Tanzania yakubali ombi la Kenya kuwapatia madaktari 500

Samahani sikuweka link, anyway hii hapa http://sikika.or.tz/wp-content/uploads/2013/11/Practice-Status-of-Medical-Graduates-FINAL.pdf
 
Ndg yangu kuongeza ufanisi si kutoza watu au bima au kujenga mortuary

Kuongeza ufanisi katika sekta ya afya ni kupunguza mzigo 'burden' kwa serikali

Sekta ya afya haiingizi na haitaweza kuingiza mapato kama bandari, elewa hilo

Sekta ya afya ni ya kutoa huduma. Hata hivyo, ina mchango mkubwa katika mapato

1. Ukidhibiti maradhi kama communicable diseases unapunguza gharama za uendeshaji wa hospitali na hapo umepunguza mzigo wa serikali na kuelekeza resource kwingine
2. Ukipunguza maradhi, unaongeza productivity kwa wananchi

Kuna njia mbili au tatu, kwanza, prevention, na pili curative.
Yote mawili yanategemea utaalam wa afya ambao ni madaktari na wengine.

Utashangaa nikikuambia kuwa gharama zinazotokana na matibabu ya communicable diseases ni kubwa sana na kimahesabu ukidhibiti hayo, unaweza kununua Dreamliner zako kila mwezi.

Elewa 'qualitative and quantitative analysis' ya healthcare huwezi kui scale na dreamliner, never! Huwezi kupata matokeo ya healthcare kirahisi kama dreamliner kwasababu ni kitu complicated na pengine ndio maana unadhani ni suala la kujenga mortuary nyingi za kuhifadhi maiti na kununua bima!

JokaKuu
 
Hehehe Wanyuturu nawavulia kofia, raha sana. Vipi unapafahamu Singidani, au unafahamu namfua.
Mboyane!!!

Kama kote umefia huko inabidi tungufunge ' speed governor'.

Majukumu ya kujikinga na magonjwa ni ya watu wenyewe. Kama unavyotaka afya iwe kipaumbele kwa serikali, pia iwe kipaumbele kwa wananchi.

Shirika la ndege lenye nguvu litaleta mapato ambayo yatasaidia hata kwenye afya. Ni utoto kutumia mapato yetu yote kwenye mambo ambayo hayazalishi kwa namna yoyote.
 
ndiyo maana nimkuambia kuna kitu huelewi na huonekani kama unataka kujifunza.

Healthcare popote duniani si suala la mwananchi, linafika kwa mwananchi kama hatua ya mwisho. Jiulize kwanini tuna TFDA, Mkemia Mkuu, Bohari ya Madawa, Hospitali za rufaa, vyuo vya afya n.k.

Healthcare kama ungefuatilia ni tatizo kubwa sana US kwasasa.
UK kupitia NHS wanahangaika kama mataifa mengine.

Wewe unafikiri dreamliner tu, my foot. Kwakweli siwezi kuendelea mjadala na wewe
Kiwango chako cha dreamliner ni cha hali ya juu sana, sijafikia huko

Ahsante sana
 
Bora umemaliza mjadala, kinachofuata subiri Mbowe akwambie ufanye nini halafu urudi tena.
 
Duh hapana, mbaki naye huyo huko huko kwenu. Nimeona sakata la Makonda kuvamia kituo cha habari akiwa na mapolisi halafu Magu akamkingia kifua, mambo kama hayo yabaki huko.
Hahahaha story ya marafiki hiyo! Na walio comment ni watu wako! Hapo sasa!
 
Duh hapana, mbaki naye huyo huko huko kwenu. Nimeona sakata la Makonda kuvamia kituo cha habari akiwa na mapolisi halafu Magu akamkingia kifua, mambo kama hayo yabaki huko.

 

Hehehe!! Huyo mama alikua amekasirika baada ya wana habari kuandika mambo yasiyo na kuaibisha familia yake. Simtetei au kusema alichokifanya ni sahihi lakini kawaida protests dhidi ya wana habari hutendeka mara nyingi.
Lakini hiyo yenu ni balaa, yaani jamaa anakua personal na kubeba stories kwenye flash disk akizunguka nazo kulazimisha media waanike, halafu hata stori yenyewe haimuhusu yeye binafsi. Hivyo hamna sehemu ametajwa, analazimisha stori ya mhubiri ili aanikwe.
 
Kwani brother hujaisikia report ya CAG kuhusu allocation ya pesa katika sekta tofauti....
so far naona sekta ya ujenzi ndio inapokea pesa nyingi kuliko sekta nyinginezo na kwa kuwa allocation haiiangalii bajeti iliopangwa na bunge hivyo,suala hili haliepukiki

Magufuli simlaumu kwa maana naona anashindwa kutofautisha kati ya ukuaji wa kiuchumi na maendeleo ya kiuchumi, pia kama sivyo bhasi kuna shabaha yake anayoilenga ambayo pengine inakuwa ngumu kwetu kumuelewa
 
Nilidhani kenya ndiyo itakayokuwa inaongoza, sijawahi fikiri kenya inaweza kuwa second kwenye kitu chochote hapa EA.
 
Kiukweli umeuliza maswali ya msingi lakini watu watajitia upofu kwa kuwa ni jukwaa la kenya lakini ni hekima kulichambua hili suala kwa mapana.....

