Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zenye mishahara mikubwa Afrika

Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zenye mishahara mikubwa Afrika

Wametoa hizi data kwa bibi yao Twaweza siyo bure aiseeeeh.

Naona watakuwa , wamechukua mishahara ya wakurungezi wa private sector wanaolipwa hadi Tshs 30 millions kwa mwezi na kuchukua anayelipwa elfu 30/= kwa mwezi kisha wakapata wastani wa hiyo laki 9/=.

Ndiyo wamefikia, hapo kwenye 900,000/=

Vinginevyo tutatafuta mchawi .
 
Huu utafiti ulitakiwa uwe na mfumo kama huu,
Madakitari.
Polisi.
Waalimu
Wauguzi.
Uvuvi.
Ardhi na kadhalika na siyo kutoa utafiti wa jumlajumla kama mazombi yalonywesha chang'aa usiku kucha
 
Mimi najua rais mzalendo ni Mujika wa Urugui, wengine wote uzalendo maslahi tu! We unalala bure, chakula bure, usafiri bure, elimu ya watoto bure, bima bure, ulinzi bure, muziki bure, hewa bure, packing bure, mavazi bure, matibabu bure, halafu mshahara 30m+, halafu tukuombee sala bure, looh. Hivi Mungu wa Ibrahim, wa Isaka, wa Yakobo ndio huyo wa huyu? Ndio wakwetu? Ndio wa wale wa kimara?
 
Kwenye kampuni nyingi za hiyo conclusion huwa wanaipata wapi? Kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi kilichotangazwa na serikali ni Tsh 100,000(laki moja) hizo laki tisa wanalipwa watu gani wa kawaida? Mtoa mada atakuwa amepigwa chenga na kilugha kilichotumika kumfikishia taarifa hiyo! Mshahara wa laki sita ni wa mameneja!
Naweza kukubaliana na mleta uzi. Katika nchi yetu, kuna gap kubwa sana ya mishahara. Ni kwa sababu tu watu wa kawaida huwa hatufuatilii haya mambo. Wakati kuna watu wanalipwa sh 200,000 kwa mwezi, kuna mabosi wao hapo hapo wanalipwa milioni 15 au 20 kwa mwezi, pamoja na stahili nyingine kibao. Kwa hiyo ukichukua wastani, data ya wastani wa Sh 900,000 kwa mwezi inaweza kuwa sahihi.
 
Nani huwa anafanya analysis ya wage bill kwenye serikali yetu? Nina hakika asilimia 5 tu ya watumishi wa ngazi za juu (Kuanzia wakurugenzi wasaidizi, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa kisiasa na wastaafu) ndio wanaokula 70% ya wage bill hiyo.

Trust me on this one. Tatizo ni kwamba hakuna wa kumfunga paka kengele. Salary gap kati ya kada za kawaida na kada za uteuzi, na nafasi za kisiasa ni unbearable! Na bado watu hao hao ndio wanaopewa magari, nyumba, maji, umeme na simu bure. This is absurd.....
 
Nani huwa anafanya analysis ya wage bill kwenye serikali yetu? Nina hakika asilimia 5 tu ya watumishi wa ngazi za juu (Kuanzia wakurugenzi wasaidizi, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa kisiasa na wastaafu) ndio wanaokula 70% ya wage bill hiyo. Trust me on this one. Tatizo ni kwamba hakuna wa kumfunga paka kengele. Salary gap kati ya kada za kawaida na kada za uteuzi, na nafasi za kisiasa ni unbearable! Na bado watu hao hao ndio wanaopewa magari, nyumba, maji, umeme na simu bure. This is absurd.....
Hakika mwenye nacho anaongezewa mkuu.
 
Hiyo Laki tisa wanalipwa Tanzania ipi nami niende huko? [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
What about the cost of living si ajabu tukawa wa kwanza kwenye kuangalia gharama za bidhaa na huduma za jamii, matokeo yake mfanyakazi Algeria anaepokea sh 650000 akawa na maisha bora kuliko mtanzania anaepata 900000
 
Limeuliza watumishi wa umma kweli?

Yawezekana wakawa wameuliza mashirika binafsi tena ya kimataifa na ma NGO ya kimataifa.

Wametembelea kweli viwanda vya wahindi, makambuni ya wachina, wahindi, wabongo wenyewe kama Sahara Media Group?

Je wameuliza watu wa aina gani hao? Au ma CEO wanaolipwa milioni 40 kwa mujibu wa Rais Magufuli.

