2025.
============

Mkutano wa CMAG 71 uliamua kwamba Tanzania iingizwe kwenye Ajenda Rasmi ya CMAG kwa mkutano ujao mwezi Machi 2026, ili CMAG ichukue uamuzi kuhusu Tanzania. Uamuzi wa CMAG utategemea kutimizwa kwa masharti yafuatayo:

a. Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe upatikanaji kamili na huru kwa wadau wote muhimu haraka iwezekanavyo;

b. Kufutwa kwa vikwazo dhidi ya uhuru wa mikutano na maoni, asasi za kiraia, na vyombo vya habari;

c. Kufanyika kwa jukwaa la ushauri kati ya vyama vya siasa ili kukubaliana juu ya mfumo wa pamoja wa kuelekea uchaguzi ujao; na

d. Kutekelezwa kwa taratibu za kisheria na kiutawala zilizo wazi za kuwajibisha wahusika wa vurugu na matokeo yake na kutoa fidia kwa waathirika, pale inapofaa.
Baada ya kuharibu ushahidi ndio wamekubali?
 
Ataahirisha tena kutangaza ripoti ya tume yake ya matapeli

Vinginevyo itaanikwa wazi kwamba majaji wa tume wameandika madudu na uongo mtupu
 
Nimeelewa Palamagamba Kabudi tu, na hio maana hawezi kufanya mnavyotaka nyinyi, ushaelewa?
Labda Kiingereza ni tatizo. Tanzania iligoma kuwapa free access na kusema wameunda tume yao. Jana ilikuwa commonwealth wafanya maamuzi yao.
Kabudi kaenda ma kukubali yote ambayo December waliyakataa.
Sasa tume ya commonwealth itaingia ikiwa na Uhuru wote.
 
“… CMAG welcome Tanzania’s commitment to receive and facilitate the visit….looks forward to a robust assessment…on issues raised by CMAG”.
Hayo masharti ni yapi?
kuleta wachunguzi huru… hiyo sentensi haimo kama heading inavyosema.
Rudi kwenye azimio lao la December 2025 utakipata hicho unachokisema.
Toka December Tanzania walikuwa wanagoma na sasa wameachia. Tanzania wamekubali azimio la Commonwealth la December 2025.

Masharti ni haya hapa


a. Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe upatikanaji kamili na huru kwa wadau wote muhimu haraka iwezekanavyo;

b. Kufutwa kwa vikwazo dhidi ya uhuru wa mikutano na maoni, asasi za kiraia, na vyombo vya habari;

c. Kufanyika kwa jukwaa la ushauri kati ya vyama vya siasa ili kukubaliana juu ya mfumo wa pamoja wa kuelekea uchaguzi ujao; na

d. Kutekelezwa kwa taratibu za kisheria na kiutawala zilizo wazi za kuwajibisha wahusika wa vurugu na matokeo yake na kutoa fidia kwa waathirika, pale inapofaa.
 
Wewe unajua mpaka nafika kuuliza unajua kilichoandikwa mimi sio fala umeelewa mkuu angalia vizuri kilichoandikwa hapo au unataka nikutafasirie sio kila kitu mnachekelea sasa mjumbe kuja kukutembelea eeh haya akishakutembelea wewe unapata nini si wanaongea na waliofanya ya kufanya kwani wanaongea na wewe? Hivi vitu vingine sio vya kuvichekelea
Shida yako hujaelewa Azimio lao la December 2025 linasema nini. Lisome hilo ndio utajua wanakuja kufanya nini.
Kilichoamuliwa jana ni kutekeleza azimio la 71 ambalo lilitolewa December 2025. Wewe umesoma tu Azimio la 72 bila kufanya reference ya azimio la 71.
 
Nyalandu kweli umri umeenda , mpaka umeamua kupaka kiwi 😂.

Mzee wa logistically
 
TOKA MAKTABA
February 2026
TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025,
1773048601600.jpeg

DAR ES SAALAM: TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 17, 2026 imekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo

Mkutano huo wa Tume na Waziri Kombo umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.

1773048811884.jpeg

Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na kimataifa

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.
1773048724545.jpeg
 
10 March 2026
Chief Yemba mwanasiasa mkongwe atoa angalizi

View: https://m.youtube.com/watch?v=G5WWi92AIME
Aonya chama cha CHADEMA kubanwa , Kwa kuwa sasa kuna Movement kubwa isiyo fuata chama chochote lakini wote wanaikubali CHADEMA kutokana na CHADEMA inaonekana inasimamia maslahi ya waTanzania wote. Aikataa Jumuiya ya Madola ..

Source : SAUT DIGITAL
 
Back
Top Bottom