Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

Tanzania yapokea Msaada wa Dawa ya kufubaza COVID-19 kutoka Madagascar

Je kwao wana case ngapi na vifo vingapi na wangapi wameponaa
baadhi ya wachangiaji sijawaelewa kabisa
mzungu ametuweza sana sisi wa africa yaani kuaminiana wenyewe kwa wenyewe ni kama haiwezekani kabisa
dawa imepatikana angalau ya kuonyesha njia watu wanabeza
wanataka dawa mpaka itangazwe na WHO hahahaaaa
midawa yenyewe unakuta ni midonge/misindano inayoambatana na ma hallucination ya kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninashauri Serikali wangeileta hiyo dawa kimya kimya na kuwapa wagonjwa waliopo Amana na sehemu zingine afu wasubiri matokeo. Kama itaonekana inatibu kweli hiki kinachoendelea sasa ndio kifuate
 
Ebu tuacheni kejeli au kwa kuwa nduyu yako haujamkumba huu ugonjwa.Covid ni hatari inapiga kama koboko lazima kutumia silaha yoyote kwa sasa.Kuna watoto wadogo wameshakuwa yatima tunavyoongea sasa hivi.
 
Kwa kweli awamu hii wamelitia aibu Taifa ....... Aibu hii itachukua miaka na miaka kuisafisha!!

Mzee Mwanakijiji, lini utaleta utetezi wako? Jamaa yako inaonyesha kabisa hana leadership skills. Ameshindwa kuhudhuria kikao cha EAC na kashindwa kuitisha crisis meeting ya SADC hata kuhudhuria pia......!!
Taifa la kipumbavu huchagua kiongozi mpumbavu!
 
Bandugu habari za jioni.

Mimi nawapa taarifa tu ya kuwa mzigo umeshaingia toka kwa ndugu zetu wa kisiwa cha mbali, kwa Rojuelina. Nadhani umepokelewa na mnayemuona anapiga dose yake kabisa. Kama utani vile.

Sina maelezo mengi picha zinajieleza.

Take care, corona kills.
 

Attachments

  • IMG-20200508-WA0008.jpg
    IMG-20200508-WA0008.jpg
    48.4 KB · Views: 2
  • IMG-20200508-WA0010.jpg
    IMG-20200508-WA0010.jpg
    56.9 KB · Views: 2
  • IMG-20200508-WA0009.jpg
    IMG-20200508-WA0009.jpg
    67 KB · Views: 2
Tanzania inatafuta shortcut ya kutatua matatizo ya msingi, hivi Serikali inafikiri nchi nyingine ni wajinga kuendelea kupima watu wake na kuchukua hatua ngumu dhidi ya Covid19 na badala yake na wao waagize dawa kutoka Madagascar?
Unaongelea jiwe ambaye alifunga safari siku kadhaa akaenda kupanga foleni loliondo kupata kikombe cha babu, huyu mzee unaweza muaminisha kinyesi kinatibu akasema kila mtu ale
 
Naona Kabudi ameenda kuchukua ARV za Corona. Yani ndege ya Rais imeenda kuzurura huko huku marais wenzake wakiwa bize kuumiza vichwa kuhusu Corona. Sasa unaletaje dawa wakati maabara inahakikiwa?

Huyu mzee kwakweli ni mzigo usiobebeka.
 
kama kweli corona imetengenezwa basi kwa afrika mashariki Tanzania ndio itakuwa imeteuliwa kuwa uwanja wa mauti kwa7bu bbc wanasema Madagascar kwenyewe saizi maumbukizi yameongezeka kwa kasi.

Sent from my SM-G975F using Tapatalk
 
baadhi ya wachangiaji sijawaelewa kabisa
mzungu ametuweza sana sisi wa africa yaani kuaminiana wenyewe kwa wenyewe ni kama haiwezekani kabisa
dawa imepatikana angalau ya kuonyesha njia watu wanabeza
wanataka dawa mpaka itangazwe na WHO hahahaaaa
midawa yenyewe unakuta ni midonge/misindano inayoambatana na ma hallucination ya kutosha
Hehehe tatizo ni akili yako finyu, dawa sio lazima iletwe na wazungu, swala ni mbona dawa haina proof, yaani hana proof hata moja kua inatubu anasema tumuamini tu kua inatibu huku ye mwenyewe nchi yake ipo kwenye lockdown hadi leo. Unadhani hao wazungu unaowachukia wangepata dawa leo hii wangekua kwenye lockdown? Watu hua sijui akili mnaweka wapi. Bila shaka na wewe unaamini kikombe cha loliondo
 
Ndo kwanza ata azija tua chato kwa uchunguzi zaid ..maana mahabara ime hamia chato
 
Back
Top Bottom