Tanzania Yatumbukia Rasmi Kwenye Mtego wa Udini

Tanzania Yatumbukia Rasmi Kwenye Mtego wa Udini

Kwa macho ya kawaida, Tanzania inaonekana shwari. Lakini kwa waliopasua pazia la unafiki, hali si ya kawaida tena. Udini umejitokeza waziwazi, tena kwa ushawishi wa kutisha.

Mawaidha ya Eid mwaka huu yameacha majeraha ya kihisia kwa baadhi ya viongozi wa dini nyingine, waliodai kuwa wamepingwa na kulengwa kwa maneno makali na kejeli.

Kwa bahati mbaya, hata Rais Samia Suluhu Hassan ameonekana kuwa muhanga wa chuki hizi za kidini. Wapo wanaompinga si kwa sera zake, bali kwa sababu ya dini yake. Hawasemi moja kwa moja, lakini kauli zao zinaonesha mzizi wa ubaguzi. Hawamtaki Samia kwa sababu sala zake hazifungwi kwa maneno yao. Hii ni hatari kwa Taifa.

Na kama hiyo haitoshi, Shehe Ponda kujiunga na chama cha siasa wakati huu kumeibua maswali mengi.

Amedumu miaka mingi kama kiongozi wa dini asiyeegemea upande wowote wa kisiasa kwa nini sasa?

Je, kuna mkakati mpana unaoibuka kama jibu kwa mashambulizi ya kifikra dhidi ya Waislamu?

Rafiki zangu, huu si wakati wa kupumbazwa na maneno matamu ya kidini.

Tuamke na tuchuje kila tunachosikia.

Tukumbuke: dini si silaha ya kumdhalilisha mwingine. Na Mungu wetu hawezi kupenda chuki kwa jina lake.

Tufumbue macho. Tuseme ukweli. Tukiwa tunatazamana usoni.
Sio jambo la ajabu wala Mara ya kwanza, kenge wa ccm kutumia dini kuwagawa wabongo, Kipindi cha Mkapa, IGP Omary mahita, alitumika Sana kueneza propaganda za kidini kuhusu CUF, ikasemwa CuF imeingiza kontena za mapanga kuua wakristo, hii ni baada ya kuona wa Islam wamekimbilia CUF, kwa sasa hv, kwa yanyoendelea Salama ya Samia ni kuegemea kwenye dini yake, na kuuonyesha ukristo, na wakristo kwamba wanampinga kwa vile ni muislam!na kwa upeo mdogo wa, elimu wa wabongo, dini "will be the straw which will break the camel back" Kamba hu katika pembamba
 
Uwezo mdogo hii hoja inataka akili kubwa
Wewe unaamini hivyo?
Hoja ya kuwaa na uchaguzi ambao wapiga kura wanatakiwa kuwa na HAKI na UHURU wa kumpigia kura mtu wanayemtaka wao, hili linataka mtu awe na "akili kubwa" kulielewa?

Kama hawa watawala tulio nao sasa wanalikataa hili, kwa vile tu wao "wana uwezo mdogo" wa akili kulielewa jambo rahisi namna hii; sasa tuwategemee kuwa na uwezo wa jambo gani tena?
 
Back
Top Bottom