Kuna matumizi mabovu ni ukweli haswaa yanayoendelea chato kwa kuwa hayana faida kwa taifa lakini kuna mengineyo kama kuhamia dodoma kwangu ninaiona ni movement nzuri ili kuondoa centralization ya kiuchumi na kiserikali na pia kuiendeleza central corridor ya nchi

Kuhusu madaktari kutokuajirika ni upuuzi mkubwa na ni aibu kwa nchi yetu kutoweza kuajiri watu wa sekta muhimu kwa taifa letu....
Kinachohitajika

Serikali inatakiwa kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma kwa kuvutia uwekezaji maana demand ipo kubwa lakini supply ni ndogo

Serikali inatakiwa kupunguza restrictions na mlolongo wa uanzishwaji wa vituo vidogo vya afya

Pesa ya kutosha ielekezwe katika sekta ya afya
 
Jana nimesikia Uhuru akitetea swala la Kenya kupata madaktari kutoka Tanzania!!

Ila wabongo mjue hatutafuti daktari wale, hujidai wanatibu Mapenzi, sijui kupata mme au Kazi, Maana hata sahi ndio hayo mabangio yamezidi kuanzia namanga hadi kitengela, eti Daktari Kutoka Tanzania... na tibu, Mapenzi ........ hatutaki hao
 
Hutaki wewe wenzako wanataka.
 
Nilidhani kenya ndiyo itakayokuwa inaongoza, sijawahi fikiri kenya inaweza kuwa second kwenye kitu chochote hapa EA.
[emoji81] [emoji81] [emoji81] [emoji81] inashindwa kwa vitu vingi tu mbona.
 

..asante kwa mchango wako mzuri.

..nakubaliana na wewe kwamba serikali yetu kushindwa kuajiri madaktari ni uzembe.

..natofautiana na wewe kuhusu suala la kuhamia Dodoma.

..kama tunataka Central corridor na Dodoma ziendelee basi tulenge kwenye sekta ya uchumi ambayo inashirikisha wananchi wengi wa maeneo hayo.

..kwa mfano, tungeweza kuwekeza ktk sekta ya zabibu na uzalishaji wa wine/mvinyo. Au, tungeweza kuwekeza ktk sekta ya mifugo kwa kuanzisha viwanda vya ngozi na kusindika nyama. Nakumbuka zamani kulikuwa na nyama toka Kongwa Dodoma, ukienda bucha unanunua kongwa steak.

..kwa hiyo maoni yangu, kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa Dodoma na Central corridor ni njia bora zaidi ya kujenga uchumi wa eneo hilo na kuinua kipato cha wananchi kuliko kujenga ikulu na kupeleka makao makuu ya wizara za serikali.

NB:

..nimeangalia miji mikuu kama Washington DC, Berlin,Ottawa, Moscow, New Delhi, yote haiko katikati ya nchi zao. Kwa hiyo dhana kwamba mji mkuu ukiwa katikati ya nchi tunapeleka serikali/huduma karibu na wananchi inawezekana haina mashiko sana.
 
joka kuu na nguruvi sielewi kwa kweli kwa nini mnapinga kufufuliwa kwa ATCL, kama kungekuwa na mbadala wake ningejaribu kuelewa ila kutoa lugha tu nyepesi eti kufufuliwa kwa ATCL ni kukosa vipaumbele inaonyesha una msukumo wa kisiasa.

Sote tunafahamu umuhimu wa usafiri wa anga kwa utalii, ukiacha tu utalii ndio inachangia sehemu kubwa ya GDP yetu pia ndio inayoingiza pesa nyingi ya kigeni. Tz usafiri wa anga unaonekana kama anasa kwa sababu hakuna ushindani mzuri na mashirika yote bado ni madogo. Tusiiangalie ATCL kama nembo ya taifa tu, tuiangalie kama nyenzo muhimu ya kuboresha mazingira ya utalii na usafiri wa anga, je kwa jicho hilo kwako ni kutokuwa na kipaumbele ?

Suala la makao makuu kuwa Dodoma lilishaamuliwa zaidi ya miongo minne iliyopita, huu ni utelekelezaji tu. Muda unavyozidi kwenda na ndivyo gharama za kuhamia Dodoma zinaongezeka, hata kama Magu asingehama saivi, yupo ambaye angekuja kuhamisha baadaye kwa gharama kubwa saivi. Kupanga ni kuchagua, cha muhimu pesa yetu popote inapoenda inatumika vizuri na kuna value for money.
 
Suala la madaktari lina kahistoria yake, ndio maana mwaka jana waliajiri baadhi kwa vituo vyote vipya vya afya kama Mlonganzila, vile vile serikali imeshasema itachukua madaktari 450 mwaka huu, ila hii haiwezi kuondoa surplus iliyopo mtaani.

Tatizo la sekta ya afya si la leo na wala haliwezi tatuliwa kwa siku moja na naona kama linaanzia kwenye sera huko, watanzania walio na bima ya afya bado ni wachache sana, sekta binafsi ndio inabidi iwe kiungo mkubwa kwa afya kwa mijini. Hauwezi kuajiri madaktari wakati hauna sehemu ya kuwapeleka, kuwaruhusu kwenda Kenya ni uamuzi wa busara kwa muda huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…