Tanzania yasisitiza: Hatujavunja Sheria, tunatekeleza majukumu yetu kama Taifa Huru

Hii ilikuwa lini alipo "ufyata mkia na kunyamaza"?
Au ni wewe uliziba masikio?
Jambo liongelewe leo unataka na impact yake uione leo leo mkuu?

Matokeo ya jambo lolote huonekana baada ya muda.
 
Ili kuondoa sintofahamu,

CDM itaachwa ishike dola.
Sisi wapenda Demokrasia, hatutaki ushindi wa upendeleo ama ushindi wa kubebwa, tunataka viongozi watokane na ushindi halali wa kura za uchaguzi.

Mambo ya uchaguzi yakiwa huru na haki, kiongozi yeyote, awe wa Ccm, Cdm ama chama chochote atakayepita kwenye tanuri la uchaguzi, huyo ni wetu, tutamuunga mkono 100%.
 
We jiulize, kiongozi ni wa 3 baada ya Yesu & Muhammad kama 1 wao alivomtukuza, ana xifa hizo anazoimbwa kuwa nazo, anazarau ripoti rasmi za kumsaidia kazi ili kleta maendleo ya wa2 wake, watu wanafanyiwa madhila ya kila namna, yy yuko bize na magoli ya timu ...nk. Utamwitaje mtu huyo!?
 

Ngoja tuone ila kuelekea mjadala tu maelewano yakaanza kuonekana. Kwani nani anataka Shari?
 
Una hoja ila hicho kiiinglishi mtihani!
 
Tutafika tuu!
 
Tunasemaje mabeberu wasitupangie sisi ni taifa huru tunafanya vile tunavyotaka tukiamua kuifuta chadema sawa kwahyo tusipangiwe wao c wana nchi zao
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi msimamo wake kuhusu hali ya kisiasa nchini, ikisisitiza kuwa hakuna sheria yoyote iliyovunjwa katika utekelezaji wa majukumu yake kama taifa huru linalozingatia utawala wa sheria.

​

Akizungumza na wahariri jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema kuwa serikali imekuwa wazi na ya uwazi kuhusu masuala yote yanayohusu mwenendo wa kisiasa nchini. “Hatujavunja sheria yoyote ile na tumeendelea kuzingatia sheria,” alisema Balozi Kombo.

Kauli hiyo imekuja kufuatia sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani, baada ya vyombo vya dola kumshikilia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na shtaka la uhaini.

Lissu alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 10, 2025.

Katika hatua nyingine, Waziri Kombo amewataka wanadiplomasia wanaowakilisha mataifa yao nchini kuheshimu masharti ya Mkataba wa Vienna.

Amesisitiza kuwa hairuhusiwi kwa wanadiplomasia kufika mahakamani bila kibali rasmi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje, akieleza kuwa ni muhimu kufuata taratibu za kidiplomasia kama ilivyoainishwa katika mkataba huo wa kimataifa.

Aidha Serikali imeendelea kusisitiza kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, na kwamba haki na taratibu zote za kisheria zitafuatwa ipasavyo kwa kila mwananchi, bila kujali nafasi yake ya kisiasa na Kijamii.
 
Tanzania lazima ikubali kwamba kuna mikataba ya kimataifa inayolinda haki za kiraia na binaadam ambayo tanzania ni sehemu ya mikataba hiyo,hivyo akiienda tofauti na ilivyo ni lazima awajibike. Huwezi kusema wewe ni taifa huru wakati unakiuka mikataba ya kimataifa.
 
mnataka kuficha nini huko mahakamani?

endesheni mahakama ya wazi ili kama TAL ananyongwa hadi kufa wote tuone mmefikiaje hio hukumu

sio mtu mmoja magogoni sababu ya kuogopa uchaguzi huru na wa haki, ndo anashinikiza wenzake wanyongwe ili abakie yeye

kama CCm mliridhia hayo ni ya kwenu hayatuhusu ila hii nchi ya kwetu sote lazima tuilinde kwa wivu mkubwa
 
Jambo liongelewe leo unataka na impact yake uione leo leo mkuu?

Matokeo ya jambo lolote huonekana baada ya muda.
Inawezekana hukuelewa nilicho kuuliza. Ni wazi kuwa hata hiyo "kuufyata mkia" uliitumia tu bila uhalisia wake.

Hivi hujui mtikisiko uliosababishwa na IMF na World Benki kwa uchumi wa dunia wakati huo, mtikisiko uliotokana na yale yale yaliyokuwa yakipingwa na Mwalimu Nyerere?
Ni rahisi kwetu leo hii kuja humu na kupotosha watu; kwa kujuwa kuwa hawana kumbukumbu zozote ya yaliyotokea wakati huo.
 
Labda nikuulize, Nyerere angeliweza kugomea kuishusha thamani Shillingi ya Tz, je thamani isingelishuka kweli?

Sipotoshi mtu, hapa tunajadili tu jinsi watu tulivyoyapima mambo kwa wakati ule.

Kwa sababu masharti aliyoyagomea, ndiyo Mwinyi alikuja kuyatekeleza, tena kwa muda mfupi sana na kufungua 'soko huria' baada ya kuona kwamba hilo ni hitaji la kidunia, hasa kwa watu wanaotembeza bakuli kama sisi.

Hapo wajuaji wa mambo waliona kuwa Nyerere kalinda 'ligasi' yake, lakini mambo aliyoyasimamia, alijua fika kuwa asingeliweza kuyazuia.
 
..kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa, kwa kuangalia damu zilizotapakaa eneo alipotekwa, bila shaka Mdude alipaswa kufikishwa hospitali. Kwa kweli inatia wasiwasi sana kwamba Mdude hajaonekana tangu alipotekwa.
Nasikia ameonekana Arusha kwa Lema 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…