Hata baada ya "Kujitawala" sisi wenyewe, bado tuendelee tu kulaumu mfumo? Haiwezekani tukasema sisi tunataka kufanya mambo tofauti kidogo tuonavyo inafaa sisi wenyewe?
Ninajua jibulako mkuu, usihangaike kunijibu hilo swali nililouliza hapo.
Ngoja nitumie muda kidogo kutumia hoja yako hii, nami kuweka ninachoamini juu ya hali yetu hii tuliyomo.
Binafsi ninaamini lawama hasa inaanzia kwetu sisi wenyewe na viongozi wetu wanaotuongoza katika awamu mbalimbali, na hasa hasa hizi awamu za miaka hii ya karibuni.
Tunashindwa hata kufanya mambo madogo madogo yaliyomo katika uwezo wetu, kubadili hali zetu, na badala yake tunasubiri mikopo kama hii, inayojadiliwa hapa.
Wananchi wengi wanaoishi ndani ya nchi yetu sasa hivi ni zao la uhuru wa nchi yetu, wengi wamesoma shule zilizoanzishwa na sisi wenyewe, lakini zikashindwa kuwapa uwezo wa kutumia akili ya kutumia nyezo zilizo katika uwezo wao kubadili mazingira yao. Hata vyoo vya mashimo, inakuwa ni tatizo kwetu, kweli?
Zahanati na vituo vya afya vimejengwa huko vijijini, lakini hatuna uwezo wa kuvifanya vifanye kazi kwa ufanisi. Hatujiulizi inakuwaje?
Kilimo chetu kwa sehemu kubwa ni kilekile alichotuachia mkoloni! Mkulima ambaye amesoma kwenye shule tulizoziendesha sisi wenyewe, hajabadilika, miaka sitini? Tunasubiri mikopo,kama hii, na inapopopatikana, hatujui inakopitia?
Hapo mwanzo, baada ya uhuru, tulisema kukosa watu wetu wenye elimu na utaalam katika mambo mbalimbali ilikuwa ni kikwazo kwetu.
Watu wakasomeshwa, tena kwa wingi na kwa gharama kubwa. Leo hii sidhani kuna eneo ambalo hatuna watu walilolisomea ndani ya nchi hii, lakini huoni kazi za hawa watu, sana sana itakulazimu uende ndani ya CCM, na utawakuta wamejazana huko, wakifanya yao yanayowafaa wao wenyewe, na siyo kunufaisha taifa.
Viongozi wetu sasa wameamua, kwamba sisi hatuwezi kuleta maendeleo katika nchi hii, kwa hiyo njia sahihi na bora iliyopo, ni kuagiza watu toka nje, waje watuletee maendeleo!
Hakuna kiongozi anayetaka kufanya kazi na wananchi hawa, kuwatia moyo na kuwahimiza wajiletee maendeleo ya kweli. Wananchi nao sasa wanawasikiliza viongozi wao, wakisubiri waletewe maendeleo, huku raslimali za nchi yao zikizolewa kama takataka!
Sasa acha tusubiri maendeleo, miaka sitini mingine inayofuata toka sasa! Sijui kama bado utakuwa upo kuyafaidi hayo maendeleo, au vipi mkuu 'BloodofJesus'?