Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zenye mishahara mikubwa Afrika

Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zenye mishahara mikubwa Afrika

ya wafanyakazi nchini Tanzania wapo kwenye sekta ya kilimo kama njia kuu ya kuwasingizia kipato. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Tanzania ime
nimecheka kidogo
 
Naweza kukubaliana na mleta uzi. Katika nchi yetu, kuna gap kubwa sana ya mishahara. Ni kwa sababu tu watu wa kawaida huwa hatufuatilii haya mambo. Wakati kuna watu wanalipwa sh 200,000 kwa mwezi, kuna mabosi wao hapo hapo wanalipwa milioni 15 au 20 kwa mwezi, pamoja na stahili nyingine kibao. Kwa hiyo ukichukua wastani, data ya wastani wa Sh 900,000 kwa mwezi inaweza kuwa sahihi.
Just note! Mshahara wa kawaida ni ule ambao unalipwa kwa wafanyakazi wa kawaida! Huyo anayelipwa milioni 15 ni wa kawaida kweli?
 
Just note! Mshahara wa kawaida ni ule ambao unalipwa kwa wafanyakazi wa kawaida! Huyo anayelipwa milioni 15 ni wa kawaida kweli?
Wa kawaida na asiye wa kawaida ndiyo nini tena hicho mkuu?
 
Kwa mishahara hii haturudi ng'oo.

Hata ukianzisha biashara, hakuna clientelle

Wacha tupige hela ya maana viwanja vikubwa tu.

Sent from my Kimulimuli
 
1. Huu ni uongo wa siku
2. Kima cha chini kwenye sekta nyingi hakifiki 300,000. Je hizo laki tisa zinatoka wapi????
3. Si kweli "Zaidi ya nusu ya wafanyakazi nchini Tanzania wapo kwenye sekta ya kilimo kama njia kuu ya kuwasingizia kipato". Labda wangesema sekta ya Elimu.
4. Japo wanasema tafiti hupigwa na tafiti, ila hii pumba.
 
Hili shirika ni la kupuuzwa sana.
Tanzania hiihii kuna watu wanalipwa mpaka elfu 90 kwa mwezi.
Au wamechukua sample kwenye mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Tz?
 
Tuwe makini na hizi takwimu. Baada ya kusoma hilo imebidi nipembue kidogo.
Mshahara sio issue pekee. Tuangalie bei za vitu. Nimechukua mfano wa kilo ya sukari. Angalia huo mshahara, na bei ya kilo kwa baadhi ya nchi6

Tanzania / 900,000 / 2500 +
Zambia/ 3,300,000 / 1,309
Mauritius / 1,500,000 / 1,670
Ghana / 700,000/ 1,400

Kwa mwendo huu, wapi Kuna nafuu?
Kwa vyovyote vile, ni ghali sana Tanzania. Au kwa lugha nyepesi ni ngumu zaidi kumudu maisha Tanzania kwa mshahara
Hapo kwa wawemba hapo pako vizuri sana
 
Muongo ww laki Tisa bongo kima cha chini kweli???
 
Hiyo laki 9 ni mshahara wa familia au wa mtu mmoja mmoja?
 
Exactly. Mi nipo kuna rafiki yangu yupo Zambia mshahara wa serikalini kwa kiwango cha chini ni kwacha 4800! Ambayo ni kama milioni moja kwa mwezi. Hao ni walimu wa primary.
Yawezekana wakawa wameuliza mashirika binafsi tena ya kimataifa na ma NGO ya kimataifa.
 
Mishahara ya wabunge+Baba Ubaya ndo yameleta hicho kiwango..



Ni heri ulipwe laki 3 lakini ununue sukari kilo 1 kwa sh.200 kuliko laki 9 halafu sukari sh2500+!
 
Back
Top Bottom