Tanzania yapata Mkopo wa Dola Mil 278 kutoka Benki ya Dunia

Daah!
 
Naona mimi na wewe "tunazunguka mlemle tu" mkuu wangu 'Blood of Jesus', tunalalamikaaaaa, na hakuna tunachoweza kubadili.

Ninaamini, Katika yote haya tunayolalamikia, tungeweza kuyaweka pembeni na kuamua kufanya hata hicho kidogo kama tungekuwa na VIONGOZI wenye maono ya kuelewa tunatakiwa kufanya nini ili tujisitiri kwa kiasi tuwezacho sisi wenyewe kwa nguvu zetu.

Hakuna sababu ya kupambana na haya mapapa ya dunia, lakini tungeweza kufanya yetu bila kuyaamusha hayo mapapa yatushughulikie kama yalivyomshughulikia Mugabe.

Ninajua kuna njia nyingi za kuwahamasisha wananchi wafanye kweli katika maendeleo yao katika maisha yao ya kila siku, na kuweza kubadili hali zao za maisha kama viongozi wangeamua kulisimamia hili kwa umakini mkubwa.

Na wala sisemi kujitenga na yeyote duniani, la hasha, bali kujua jinsi ya kufanya mambo yetu kutimiza malengo ya nchi yetu bila ya misuguano isiyokuwa na lazima kuwepo.
 
Huu mkwamo sio mdogo mkuu, labda fanya halahala Mungu akupe chance ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi labda kuna ambalo litatokea kama unavyoamini.
 
Bora ya Samia mara 100000 kuliko yule sadist wenu aliyekuwa anakopa kimyakimya ...na kuhonga wapinzani wamuunge mkono
Kwamba kwa akili yako Samia yeye wapinzani hawaongi? Au unafikiri Zitto na Mbowe wako kimya kwa sababu wanamuogopa sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…