Tanzania yashika nafasi ya sita kwa kuwa na masikini wengi zaidi Duniani

Yaani hadi Congo wametuzidi? kweli Tanzania ni maskini, sijapenda
 
Humo kwenye hiyo data hao maskini ni sisi tu waislamu au na makafir wamejumuishwa maana uku mtaani tunaambiwa sisi waislamu ndo maskini na makafir ndo matajiri
 
Kwamba wengi tunaishi chini ya dola moja kwa siku,dola moja ni Tsh 2600,bando GB 1 ni 2100 na tupo online daily watu 40+m,hizo tafiti za kipuuzi tu,dola moja unaishije tz?
Watu 40 Mil kati ya 60 Mil wako online? Tanzania ina watu 60 Mil. Kati yao 30 Mil ni under 18. Unasemaje watu 40 Mil wako online.?

Hizi data za Online zinapatikanaje? Au mimi mwenye line 3 nahesabika watu watatu?
 
Huu ni upumbavu.
Nchi ina madini ya kila aina! Nchi ina mito mikubwa na midogo, mabwawa, maziwa makubwa, bahari, mbuga za wanyama, ardhi nzuri yenye rutuba, na nguvu kazi ya kutosha!

Kwa nini tutambulike kama nchi masikini? Wanasiasa wachache wa ccm wanaona ufahari kwao na familia zao kuishi maisha ya kifahari! Kuingia mikataba ya hovyo na wageni ili wazifaidi raslimali zetu! Huku wananchi walio wengi wakiishi kwenye dimbwi la umasikini!

Hii ni laana ambayo itasababisha vizazi vijavyo kuja kuyapiga fimbo makaburi yetu.
 
📌

It is worse than I thought.

An absolute disaster.

This is what happens when leaders could not care less that their own citizens are suffering. They have normalised pain and oppression to the extent that they probably find those figures acceptable. To them it is just numbers, they do not feel empathy for the millions of lives that struggle everyday just to survive.

The millions of Tanzanian lives that it is the Government of Tanzania’s responsibility to care for, nurture, protect, respect, and even love.
 
IPo kwenye mitandao, sio jambo jipya. Takwimu za benki ya dunia zinaonyesha kuwa watanzania 4 kati ya kumi ni mafukara.

Ufukara huu unapimwa kwa kipato. Hawa wanaishi chini ya dola tatu kwa siku. Pili, wanaangalia hali ya lishe, upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya nk.

Umaskini mkubwa zaidi uko maeneo ya vijijini ambako asilimia 31 ya kaya zinaishi chini ya kiwango cha umaskini, huku kanda ya ziwa na magharibi zikiongoza.
 
Kwa Tanzania mikoa inayochangia ni ifuatayo
Dodoma,Singida,Simiyu,Mwanza,Tabora,Geita,Lindi,Pemba,Kagera sio kwamba hawa watu ni wavivu wa kufanya kazi hapana bali wamekosa msaada wa kiuzalishaji kwani wanazalisha mazao yanayohitaji mtaji wa kutosha na technolojia.Dodoma zabibu bado hazijazalishwa kwa kuwango cha Dunia tukiwa serious Dodoma inaweza kunywesha Tanzania nzima na Africa,Singida vile vile.Kanda ya Ziwa pamba imesalitiwa na politicians.Badala ya kuzalisha ajira inazalisha chawa wa kiwango cha kimataifa.Mkoa wa Njombe unatakiwa utumike kama case study kwa sababu ya ubunifu wa kilimo unaosaidia kuondoa umasikini japo serikali bado iko nyuma kuwezesha miundo mbinu na viwanda.Misitu na chai vilipoyumba kidogo watu wakaja na Parachichi fasta imesaidia kuongeza mzunguko wa fedha,Viazi vya mvua vilipozingua watu wakabuni umwagiliaji fasta.
Serikali pia na yenyewe iache anasa bado serikali inafanya matumizi makubwa sana yanayofanya fedha za kigeni zinapotea bure kwa matumizi na safari zisizorasmi
 
Weka na orodha ya nchi zdnye matajiri wengi afrika.

Itagundua kwenye matajiri wakubwa kuna masikini wengi
 
🛑🛑Sufuria ya kupika DATA za uongo! IPO kenya, any one can cooks any data he will, its easy with mobile,you can do that!🛑🛑
 
Kwamba wengi tunaishi chini ya dola moja kwa siku,dola moja ni Tsh 2600,bando GB 1 ni 2100 na tupo online daily watu 40+m,hizo tafiti za kipuuzi tu,dola moja unaishije tz?
Mbona ulichoongea wewe na wao ni sawa. Kama watu 40M wanaishi juu ya dollar 1, waliobaki ambao ni zaidi ya 25M wapo chini ya dollar 1. Kitu ambacho ni sawa huo utafiti umesema watu 23.9M. Kumbuka nchi yetu ina watu zaidi ya 65M.
 
Hapo wameangalia idadi ya watu. Inawezekana nchi zingine ni masikini sana ila zikawa na population ndogo. Mfano somalia inakadiriwa kuwa na watu 20.5M. Hao wote wakiwa masikini haijazidi idadi ya watu masikini kwa Tanzania ambao ni 23.9M. Kwahiyo bado Tanzania itahesabika kuwa na idadi kunwa ya watu masikini
 
hawa watu wamezingatia vigezo gani maana kuna nchi zipo kama kuzimu sudan kusini, Eritrea, burundi, malawi gaza na nyingine nyingi zina hali tete sana
 
Tanzania inaaskini wengi tutembee. Mimi nakubaliana na huo utafiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…