Sina imani na huo utafiti. Hawana tofauti na TWASHINDWA ya Tanzania.

Eti kaweka wastani(average) TZS 900,000.00.tunataka aseme kati ya wafanyakazi 670,000 hivi ni wangapi wanapata chini ya tzs 300,000.00 na kama siyo zaidi 40% ya watumishi wote na atuambie kama sio kweli 15% ya watumishi wote ndio wanaolipwa 50% ya wage bill,

Kama wakuu wa idara wanalipwa wastani wa TZS 4,500,000.00 (mshahara na posho zitokanazo na ajira) kiasi hiki ni mara 15 ya mtumishi anayelipwa TZS 300,000 p.m hapa cha mtoto kwa yule anayelipwa 15,000,000. ni mara 50 ya 300,000.00,nasema tumrudishie akatafiti upya aje na utafiti bora zaidi.
 
Mh!
Hizo takwimu za Tanzania zina walakini.
 
Ndio mana Lisu anaropoka akipata kioja kutoka nje kinachohusu nchi yetu. Huo mshahara wa laki Tisa ni ndoto. Degree holder anayeanza kazi hapati hiyo hela
 
Inawezekana mshahara wa bosi mkuu umechangia average yetu kupanda.

Marais wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Afrika. Top ten in (TZS).

1. John Pombe Magufuli
5th President Tanzania
Born: Tanzania 1959
Married
Children: 5
Annual: TZS 422,136,637.00
Monthly: TZS 35,178,053.00
Weekly: TZS 8,118,012.00
Daily: TZS 1,156,539.00

2. Robert Mugabe
President Zimbabwe
Born: 1924 Zimbabwe
Married
Children: 3
Annual: TZS237,451,858.00
Monthly: TZS 19,787,655.00
Weekly: TZS 4,566,382.00
Daily: TZS 650,553.00

3. Uhuru Kenyatta
President Kenya
Born: 1961 Kenya
Married
Children: 3
Annual: TZS 352,435,114.00
Monthly: TZS 29,369,593.00
Weekly: TZS 6,777,598.00
Daily: TZS 965,576.00

4. Ellen Johnson Sirleaf
President Liberia
Born: 1938 Liberia
Children: 4
Divorced
Annual: TZS197,876,549.00
Monthly: TZS16,489,712.00
Weekly: TZS 3,805,318.00
Daily: TZS 542,128.00

5. Jacob Zuma
President South Africa
Born: 1942 South Africa
Married
Children: 20
Annual: TZS 598,026,903.00
Monthly: TZS 49,835,575.00
Weekly: TZS 11,500,517.00
Daily: TZS 1,638,430.00

6. Alpha Condé
President Guinea
Born: 1938 Guinea
Married
Children: 1
Annual: TZS 48,369,823.00
Monthly: TZS 4,030,819.00
Weekly: TZS 930,189.00
Daily: TZS 132,520.00

7. Archibald Lesao Lehohla
Lesotho's Deputy Prime Minister and Minister of Home Affairs and Public Safety and of Parliamentary Affairs
Born: 1946 Lesotho
Married
Children: 2
Annual: TZS 52,923,195.00
Monthly: TZS 4,410,266.00
Weekly: TZS 1,017,754.00
Daily: TZS 144,995.00

8. José Eduardo dosSantos
President of Angola
Born: 1942 Angola
Married
Children: 7
Annual: TZS 178,253,791.00
Monthly: TZS 14,854,483.00
Weekly: TZS 3,427,958.00
Daily: TZS 488,367.00

9. Yayi Boni
President of Benin
Born: 1952 Benin
Married
Children: 5
Annual: TZS 64,386,830.00
Monthly: TZS 5,365,569.00
Weekly: TZS 1,238,208.00
Daily: TZS 176,402.00

10. Edgar Lungu
President Zambia
Born: 1956, Ndola, Zambia
Married
Children: 6
Annual: TZS 123,123,186.00
Monthly: TZS 10,260,265.00
Weekly: TZS 2,367,754.00
Daily: TZS 337,324.00

Salary Survey South Africa – Online Wage, Pay Survey at Mywage.co.za
toa uongo wako hapaaaa
Top 10 Highest Paid African Presidents Listed | IT News Africa – Africa's Technology News Leader ingia hapo uone

Ngw'ana Kabula
 
A to Z Kilichopo Arusha ndio kiwanda kinachoongoza kwa wafanyakazi wengi Tanzania kima cha kwanza cha mshahara ni Tsh. ngapi? wangeuliza kwanza hapo
 
Back
Top Bottom